Global publisher5 watudanganya picha ya aliyekuwa na marehemu kamanda barlow

mwila

Member
Oct 17, 2012
38
10
Global Publishers watumia picha feki na kudai ni mwanamke aliyekuwa na Kamanda Barlow


*Blogger Stella Tillya (Tanzanite Glamor) amegundua picha fake ambayo mtandao maarufu wa full udaku, uzushi, umbea, upashkuna, ushambenga na ushankunpe, unaoitwa Global Publishers, umeitumia kuudanganya umma. Mtandao huo umeweka picha ya mwanamke na kudai anaitwa Doroth Moses, na ndiye aliyekua na marehemu Kamanda Liberatus Barlow usiku aliouawa na kwamba mwanamke huyo “anajua mengi!” USHAHIDI: Kuona stori hiyo, gonga link ifuatayo: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/kuuawa-kwa-rpc-huyu-anajua-mengi

K itu cha kusikitisha na kuchekesha kwa wakati mmoja ni kwamba mwanamke huyo si Mtanzania, si Mwafrika, na pengine hajui hata kama kuna nchi inaitwa Tanzania. Mwanamke huyo ni Mmarekani ambaye picha yake hiyo imetumika katika website ya nchini humo, katika makala inayozungumzia unene wa wanawake(wa USA) weusi. USHAHIDI: Kuona makala hiyo, click link ifuatayo: http://thegrio.com/2012/07/06/study-obesity-in-black-women-linked-to-childhood-abuse/.
*
Angalia picha mbili hizo chini. Ya juu kutoka Global Publisher, na ya chini ni original photo.
Hivi wamefikia vipi huko!? Yaani jamaa wanatafuta random photos kwenye intaneti, kuzifanyia photoshop na kudanganya kwamba ni wahusika wa matukio fulani yanayodaiwa kutokea Tanzania!? Au?


*Picha kwenye stori ya Global Publishers website, inayodai mwanamke huyo “anajua mengi” kuhusu marehemu Kamanda Liberatus Barlow na kifo chake
 
daah hawa jamaa leo nimewashushia heshima yao saana yaani looh wapaka matope mno
 
Back
Top Bottom