Ghorofa 100 Dar bomu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Ni bora yavunjwe haraka sana ili kuwanusuru Watanzania kutopoteza maisha yao ndani ya maghorofa hyo bomu.

Ghorofa 100 Dar bomu
Shadrack Sagati, Dodoma
Daily News; Friday,June 27, 2008 @19:01

Zaidi ya maghorofa 100 jijini Dar es Salaam yamebainika kuwa yalijengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge limeelezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa, kati ya maghorofa 505 ambayo waliyakagua, 147 yalikutwa hayana nyaraka za ujenzi.

Lowassa aliunda tume baada ya jengo la Hoteli ya Chang’ombe Village Inn, Keko, Dar es Salaam kuanguka mwaka 2006 na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa. Ilidaiwa kwamba ulikuwapo ukiukwaji katika ujenzi wake.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia Bunge kuwa tume hiyo ya Lowassa, ilibaini kuwa ukaguzi huo, pia maghorofa 81 yalikutwa yamekiuka masharti ya ujenzi huku maghorofa mengine 22 wenyewe hawakupatikana na yalikuwa yamejengwa bila kuzingatia sheria za ujenzi.

"Can you imagine, mtu kaamua kupandisha ghorofa lake hapo bila kufuata taratibu za mamlaka husika, hii ni hatari kubwa," alisema Pinda wakati anatoa majumuisho ya hotuba ya matumizi ya ofisi yake bungeni kwa mwaka 2008/09.

Panda alisema maghorofa mengi yanayojengwa Dar es Salaam yanajengwa holela bila kufuata taratibu za ujenzi, hivyo kuyafanya kuwa hatari kwa maisha ya binadamu. Alisema kama hatua za haraka hazitachukuliwa na serikali, kuna hatari ya watu wengi kupoteza maisha kwenye maghorofa hayo ambayo yanachipuka kama uyoga katikati ya Dar es Salaam, likiwamo eneo la Kariakoo.

"Tatizo ni kubwa…kuna hatari ya kupoteza maisha ya Watanzania wengi zaidi kuliko hili lililotokea juzi kama tukiendelea kuwaachia Manispaa suala hilo," alisema Waziri Mkuu. Alisema tukio la kuporomoka kwa ghorofa kulikotokea wiki iliyopita Kisutu, Dar es Salaam, ni uzembe wa baadhi ya watendaji wakiwamo wahandisi wa manispaa husika.

Alisema kutokana na taarifa hiyo ya tume, serikali inaandaa utaratibu mzuri wa utekelezaji wake kuhakikisha maghorofa yanayojengwa yanakuwa bora yanayofuata taratibu zote za ujenzi. Sambamba na suala hilo, alisema serikali pia inaangalia uwezekano wa kuingia katika Jiji la Dar es Salaam, kwani imegundulika kuwa manispaa haziwezi kuachiwa kuendeshwa jiji hilo lenye shughuli nyingi za uchumi.

"Ni lazima serikali tuingilie kati, Dar es Salaam haiwezi kuendeshwa na manispaa, lile ni jiji ambalo ni kioo cha taifa letu," alisema Pinda. Alisema serikali inaangalia mfumo bora wa uendeshaji wa jiji hilo, baada ya kuonyesha mfumo wa sasa wa kuwa na manispaa tatu umeshindwa kupata mafanikio.

Pinda pia ameliambia Bunge kuwa serikali imekubali kutenga Sh bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Itigi kwenda Tabora. Alisema maeneo mengine yataendelea kufanyiwa upembuzi yakinifu ili miradi iliyopo sasa ikitekelezwa, ujenzi wa barabara hiyo uanze mara moja.
 
wanavyoliionglea hili suala ni kama vile wanamwambia mtu umepata virusi vya ukimwi hiyo ishi kwa matumaini, yaani una muda mrefu wa kujiandaa na kubadili tabia. hii ni hatari nilifikiri wangeshughulikia mapema iwezekanavyo, wabomoe hizo ghorofa. huo muda wa kukaa na kujadili hilo bungeni wangekuwa wameshafanya mambo mengine ya maana sana juu ya ghorofa hizo.
 
Tatizo La Nchi Yetu Kila Kitu Ni Siasa, Na Ukishaweka Siasa Ukasahau Utaalamu Ni Bureee. Hayo Magorofa Yanayozungumziwa Siyo Kuwa Yalijengwa Chini Ya Kiwango, Hayakufuata Utaratibu Wa Kawaida Kama Nuilding Permit.kama Yalijengwa Chini Ya Kiwango Yangekuwa Yameshadondoka.

Hiyo Tume Ya Lowasa Ilikuwa Inachunguza Nini? Sana Sana Ni Makaratasi. Hakuna Aliyechukua Concrete Tester Aka-drill Ukuta Kuona Ubora Wa Zege.

