GLOBAL HUNGER INDEX: Kiwango cha njaa chazidi kupungua nchini Tanzania nakala kwa Zitto

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,052
28,242
Screenshot_2017-10-13-12-25-58.png
Kiwango cha njaa nchini kimeendelea kupungua kulinganisha na miaka kadhaa ya nyuma.

Hii ni kwa mujibu wa Utafiti wa Taasisi ya GHI ambayo imetoa ripoti ya mwaka 2017.

Ikumbukwe kuna baadhi ya wanasiasa wakiongozwa na Zitto walitaka Rais atangaze hali ya hatari kisa upungufu wa chakula ilihali uhalisia wa mambo ni tofauti.

Katika Afrika Mashariki Tanzania imetanguliwa na Kenya huku pia cha kuvutia ni Kuipita Nchi ya India na Ethiopia ambazo tunakimbizana nazo kwa kasi ya ukuaji wa uchumi.
 
Wengi wanaponzwa na kuwa na familia kubwa. Kule vijijini unakuta mtu ana umri mdogo ila tayari ana watoto lukuki wakati hata shughuli za kumpatia riziki hazieleweki...
Ili kupunguza njaa, inabidi kila familia iwe na idadi ndogo ya watoto ambayo wataweza kuitunza na kuipatia lishe nzuri....
 
Taja exactly hivo viwango vya njaa vya mwaka huu na mwaka uliopita...

Just because kiwango cha njaa 'kinaweza' kikawa kimepungua, haimaanishi ndo kulikuwa hakuna upungufu mkubwa wa chakuka
Nimeattach screenshot hapo juu
 
Wengi wanaponzwa na kuwa na familia kubwa. Kule vijijini unakuta mtu ana umri mdogo ila tayari ana watoto lukuki wakati hata shughuli za kumpatia riziki hazieleweki...
Ili kupunguza njaa, inabidi kila familia iwe na idadi ndogo ya watoto ambayo wataweza kuitunza na kuipatia lishe nzuri....
Zamani watoto walikuwa wanazaliwa wengi ili kuwa nguvukazi
 
Zitto muongo sana jimboni kwake wanashindia udaga mlo ambao unamadini ya ubishi.
 
View attachment 608381 Kiwango cha njaa nchini kimeendelea kupungua kulinganisha na miaka kadhaa ya nyuma.

Hii ni kwa mujibu wa Utafiti wa Taasisi ya GHI ambayo imetoa ripoti ya mwaka 2017.

Ikumbukwe kuna baadhi ya wanasiasa wakiongozwa na Zitto walitaka Rais atangaze hali ya hatari kisa upungufu wa chakula ilihali uhalisia wa mambo ni tofauti.

Katika Afrika Mashariki Tanzania imetanguliwa na Kenya huku pia cha kuvutia ni Kuipita Nchi ya India na Ethiopia ambazo tunakimbizana nazo kwa kasi ya ukuaji wa uchumi.

Mkuu kwa takwimu hizo bado hali si nzuri,Taifa lililojibainisha kuwa lina zaidi ya watu 80% wanaotegemea kilimo lilipaswa kuwa kinara katika orodha hiyo,kama uchumi wetu unategemea zaidi kilimo,tunapaswa kujiuliza kwa nini tuwe na njaa?
 
Ni kweli unavyosema lakini Trend inaashiria tunaelekea kuzuri kutoka kubaya.

Hiyo inaendana na Juhudi za Serikali na wadau mbalimbali.
 
Hiyo improvement siyo kazi ya JPM. Score ya mwaka ni product ya sera za at least miaka mitano ya nyuma. Kuimprove access to mbegu bora, barabara nzuri vijijini, huduma za ugani sio kazi ya miaka miwili paaaaaaaaap.
JPM atakuwa assessed at least after five years!
 
Zitto muongo sana jimboni kwake wanashindia udaga mlo ambao unamadini ya ubishi.

Acha dharau,kama serikali haijawekeza vya kutosha katika upatikanaji wa mbegu bora na pembejeo zote,mkulima masikini atawezaje kujikimu kupitia kilimo duni chenye kuutweza hadi utu wake?

Kula mihogo si dhambi,ulaji/ulimaji wa baadhi ya mazao unatokana na jiografia ya mahali husika,sasa kama ardhi ya Buha inastawisha zaidi mihogo,kwa nini isilimwe?Baada kuilima ulitaka ifanyweje kama si kutumika kama chakura?
 
Back
Top Bottom