Giza na Nuru havitangamani

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,474
37,745
Nianze kwa kukiri, naamini katika Ukristo na hivyo mifano yangu itaegemea kwenye kitabu chao Biblia. Katika Waraka wa pili wa Paulo kwa Wakorintho 6:14, Mtume Paulo anawaasa Waamini wa Kanisa la Korintho kwamba hakuna Ushirika kati ya Giza na Nuru. Akimaanisha huwezi kuwa mtu wa haki kama unapenda dhuluma, huwezi kumpenda Mungu kama Unampenda shetani, lakini kikubwa zaidi huwezi Kupenda IBADA kama unapenda MATAMBIKO.

Tanzania ni nchi isiyo na dini kama Taifa lakini lenye wananchi wanaoabudu katika dini na madhehebu mbalinbali. Dini kubwa zikiwa Uislamu na Ukristo na wachache Wabudha, Wapagani nk. Miaka ya karibuni kumekuwa na desturi ambapo viongozi wa dini mbili hizo za Uislamu na Ukristo wamekuwa wanaalikwa kwenye mikutano na sherehe kubwa za Kitaifa na kutanguliza maombi kwa Mungu wa mbinguni kwa maelezo kwamba wanaliweka taifa mikononi mwa Mungu.

Ili kuepuka kuchanganya Nuru na Giza hakuna mahali Wapagani wamewahi kuitwa kuja kutambika hadharani uwanja wa Taifa kuonesha taifa linathamini utamaduni na dini za asili za Mtanzania.

Ni wazi na wala halihitaji uchunguzi kujua kwamba Machifu wa asili wa kiafrika wanaabudu katika matambiko na shughuli zao hazina mahusiano yoyote ya kiibada na Mungu anayeabudiwa na Waislamu na Wakristo. Katika Uislamu na Ukristo matambiko ni HARAMU na CHUKIZO mbele za Mungu, lakini mila na dezturi za Machifu matambiko ni sehemu muhimu katika ibada zao za sirini na hadharani.

Sasa swali langu kwa viongozi wa juu wa nchi hii ambao wote ni aidha Waislamu au Wakristo, haya matamasha ya waabudu mizimu mnayoyaandaa yamehalalishwa na dini zenu mnazoswali/sali au mnalipotosha Taifa makusudi ili liadhibiwe na Mungu mnayemwabudu ambaye anachukizwa na matambiko?

Au viongozi wa dini wa viongozi hawa mmewaruhusu waumini wenu kuhidhuria matamasha ya mizimu kwa vile kuna Uhuru wa kuabudu nchini? Kwa Muislamu safi kuvikwa vazi linalotumika kuabudu mizimu ni sahihi kwa vile ni Uhuru wake?

Je, viongozi wetu hamuoni hatari ya kuchanganya Taifa katika Giza na Nuru kwa kuwaaminisha wamlilie Mungu wa Ukristo na Uislamu kisha taifa linaamuriwa kuungana na Machifu kuomba Mizimu?
 
Utatumia nguvu nyingi sana za bure ili kuhoji serikali kama inafuata maadili ya dini. Serikali yoyote ipo kwa ajili ya ku-win influence ya watawaliwa (raia wake) ili waiunge mkono na kushirikiana itimize ajenda zake za kisiasa na kitawala.

Mengine yote (mema na mabaya) yanaratibishwa na kutumika kama chambo na njia na msaada na nyenzo za kutimizia LENGO LAKE HILO. Umeelewa sasa?
 
Utatumia nguvu nyingi sana za bure ili kuhoji serikali kama inafuata maadili ya dini. Serikali yoyote ipo kwa ajili ya ku-win influence ya watawaliwa (raia wake) ili waiunge mkono na kushirikiana itimize ajenda zake za kisiasa na kitawala.

Mengine yote (mema na mabaya) yanaratibishwa na kutumika kama chambo na njia na msaada na nyenzo za kutimizia LENGO LAKE HILO. Umeelewa sasa?
Wala sijaluelewa Mkuu. Ningekuelewa kama viongozi wetu wasingekuwa na dini na wasingetuhimiza kumwomba Mungu mmoja wa mbinguni alibariki Taifa na kuliokoa na majanga. Leo unaita viongozi wa dini kesho unakusanya Watambikaji halafu unasema serikali inataka kuwin influence za watawaliwa? Kwa faida ya Nani? Ya kikundi kidogo wakati wanaliangamiza Taifa Kwa kulifungamanisha na matambiko ya kishetani?
 
Huwezi, kutumikia mabwana wawili lazima atamtii mmoja mwingine atakuwa mbeba mizigo ,hapo tunadanganyana hapo anatumikiwa mzimu MUNGU achanganywi na kitu chochote, hapo nchi inawekwa kwenye kiringe ama kwa makusudi au lazima.
 
Kichwa kinaanza kufikiri kabla hata sijazaliwa uwepo wangu haukutabiliwa kama nitakuwepo hapa duniani; Hawa waliotuletea hizi dini ambazo tunaziamini na kuzifuata walikuja tu kutuletea kwa lengo la Umungu kweli au walikuja kufanya Biashara =yaani matatizo ya matumbo yao
 
Back
Top Bottom