Gini Wijnaldum mwanzo na mwisho wa total football ya Rinus Michels

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,691
Miaka ya 1970 pale Amsterdam Uholanzi, alikuwepo binadamu mmoja wakuitwa Rinus Michels, binadamu huyu alituletea kitu kipya kwenye soka
.
Michels kama kocha hakutaka mchezaji wa namba moja pekee, alitaka mchezaji wakucheza namba hata 8 uwanjani, hii inaitwa Universality inayopatikana kwenye Total football, YES ni soka la Waholanzi
.
Sahau kuhusu Philp Cocu aliyeweza kucheza namba zote kasoro kipa na right back, nataka upate mfano wa mnyama mmoja wa kuitwa Ruud Gullit, yule Ballon d'or winner wa 1987
.
Gullit wa Uholanzi alicheza kama namba tisa au 10, akishirikiana na Marco Van Basten, ila pale Milano alicheza 10 ila alipoanzia soka pale Haarlem alikuwa ni centre back, huyu alikuwa blueprint ya kwanza ya Michels
.
Miaka mingi imepita soka lao limebadilika pale Uholanzi, ila tuna mtu mmoja kutoka Rotterdam, Gini Wijnaldum huyu pale PSV alicheza kama 10 aliweka kambani mabao 57, akishirikiana na Memphis Depay bishoo mmoja hivi
.
Gini alipokuja EPL pale Newcastle United, alitumika kama winga chini ya Steve McLaren, alifanya makubwa sana pale St James Park, Klopp alivutiwa sana na ubora wake
.
Wakati dunia inalia uhaba wa total footballers, Gini bado anatuonesha kitu, pale Anfield game kama 16 amecheza kama kiungo wa ulinzi 'holding midfielder', pale pia ametumika kama namba 8, kufanya operation ya ulinzi na attack, ni mboni ya Klopp kwenye transition zote ndani ya uwanja
.
Gini bado pale Anfield hucheza pia kama namba 10, japo sio free kama pale Uholanzi, pale Liverpool ile roaming huifanya sana Roberto Firmino, ila pia hucheza pale
.
Gini akiwa na timu ya taifa kocha Ronald Koeman humtumia kama deep lying forward, sehemu ambayo kocha anaamini ndipo sehemu yake sahihi kabisa fundi huyu ni team player na mwenye kipaji cha hali ya juu sana, ana killer instincts, dhidi ya Estonia nadhani tuliona Hatrick yake
.
Wakati dunia inajitahidi kuisahau Total football, ni Gini au mtoto wa Gini wanaweza kuendelea kutupa burudani hii, sisi huku mtaani tunamuita 'Jini Adamu'

Huko kwenu si bado ule mchezo wa Kocha hajanichezea kwenye namba yangu au sio wazee

jr_farhanjr-20191201-0003.jpeg
 
Kwenye mpira kuna mashujaa wasioimbwa hasa huyu jini adamu wengine ngolo kante,Sergio busquets kwa kizazi hiki ila vya nyuma kuna makelele,sedof,okocha na wengine kibao
 
Huyu jamaa ni engine muhimu sana ya klopp ,anaifanya midfield ya Liverpool iwe compact sana.
Mimi Chelsea ila kwa hili nimekubali ulichosema.mpambanaji Hana makuu yeye kazi tu.na roho yake ya upambanaji.apewe u kaptain
 
#aaron
huyu kiumbe kwang huwa namuona kama alonso hana mbwembe yeye ni mpra tuu.nataman sana angekuwa pale kwenye timu ya arsnl nngejivunia mno
 
Kweli huyu jamaa ni fundi sana! Anajua kufunga, anajua kuzuia na pia anajua tena sana kuchezesha timu! Natamani mmasai OGS amlete OT!
 
Box to Box Midfielder.

Ana uwiano sawa wa kushambulia na kukaba. Huwa na mtu asiyeimbwa lakini anafanya mambo yana click tu. Ni ngumu kumuona kwa jicho la kawaida. He is underrated

Hongera leo kwa kumkumbuka!
 
Gini wijnaldum , kwa mara ya kwanza sikumuelewa klopp kutoa zile £25m kwa huyu mwamba , ila leo naweza kusema newcastle utd waliibiwaa..
 
Back
Top Bottom