Ghasia awatahadharisha watumishi waliotangaza nia ya kugombea 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ghasia awatahadharisha watumishi waliotangaza nia ya kugombea 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jun 5, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia.


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, amewataka watumishi wa umma waliotangaza nia ya kuwania uongozi katika Uchaguzi Mkuu ujao, kuomba likizo ili kuepuka ukiukwaji wa sheria.

  Ghasia aliyasema hayo wakati akifunga mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika utumishi wa umma, mjini Dodoma jana.

  "Kama umeshatangaza nia ya kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi, omba likizo ili kujiepusha kuchanganya kazi na masuala ya kisiasa,"alisema.

  Pia aliwaasa watumishi wa umma wasihusike katika kushabikia vyama vya siasa, ili kuepuka kukiuka misingi ya sheria za kazi.

  Aliwataka kusoma waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma namba moja wa mwaka 2000, unaofafanua utaratibu unaosimamia ushiriki wa watumishi wa umma katika siasa.

  Akizungumzia kuhusiana na programu ya kuleta mabadiliko katika utumishi wa umma, Ghasia alisema serikali inasisitiza utendaji wa kazi unaozingatia matokeo.

  Pia alisema programu hiyo, inaimarisha uwajibikaji wa maadili ya watumishi wakati wakiwahudumia wananchi.
  Hata hivyo, alisema utumishi wa umma unakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo baadhi ya watumishi kutokubali mabadiliko ya kifikra na ukosefu wa maadili.

  Alisema kutokana na hali hiyo masuala ya uwajibikaji na tija yataendelea kuwa sehemu ya ajenda pana ya kuimarisha utumishi wa umma.

  Ghasia alisema umuhimu huo unafanya masuala hayo kuendelea kuwa moja ya maeneo ambayo yatashughulikiwa na baraza lijalo.

  Mmoja wa wajumbe hao, Edna Mwaigomela, alitaka serikali kutilia umuhimu ushauri wa baraza hilo lililomaliza muda wake, wa kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi.

  Alisema mazingira mazuri ama mabovu yana uhusiano katika utoaji huduma kwa wananchi.


  CHANZO:
  NIPASHE
   
 2. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ni vyema awakumbushe maana wengi wametangazz nia....
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  ......akiwemo mumewe ndio maana kaongea kwa upole
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Jun 10, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hapana, kuomba likizo ni makosa; mtu akitaka kuwania nafasi za kisiasa anatakiwa ku-resign kabisa kutoka kwenye utumishi wa umma. Baada ya ku-resign, anabaki mtu huru ambaye akifanikiwa ndoto yake ya kisiasa, basi anakuwa mheshimiwa, na akikosa, basi tunabaki naye mtaani akila pensheni yake kama anayo.

  Hiki kitendo cha kuomba likizo akajaribu na akikosa aruhusiwa kurudi kwenye utumishi wa umma kinasababisha huduma za umma kupindishwa kwa sababu za kisiasa. Vile vile mtu anayetaka kuwania nafasi za kisiasa inabidi aache majukumu ya umma kwa muda mrefu upatao mwaka na nusu au zaidi kabla ya hajaanza kuwania nafasi za kisiasa. Kutokufanya hivyo kunaweza kumfanya akatumia nafasi yake ya kuhudumia umma kwa njia ya upendelea kisiasa muda mfupi kabla hajaanza kampeini.
   
 5. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kichuguuu hapo umeongea NENO kwani sharia inasema hivyo na yeye anasupport mara anasema soma kifungu fulani kwani ukiwa Likizo sio mtumishi wa Umma?? kama ndivyo Basi Mh. Waziri akiri amejichanganya
   
Loading...