Giang Quoc Nghiep na Giang Quoc Co: Makaka walioweka rekodi ya dunia ya kupanda ngazi 90 mmoja akiwa kichwani kwa mwenzie

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,743
4,272
guiness2.jpg


Makaka wawili mashababi waliweka rekodi ya dunia mnamo Disemba 22 mwaka 2016 baada ya kupanda jumla ya ngazi 90 mmoja akiwa kichwa chini miguu juu kichwani mwa mwenzie.

Makaka hao, Giang Quoc Nghiep na Giang Quoc Co walipanda ngazi zilizopo kwenye kanisa la St. Mary's huko Girona Uhispania kwa muda wa sekunde 52 tu.

Rekodi iliyowekwa na ndugu hao ilivunja rekodi iliyokuwepo ya kupanda ngazi 25 iliyowekwa na Tang Tao na Su Zengxian wa China iliyowekwa mwaka 2014.

Akiongea na Taasisi ya Rekodi za Dunia ya Guiness, mmoja wa ndugu hao ambao ni wacheza Sarakasi, alisema walifanya mazoezi ya zoezi hilo kwa miaka 15 na kupata ajali kadhaa na majeraha katika safari yao.
 
Back
Top Bottom