Ghorofa hili ni mkombozi wa Mtanzania au gheresha tu.............?????

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
ghorofa.JPG

Jengo la ghorofa la matofali mabichi kama lilivyonaswa na mpigapicha wetu katika kijiji cha Msafiri kilichopo Bungu wilayani Rufiji jana. Ni hatari, lakini salama.
 
Ardhi tunayo nyingi lakini uwezo wa kuitumia na kuzalisha kihaswa hatuna sasa kwa nini mtu ujitese na ghorofa la udongo na mti wakati ardhi ni ya bwerere?
 
Hilo labda ni la maonyesho, akilala humo aombee upepo usivume, litageuka kuwa kaburi la pamoja na mkewe!
 
Maisha bora kwa kila mtanzania.Structural engineer sijui ni nani vile....
 
Cha kusikitisha Choo cha shimo kipo mita 20...kutoka kwenye Skyscrapper hilo...au hakipo kabisa ukiomba kwenda wapewa JEMBE...
 
hivi hizo hela si angeinvest kujenga nyumba ya kawaida yenye uimara na usalama?
 
Hiyo ndo nguvu ya uthubutu. Anafaa kupongezwa huyo na kutiwa moyo. Laiti tungekuwa na wataalam wazuri, huyo angesaidiwa mbinu za kuboresha maisha yake akiwa humuhumo kwenye mazingira yake. Kama wengine wanajenga gorofa za mabox (mbao tu na makaratasi) kwa nini yeye asijenge ya matofali mabichi?
 
Nimewahi kuishi Rufiji, vibanda vya aina hii huitwa Madungu, hivi ni vibanda vinavyojengwa mashambani kwa ajili ya ulinzi wakati wa kilimo(waweze kuona mbaali) lakini pia kujilinda na wanyama wakali hasa ukizingatia wamepakana na Selous Game Reserve.
 
Back
Top Bottom