BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Ni bora yavunjwe haraka sana ili kuwanusuru Watanzania kutopoteza maisha yao ndani ya maghorofa hyo bomu.
Ghorofa 100 Dar bomu
Shadrack Sagati, Dodoma
Daily News; Friday,June 27, 2008 @19:01
Zaidi ya maghorofa 100 jijini Dar es Salaam yamebainika kuwa yalijengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge limeelezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa, kati ya maghorofa 505 ambayo waliyakagua, 147 yalikutwa hayana nyaraka za ujenzi.
Lowassa aliunda tume baada ya jengo la Hoteli ya Changombe Village Inn, Keko, Dar es Salaam kuanguka mwaka 2006 na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa. Ilidaiwa kwamba ulikuwapo ukiukwaji katika ujenzi wake.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia Bunge kuwa tume hiyo ya Lowassa, ilibaini kuwa ukaguzi huo, pia maghorofa 81 yalikutwa yamekiuka masharti ya ujenzi huku maghorofa mengine 22 wenyewe hawakupatikana na yalikuwa yamejengwa bila kuzingatia sheria za ujenzi.
"Can you imagine, mtu kaamua kupandisha ghorofa lake hapo bila kufuata taratibu za mamlaka husika, hii ni hatari kubwa," alisema Pinda wakati anatoa majumuisho ya hotuba ya matumizi ya ofisi yake bungeni kwa mwaka 2008/09.
Panda alisema maghorofa mengi yanayojengwa Dar es Salaam yanajengwa holela bila kufuata taratibu za ujenzi, hivyo kuyafanya kuwa hatari kwa maisha ya binadamu. Alisema kama hatua za haraka hazitachukuliwa na serikali, kuna hatari ya watu wengi kupoteza maisha kwenye maghorofa hayo ambayo yanachipuka kama uyoga katikati ya Dar es Salaam, likiwamo eneo la Kariakoo.
"Tatizo ni kubwa kuna hatari ya kupoteza maisha ya Watanzania wengi zaidi kuliko hili lililotokea juzi kama tukiendelea kuwaachia Manispaa suala hilo," alisema Waziri Mkuu. Alisema tukio la kuporomoka kwa ghorofa kulikotokea wiki iliyopita Kisutu, Dar es Salaam, ni uzembe wa baadhi ya watendaji wakiwamo wahandisi wa manispaa husika.
Alisema kutokana na taarifa hiyo ya tume, serikali inaandaa utaratibu mzuri wa utekelezaji wake kuhakikisha maghorofa yanayojengwa yanakuwa bora yanayofuata taratibu zote za ujenzi. Sambamba na suala hilo, alisema serikali pia inaangalia uwezekano wa kuingia katika Jiji la Dar es Salaam, kwani imegundulika kuwa manispaa haziwezi kuachiwa kuendeshwa jiji hilo lenye shughuli nyingi za uchumi.
"Ni lazima serikali tuingilie kati, Dar es Salaam haiwezi kuendeshwa na manispaa, lile ni jiji ambalo ni kioo cha taifa letu," alisema Pinda. Alisema serikali inaangalia mfumo bora wa uendeshaji wa jiji hilo, baada ya kuonyesha mfumo wa sasa wa kuwa na manispaa tatu umeshindwa kupata mafanikio.
Pinda pia ameliambia Bunge kuwa serikali imekubali kutenga Sh bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Itigi kwenda Tabora. Alisema maeneo mengine yataendelea kufanyiwa upembuzi yakinifu ili miradi iliyopo sasa ikitekelezwa, ujenzi wa barabara hiyo uanze mara moja.