Ghorofa lapolomoka watu 15 hawajulikani walipo

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
27,545
29,791
7495fb05fdd9886ea361e6f3e02cbffe.jpg
Jengo la ghorofa saba limeporomoka mjini Nairobi na watu 15 hawajulikani walipo,
Bado juhudi za kuwa tafuta zinaendelea

========== APDATE==========

juk.jpg


WATU watano, wakiwamo mama na wanawe watatu bado kupatikana baada ya jengo la ghorofa saba kuporomoka Kware, Embakasi, limesema Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya.
Tayari viongozi mbalimbali wametuma pole zao kwa aila zilizoathirika.

Wanasiasa mbali mbali wakiwamo walio mamlakani Kaunti ya Nairobi na wanaomezea mate viti tofauti vya kisiasa kaunti hii wamejifikisha katika jumba lililoporomoka usiku wa Jumatatu Kware, Pipeline mtaani Embakasi jijini Nairobi na kutoa hisia zao kuhusiana na mkasa huo.

Mwakilishi wa wanawake Kaunti ya Nairobi Bi Rachael Shebesh na anayewania kuhifadhi kiti chake Agosti 8 kwa chama cha Jubilee, amesema wamiliki wa majengo ambayo yalitajwa na halmashauri ya kushughulikia ujenzi wa nyumba na usalama (NCA) kuwa yanafaa kubomolewa wanafaa kuheshimu agizo hilo ili kuepuka visa vya ubomokaji wa nyumba kama ilivyoshuhudiwa Jumatatu usiku Kware Pipeline, awali mtaani Huruma Nairobi na Roysambu Kasarani.

"Wakati halmashauri inayoshughulikia ujenzi na usalama wa nyumba inapokuagiza ubomoe jumba lako, unafaa kufuata maagizo hayo bila kuyapuuza. Maisha ya binadamu ni ya muhimu kuliko majengo hayo. Hiki ni kisa cha 6 majengo ya nyumba kuporomoka kando na mkasa kuu wa Huruma uliosababisha maafa ya wapangaji mwaka uliopita," akasema Bi Shebesh Jumanne wakati akihutubu alipofika kwenye eneo la mkasa wa jumba hilo lenye ghorofa 8.
Mwaka 2016 jumba la mtaa wa Huruma Nairobi lililoripotiwa kuporoka lilisababisha zaidi ya watu 50.

Bi Shebesh aidha amewataka wapangaji kuhama nyumba ambazo NCA ilidokeza zinafaa kubomolewa kwa sababu ya usalama wa wakazi kwa kujengwa vibaya.

"Si wajibu wa serikali kila wakati kuchunga maisha yako ilhali wewe hutaki kuyachunga, hata wewe mpangaji una wajibu mkuu wa kujali na kuchunga maslahi ya maisha yako," akasema mwakilishi huyu wa wanawake kaunti ya Nairobi.
"Umefikia wakati wetu sisi kama wapangaji pia kujali maisha yetu wenyewe.

Ninashauri wanaohusika na jukumu la kuhamisha walioathiriwa wasijenge kambi hapa kwa sababu za kiafya zinazotokana na uchafu, wawapeleke kwenye majumba mengine yaliyo salama," akasema Bi Shebesh akiwatuma risala zake za pole kwa waathiriwa na kuwatakia afueni ya haraka waliojeruhiwa.

Mwaniaji wa kiti cha ugavana Kunti ya Nairobi Peter Kenneth kwa tiketi ya kujitegemea ambaye pia alifika katika eneo hilo la mkasa ambapo mashirika ya kuokoa watu na kutoa msaada yanaendelea kufukua jengo hilo, amesema kuna haja ya kuchukua hatua mahususi dhidi ya nyumba ambazo ziliorodheshwa kubomolewa.

"Kwanza ninasema pole kwa walioathirika na tunatumai watu sita (ingawa idadi hiyo sasa ni watu watano) ambao hawajaonekana watapatikana.

Orodha ya majumba yasiyofaa Nairobi ichukuliwe tena na hatua ya kuyabomoa itekelezwe. Huwa tunakashifu mikasa kama hii inapofanyika japo hatuchukui hatua ya kuzuia isitendeke tena," akasema Kenneth.

Gavana wa Narobi Dkt Evans Kidero, mwaniaji wa kiti cha wanawake Nairobi kwa chama cha ODM Esther Passaris ni miongoni mwa viongozi na wanasiasa waliofika kwenye mkasa huo.

Kufikia sasa takriban watu watano ndio wameripotiwa kuwa hawajapatikana.
Jumba hilo linakisiwa kuwa na zaidi ya wapangaji 100.

Kufikia leo Jumanne mchana, watu 121 walikuwa wameshapatikana katika mchakato huo wa uokozi.
 
7495fb05fdd9886ea361e6f3e02cbffe.jpg
Jengo la ghorofa saba limeporomoka mjini Nairobi na watu 15 hawajulikani walipo,
Bado juhudi za kuwa tafuta zinaendelea
Ilipaswa iwe.......
Watu 15 wahofiwa kufukiwa na sehemu ya jengo lililo anguka
 
Back
Top Bottom