Ghorofa refu duniani lapambwa kwa rangi za bendera ya Kenya siku ya Jamhuri

ormystatus

Member
Nov 3, 2019
88
176
Usiku wa jana wa Disemba 12, wakenya wengi hawakuamini macho yao pale walipoweza kuona bendera ya taifa lao iki angaza kwa dakika tatu kwenye ghorofa refu zaidi duniani lililopo Dubai, Burj Khalifa katika maadhimisho ya Jamhuri Day. Jumla ya rangi nne za bendera ya Kenya ziliweza kushuhudiwa kwenye ghorofa hilo ambazo ni Nyekundu, Nyeupe, Nyeusi na Kijani.

Kenya imekuwa ikisherehekea sikuku ya Uhuru wa taifa hilo kila ifikapo Disemba 12, ambapo kwa hapo jana iliadhimisha miaka 56.

Inadaiwa gharama ya kurusha tangazo kwa dakika tatu (3), Burj Khalifa inafika Shilingi milioni 156 za Kitanzania.

Hata hivyo haijawekwa wazi kama Kenya ililipia tukio hilo. Inadaiwa ndani ya dakika tatu (3) itakugharimu kiasi cha Shilingi milioni 156 za Kitanzania ili tangazo lako kuonekana kwenye ghorofa hilo refu zaidi duniani kuanzia muda wa saa 2:00 usiku hadi 4:00 wakati wa wikiendi.

Na katikati ya wiki inafikia milioni 292, kama tangazo lako litaonekana ndani ya dakika tatu pekee. Hivyo ukitaka tangazo lako lionekana lazima uhakikishe umejipanga.

IMG_20191213_191837.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1291471
Ushamba unawasumbua ndio maana mnashangaa. Hapo katika ghorofa la Burji al Khalifa ni jengo la kitalii kwahivo karibu nchi zote huwekwa picha za bendera za nchi zao kama unavojua Dubai ndio kioo cha utalii duniani hivi sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Appreciate tu walichofanya Wakenya buda, sisi bado ni malimbukeni wa haya mambo tutasema ni matumizi mabaya ya fedha.
 
Punguza kutumia makwapa kufikiria, yaani hadi mtu ambaye hajaenda shule anaweza kungamua na kuona hakuna faida yoyote hapo,
At least wangeweka labda kivutio chochote cha utalii lakini bendera tu 😂😂😂
hata wangeweka picha ya Mlima Kilimanjaro iliyochukuliwa vizuri na maridadi kutoka Amboseli National Park pia bado ungelia tu na kusema hamjatendewa haki
 
Google pia walikuwa na 'doodle' ya bendera ya Kenya kwenye homepage yao hiyo jana. Kisha wakatoa maelezo kidogo kuhusu maana ya neno Jamhuri. Kiswahili tutaendelea kukieneza tu, hata kama jamaa wa domo domo hawatapendezwa.
kenya-independence-day-2018-5339362391752704-law.gif
Hiyo ilikuwa kenya tuu bro,
 
Usiku wa jana wa Disemba 12, wakenya wengi hawakuamini macho yao pale walipoweza kuona bendera ya taifa lao iki angaza kwa dakika tatu kwenye ghorofa refu zaidi duniani lililopo Dubai, Burj Khalifa katika maadhimisho ya Jamhuri Day. Jumla ya rangi nne za bendera ya Kenya ziliweza kushuhudiwa kwenye ghorofa hilo ambazo ni Nyekundu, Nyeupe, Nyeusi na Kijani.

Kenya imekuwa ikisherehekea sikuku ya Uhuru wa taifa hilo kila ifikapo Disemba 12, ambapo kwa hapo jana iliadhimisha miaka 56.

Inadaiwa gharama ya kurusha tangazo kwa dakika tatu (3), Burj Khalifa inafika Shilingi milioni 156 za Kitanzania.

Hata hivyo haijawekwa wazi kama Kenya ililipia tukio hilo. Inadaiwa ndani ya dakika tatu (3) itakugharimu kiasi cha Shilingi milioni 156 za Kitanzania ili tangazo lako kuonekana kwenye ghorofa hilo refu zaidi duniani kuanzia muda wa saa 2:00 usiku hadi 4:00 wakati wa wikiendi.

Na katikati ya wiki inafikia milioni 292, kama tangazo lako litaonekana ndani ya dakika tatu pekee. Hivyo ukitaka tangazo lako lionekana lazima uhakikishe umejipanga.

View attachment 1291469

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujinga mwingine wa majirani zetu...
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom