Ghiliba za Wanaume Kuwa Control Wenza Wao (FUNGA MWAKA PART 2)

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,662
2,000
IGWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Thread iliyopita nilirusha jiwe gizani acha watu waweweseke! NISHASEMA NA NARUDIA TENA IF YOU DONT HAVE A STOMACH FOR MY THREAD USIINGIE HUMU! WAJIPA TABU BUREEEEEEEEEEEE!!!!!!!!! UTAJIMALIZA NA PRESSURE NA KIUKARI! Mimi SITOBADILIKA!

NI KAZI CHAFU LAKINI LAZIMA MTU AIFANYE!!!! Nimejitolea kumfunga paka kengele so sitishiki na nyau!!!!!!!!

Back to Topic!!!!!!!!!

Ujue kuna vitu mwanaume anakuwa anakwambia intentionally au bila kujijua kwa minajili flani na hususani ni kukufanya uwe mdogooo kwake kama piriton. Sasa hivo vitu navijadili hapa kwa mapana!

1. "I banged this One HOT! Deadly attractive Chick one time." Hii ni ghiliba yake tu yake tu kuaka umuone nae yumo! Yote hio ni kukutaka ujisikie beneath him, na umuone he is way out of ya league coz wengi wetu sie ni wa kawaida tu, kina mwajuma ndala ndefu, tupo tupo sasa anajua akikupiga swaga za HOT, DEADY ATTRACTIVE lazima upange folleni na ukae kwa wa adabu. Manake wewe kwake bado sanaaaa!

2. "Siwezi Kuwa na Mwanamke Anaenizidi Kipato" Hii ndo ghiliba kuu kabisaaaa! Yote hio ni kukuhadaa yeye MTAFUTAJI SANAAA! Na wala sio tegemezi au wa kujibweteka hadi umzidi! Ukihadaika ukajibweteka miguu juu utashaaa! Kipato kakuzidi na mia yake huioni! Mwanamke ukiwa na economic power anakuheshi sanaa japo anaweza asikupende ila heshima mbele.

3. "My Ex GF/wife didnt understand me at all!" Hapo anakuchallange fupa limemshinda fisi wewe chiwawa utaliweza? Ndo utie akili sasa mwenzio after 5 years of devotion and hardwork aonekana badoooo sanaaaa hata research problem alikuwa hajaielewa, wewe je mwenye visiku vichache? Ufanye nini kuhamisha milima?

4. She was such a S.lut!!!" Mhhhhhhhhh! Mwenzio akinyolewa zako tia maji! Wee hesabu round zako tu in no time he will call you the B word kwa watu wengine. Usifuraie mwenzio akichambwa ukaona ndo security na mambo yao finito finito huna haja ya kuwatilia shaka.Mwenzio ndo tabia yake hio, hana jemaa wala hajui vya mgema! Stukaaa!

5."Nimeacha tu kupokea simu zake!!!!" Sasa wewe jiulize utaweza kuishi na NON COMMUNICATOR? Mkikwaruzana tu kidogo ushaingia kwa black list yake, na ana screen calls zako zote! Utajiju na ku ji j j!!!!! Hataki mjadala wala suluhu, you messed up big time yeye ana move on! KWELI? Waungwana ndo uishivo?

6. "You wont take shots with me!!!!!!? Lame!" Hapo anakughilibu tu uingiwe roho ya kutotaka kuonekana umekuja mjini na mbio za mwege, ilihali pombe huiwezi maskini ya Mola, ufakamie mi vodka na brandy ama whisky ili umrahisishie kazi yake ya shetani! Asubuhi wajikuta umefanya mambo hata hujapanga! Heri ata ujifanye uko kwenye dozi, ama hata una alcers kuliko kughilibika! Be your self usijitie kumimpress utachanika msamba!

7. "Njoo tu ulale nyumbani kwangu nothing will happen! Trust me i am gentle man" Hulalalaaaaaaaa! Mkabidhi fisi bucha uone kazi! Like seriously!!!!!!!!!!!!? Utisoma namba! Everyhing will happen within a short time.

8. "Katika ma GF zangu wote wewe ndo naekupenda zaidi haijawahi tokea!!!!!" Kalaghabao kila mtu anaambiwa hivo hivo. sasa wewe lewa sifa uione cha mgema akisifiwa inakuwaje.

