"Girlfriend" na "Boyfriend", je Watanzania tunayatumia vizuri maneno haya?

Penguini

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
377
293
Rafiki ni rafiki tu, awe wa kike au wa kiume ni rafiki; "we are friends" basi!

Ila kwa kuseparete jinsia zao kunajenga kitu kingine yaani urafiki wa kijinsia. Haya ni maneno ya kizungu yaliyotokana na tabia zao ingawa siamini kama wanayatumia maneno hayo kama sisi na ndipo napata swali.

Je, tunapoyatumia sisi waafrika ni sawa?
Na hasa watanzania.

Je, kuna Mila desturi au utamaduni wa kabila lolote la tanzania inayosapoti maneno hayo ya kizungu au ni uzungu umeingia kwetu na hivyo kila mwenye kuiga ya kizungu anaweza kuiga?
 
Hili binafsi naona tofauti ipo kati ya rafiki (friend) na girlfriend au boyfriend....mfano girlfriend si kwamba ni rafiki wa kike hivihivi tu hapana ni zaidi ya rafiki nashawishika kusema kuwa si waafrika au wazungu kwa sasa sote girl friend au boy friend is more than a friend ingawa haya majina awali hayakuwa na maana kama ya sasa yaani wapenzi hususani kwa vijana...
 
Kuelewa ni kipaji, watu tunatofautiana UWEZO wa kuelewa, kama wewe hujaelewa usiseme eti haiekeweki, sema huelewi, maana hata bubu anaeleweka
Shida yako ni moja kwamba wewe ni mmoja wa waumini wa maneno hayo kwa hiyo umeona kama naharibu!
Ninachosema -- Lucky One hapo juu kakigusa moja kwa moja --
Nikufupishie wewe mwenye shida ya kuhesabu vijiti ujue mbili jumlisha mbili!
Maneno hayo "Girlfriend" na "boyfriend"

1: ni aibu ktk familia zenye maadili
2: siyo utamaduni wa makabila yetu watanzania
3: ni DHAMBI!
kwa hiyo, kama tuna haja ya kulinda maadili ya familia zetu tunapaswa kupiga vita kwa nguvu zote Maneno hayo na matokeo yake!
 
Back
Top Bottom