Faith Luvanga
Member
- Aug 21, 2018
- 14
- 15
Baraza la Sanaa nchini Tanzania (BASATA) limemfungia kwa muda wa miezi sita (6) msanii wa Muziki wa Bongo Flava Gift Stanford Joshua maarufu kama Gigy Money, kwa kile kinachodaiwa kuwa msanii huyo alipanda jukwaani kutumbuiza katika tamasha la Wasafi Tumewasha Tour lililofanyika Jijini Dodoma Uwanja Jamhuri, kisha akavua gauni (dela)na kubaki na vazi ambalo lilikuwa linaonyesha maungo yake mwili na hivyo kuudhalilisha utu wake na kubughudhi hadhira ya wapenda sanaa ndani na nje ya Tanzania.
Adhabu hiyo imetolewa na Baraza hilo kupitia Taarifa yake kwa Umma ikieleza kuwa Kitendo hicho alikifanya huku akifahamu kuwa tukio linarushwa mubashara na televisheni ya Wasafi na kuonwa na watu wa rika mbalimbali na hivyo kwenda kinyume na Kanuni za Baraza za mwaka 2018.
Baraza limesema kuwa limejiridhisha kuwa msanii huyo alikiuka maadili ya kazi za sanaa kwenye Tamasha husika na kukiuka kifungu 4(L) cha Sheria NO. 23 ya mwaka 1984 (Re:2002), Kanuni 25 (6) (9) ya kanuni za Baraza za mwaka GNN.43/2018 na taratibu za uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini.
Baraza limefafanua kuwa msanii huyo alishaitwa mbele ya Baraza na kuonywa mara kadhaa kwa vitendo vya ukiukwaji wa maadili na kuahidi kutorudia tena. Kutokana na ukiukwaji huo wa Sheria, Kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini, Baraza limemfungia kujihusisha na shughuli za sanaa kwa kipindi cha miezi sita(06) ndani na nje ya nchi na kulipa faini ya shilingi za Kitanzania Milioni moja (1,000,000/=) kwa kosa hilo. Adhabu hii imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 64(1) (a)-(i) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za mwaka 2018.
Mwisho wa taarifa yake Baraza hilo limewakumbusha wasanii wote nchini kufanya shughuli za Sanaa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu.
>> Pia Soma: Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara