Ghiliba za wanasiasa: Je, inawezekana kuwaburuza mahakamani ili watolewe kwenye nafasi zao Kwa kulaghai ili wachaguliwe?!

Kabulala

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
695
935
Nimekua nafatilia wanasiasa wengi wakati wanaomba Kura wanasema uongo mwingi Sana na Kwa bahati mbaya wanaaminiwa na kupewa Kura na kutumikia nafasi walizozipata Kwa kulaghai bila wasiwasi wowote na mwisho wa kipindi walichoomba wanazawadiwa kiinua mgongo kama ahsante.

Kwangu Mimi naona hiyo si Sawa kwani wakati wa kampeini ni Sawa na usaili/interview Kati ya mwajili(wananchi) na mwajiliwa(mgombea). Kitendo cha mgombea kutoa information au ahadi zisizo za kweli ni Sawa na kudanganya wakati wa interview ya kuomba KAZI, na ukigundulika baada ya kupewa KAZI kwamba uliongopa ili upewe nafasi mwajili ana haki ya kukufata KAZI bila kukulipa fidia yoyote.

Je, hawa waheshimiwa wanaotulaghai kila kukicha,Sisi kama WAAJILI tunaweza kuwaburuza mahakamani tukiwa na vielelezo kama vile recordings za ahadi zao wakati wakiomba kazi (Kampeini) ili aidha kumzuia mgombea asigombee tena nafasi Ile au kuliomba bunge au taasisi husika isimpe mhusika kiinua mgongo, na pesa hiyo ielekezwe kwenda kukamilisha ahadi zilizotolewa bila kutekelezwa?

Nadhani Kwa kufanya hivyo kutawazuia wanasiasa uchwara kwenda kuwadanganya wananchi Kwa minadili ya kupata kuungwa mkono ilihali wanatambua fika kwamba ulaghai wao unawapa wananchi matumaini hewa.

Wenye ujuzi na hili naomba mnisaidie manake ninachukizwa Sana na utapeli unaofanywa na baadhi ya wanasiasa.
 
Back
Top Bottom