Niwatoe Hofu Wana Jf, Hizo Ni Siasa, Jengo Linalojengwa Chini Ya Kiwango Haliwezi Kudumu Throuht The Full Seasons. Ikja Mvua Moja Tu Linakwenda Na Maji.
From Day One, When The Building Is Erected, It Normally Undergo Settlement, Until It Finally Settled, Once Settled No Problem, Lakini Kama Kuna Tatizo Litaonekana Very Vividly. Angalieni Historia Ya Majengo Yote Yaliyoanguka, Yalianguka Wakati Ujenzi Unaendelea(unequal Settlement)

Pale Mjini Katikati Kuna Majengo Yaliyojengwa Kwa Matope Kwenye Miaka Ya 1800 Mpka Leo Yapo, Sana Sana Ukuta Unadondoka Na Wala Siyo Jengo Lenyewe.

Nitawaletea Hapa Article Kuhusu Hilo Baadaye
 
Mwikimbi unadanganya wananchi! Tunapozungumzia ubora wa ghorofa hatuangalii kuvuja mvua peke yake. Hali inatisha na pengine zaidi hata ya hiyo iliyoainishwa katika ripoti.

Mazingira ya Yemen ambako kuna maghorofa ya matope yaliyodumu kwa miaka mingi si ya kwetu. Nyumba ya vyumba sita ya matope si sawa na nyumba ya matofali hata kama si ya ghorofa. Uzito wa matofali ni tofauti na ule wa fito!
 
Swali la kujiuliza ni jee lisingeanguka hilo la Kisutu, hii ripoti tungeisikia? Zaidi ya hilo, kuna hata mmoja wetu ambaye angeiulizia?
 
Heshima mbele wakuu..... Fundi, asante Mkuu!!! Mwikimbi, hapo itakuwa ngumu kidogo kukubaliana nawe....

Kwa mtazamo wangu, tuna tatizo kubwa sana hapa nyumbani na kusema kuwa nyumba kama zingekuwa zimejengwa hazijaanguka mpaka leo ni kujidanganya kama wana fani!!

Unakumbuka hivi:
1. Design period?
2. Design load - Dead + live? pia kuna wind, earthquake/tremors that may also occur!! Kumbuka Tz ipo kwenye one of the earthquate prone areas lakini tofauti kati yetu na China ni a matter of time!!!
3. Steel failure - chemical attacks, smoothness (against ribbed/deformed bars), etc
4. Permanent deformation?
5. Maximum deflection?
6. Usisahau pia kuwa haya maghorofa marefu hapa mjini nasi tumeingia kwenye kujenga "framed structures" na sio zile tulizozoea ambapo tunapanga tofali na ring beams with few columns ambapo mirrored walls zinasaidia columns kubeba mzigo wa jumba hilo!!
7. Mwisho Mkuu unafahamu siri ya Jiji letu la Bandari ya Salama na mambo ya pit latrines, soil type (sandy to silt-sand) and closeness to the ocean/sea? Angalia kwenye designs za high rise framed structures kwenye mtandao utaona aliyesema majengo hayako safe alikuwa na maana gani!!!

Mwikimbi, hizo ni kutoka kwenye memory lane (shuleni na during my junior years) lakini kusoma email yako tu kichwa kikaniuma Mkuu.....

By the way, umesema kwamba Tume ya Lowassa haikufanya kazi sababu hawa kudrill kuta? Mkuu watake radhi wenye fani yao hapo manake walifanya kazi wewe ungewauliza their conclussions are derived/based on what kuliko ku trash their report only sababu hawakufanya test ambayo wewe unadhani ni appropriate!!
 
Fundi, hayo ndiyo yetu ya Bongo Mkuu, hatuna desturi ya kujihadhari kabla ya shari... Na hata shari ikitokea tunaishia ku "Treat symptoms and not the root cause"

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!!!
 
Mfano wa extent ya problem ni kuwa nyumba nyingi uswahili zilizojengwa na block hazina msingi. Mafundi wanasema msingi ni mambo ya kizungu au ujenzi wa serikali! Matofali yaliyotumika kujenga yalianza matofali 21( Morani hapa nisaidie) kwa mfuko hadi takhriban matofali 30 kwa mfuko! Anayetoa matofali mengi kwa mfuko ndiye mteja anamuona mahiri. Matofali hayamwagiwi maji vya kutosha kupunguza gharama. Kuta zilianza upana wa nchi tisa, zikaja nchi sita sasa nasikia nchi tano ndio fasheni! Kuta zilitokana na matofali niliyoyazungumzia. Nyumba hazina Fire-escape! Kuna jengo moja Manzese la ghorofa lina milango inafungukia nje ghorofa ya nne! Na nje sio kwenda kwenye balcony. Nadhani kwenye mchoro palikuwa na fire-escape ambayo wakati wa kujenga haikujengwa kupunguza gharama! Bado tusiogope?
 
Fundi, hayo ndiyo maisha..... Walisema mjini shule shambani kilimo... Hilo la matofali kwa mfuko aisee siku hizi ni kaaz kweli kweli manake usipomuangalia fundi kwa karibu zaidi waweza poteza saruji na wakati huo huo kununua hasara!! Wale wanaopiga mtaani ndio usiseme kuna wanaotengeneza tofali hata kubeba kupakia kwenye lori ni kasheshe Mkuu!!

Manaani amekuwa very kind to us manake siku ikipita tetemeko sijui itakuwaje hapa nyumbani, kuanzia uimara wa majengo, mipango miji, uokoaji........
 
Back
Top Bottom