NI HAYO TU!!!!!!!!!!!
 

Munkari

JF-Expert Member
Feb 9, 2013
8,090
2,000
Nimeshindwa kuelewa hilo neno hapo 'ghiliba'maana yake nini ndipo niendelee kusoma!
 

kalou

JF-Expert Member
Aug 22, 2009
4,942
2,000
wanasemaga WANAWAKE MWALIMU WAO KIPOFU....yaani sisi vidume tunarudiaga the same lines all over again na zinafanya kazi kama kawa...
 

Mkempia

JF-Expert Member
Mar 5, 2013
1,142
1,500
Nimezaliwa peke yangu mwanaume nakutana nae ukubwani kisa na mkasa wakujitwisha ya dunia ni nini??
 

Queen Horse

JF-Expert Member
Sep 12, 2013
400
500
Ha ha ha ha asante lara1 hiyoo namba 7 ndiyo inawagharimu wanawake wengi hata katika mwanzo wa mahusiano au wakiwa kwenye mitafaruku na wapenzi wao wanajisahau kwamba dushelele halina halina mabega wala mikono kusema litanasaa likiingia limeingia tu hata ujikunje vipi..
Kama umeamua kucheza segere we cheza tu sio kufanya maamzi robo robo na kuamini hayo maneno " im gentleman"... We unataka kumwamini mwanaume kama baba ako mzazi wakati mzazi mwenyewe sometimes ukijichanganya anaweza kukuchenjia
 

Mkunde Original

JF-Expert Member
Jul 20, 2013
807
1,000
lara 1 ile sredi yako ya kwanza funga mwaka part one wameifuta bana. Mie nlikuwa nasoma page to page kisha nchangie nashangaa naambiwa imekuwa merged/ moved au blocked by administrators, daah nimecehelea kuona uhondo huu, hii part 2 siiachi ili hata wakiifuta nakuwa nshasoma.
Kweli jiwe ulilotupa kwenye part one limewagonga wengi hasa kichogoni ndo maana wameumia hata kuifuta looh
 
Last edited by a moderator:

ng`wana ong`wa kulwa

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
2,421
1,500
Elimu kwa nyumba ndogo,na makahaba lakini haitawasaidia kwa tamaa yenu ya fedha mko tayari kulamba viatu vya wenye pesa......kweli vijisenti ni kiboko yenu....mwenye fedha hata ukiyajua hayo hayamtisha atakutenda ukileta ngembe anakutosa maana wengi tu wanajipitisha.......niko mgodini naona jinsi wadada wanavyo tendwa na kutendeka,nyodo mfanyie asiye na pesa atakubembeleza mpaka na machozi yamtoke.
 

Munkari

JF-Expert Member
Feb 9, 2013
8,090
2,000
we msukuma utajuaje kiswahili...labda tungeandika mabhugando ndio ungeelewa :becky:

Ghiliba maana yake ni : ~enye kudanganya

dah! Aisee! Okey!! Now nimeelewa ujue miye kiswahili nilipata F nashangaa hata hiki ninachoandka hapa cjui nimekitoa wap? Khaa! Wacha sasa nisome afu nirudi kuchangia..asante kwa kunielewesha ndo raha ya jf new thngs in the head mweh! Ila dah!..ntakuundia tume aisee hadi nimeskia joto!!
 

Daddo

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,409
2,000
Ukitaka kurudi darasani wewe soma nyuzi za Lara 1. Hakiyanani lazima utafute kamusi vinginevyo uamue kutoelewa tu yaishe.
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
53,430
2,000
Na usingeelewa tu ningekutandika makwenzi...

dah! Aisee! Okey!! Now nimeelewa ujue miye kiswahili nilipata F nashangaa hata hiki ninachoandka hapa cjui nimekitoa wap? Khaa! Wacha sasa nisome afu nirudi kuchangia..asante kwa kunielewesha ndo raha ya jf new thngs in the head mweh! Ila dah!..ntakuundia tume aisee hadi nimeskia joto!!
 

Eli79

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
28,068
2,000
Hivi, sababu gani inamfanya mtu kuongelea habari za ex bf/gf kila wakati, hasa akiwa na mpenzi mpya?
Huo sio udhaifu kweli?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom