Elections 2010 Ghasia hizi za kihistoria: GHarama ya Amani ya kweli

Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,751
7,535
Ndugu wana JF, ni takribani miaka 50 to Mungu alipoona vema niwe kiumbe hai. theluthi mbili ya maisha yangu nimeishi TZ. Nimepiga kura katika chaguzi tatu na hii ya sasa ni ya nne. Sijawahi kuona ghasia za namna hii wakati wa uchaguzi. Kwa nini Chaguzi hii ni tofauti hivi; watu wanakesha katiki offici za tume ya uchaguzi kungojea matokeo; watu wanapigwa na kuumizwa na hata wanakufa (CCM Wanamwaga damu); nyumba zinachomwa moto; magari yanachomwa moto; Sijui wewe lakini hii ni ngeni kwangu.

The bottom line ni kwamba watu wanatafuta amani ya kweli inayo patikana kwa gharama kubwa. Amani hii haiwezi kupatikana bila haki kutendeka. Wananchi wamegundua, baada ya Miaka mingi kuwa wamekuwa na kile kilichokuwa kikiitwa amani katika nchi hii na kusifiwa na nchi nyingi zinazoendelea kumbe hakikuwa amani kabisa, badala yake ni kile kinachitwa utulivu wa kisiasa (political stability).

Shukrani kwa Dr. W. P. Slaa, macho ya watanzania wengi yamefumbuliwa na sasa wanafahamu tofauti kati ya "amani" na "utulivu"; kwamba Chama cha mapinduzi kime abuse utulivu na uvumilivu wa watanzania, kwa manufaa ya mafisadi wachache ndani ya chama na serikali.

Hapo zamani za kale niliwahi kusema katika janvi hili kuwa amani ya kweli itapatikana kwa gharama ya damu, sasa yamekwisha timia: yalianza Kenya na sasa wana amani (na katiba mpya, katiba ya watu). Sasa yametufika sisi watanzania. Sina shaka hii ni njia sahihi. Hatuwezi kuongozwa na zezeta nasi tukaendelea kuwa mazezeta na kukubali kuongozwa hivyo hivyo, worse still, tuongozwe na kipofu asiyekubali kuwa ni kipofu nasi tukamfuata kama mazezeta tu. Hatuwezi kukubali waendelee kuchachua kura za thamani ili tu waendelee kutoongoza wapendavyo kwa faida ya afisadi wachache.

Watanzania tumechoshwa na hayo ndiyo maana tunafanya kile ambacho mafisadi wanakiita vurugu wakati ni kupigania haki iletayo amani ya kweli na ya kudumu. Nani anatulaumu? Sasa mimi na sema ndiyo kwanza kumekucha kweupe na tunazoziona ni mvua za rasha rasha, elninho na tsunami vinakuja. Kiongozi mwenye hekima anatakiwa kufahamu kuwa pasipo na haki hakuna amani.

Hakuna kulala mpaka kieleweke

Mungu ibariki Africa, MUNGU ibariki Tanzania MUNGU Bariki CHADEMA
 
Back
Top Bottom