Hili suala kwakweli limekuwa baya sana. Kadri siku zinavyosonga, maisha ya watu yanazidi kutegemea mtandao. Na kwa kawaida teknolojia inavyozidi kukua ndivyo bei inapozidi kushuka. Sasa inakuwaje hawa jamaa wanaongeza bei kwa asilimia 100.

Kwa Tsh 1000 nilikuwa napata GB 1 ya tigo. Sasa napata MB 500. Wanaongeza gharama mara mbili? Hili suala ni counterproductive kwa uchumi. Serikali imefika mwisho wa kufikiri na imeona njia pekee ya kupata pesa ni kodi! Haya, hizi zikifika sehemu hazitoshi mtaongeza kwenye nini tena? Maana haichukui muda hizi tozo zinakuwa hazitoshi. Mtapata wapi zingine na mmekwamisha watu biashara, mnajua ukubwa wa biashara zinazofanyika mitandaoni?

Hata wakoloni hawakuwa kama nyinyi, mnakamua bila kulisha.
Hamia Halotel mbona simpo tu
 
haya mambo haya sijui itakuwaje uko mbele Kama Leo ndo Hiv na siku zote mafuta yakishapanda na gharama za maisha lazima zipande
 
Monthly subscription of $99 and $499 for the Starlink kit (start kit)...

Mzee baba bado watumiaji hapo watakuwa ni maofisi, na watu binafsi wenye mpunga mrefu
mkuu tena hili dili mie naliwahi mapema, ujue router zao zina support hadi devices 128 full speed...
sasa kwa mtaani hapo, we weka star link 1 tu, unaweza hudumia takribani watu 100...wachangishe 5000 unlimited week au 1000 kwa siku, unlimited, kwa mwezi una almost 3 million..
unalipia kifurushi na bado unafaidika na unlimited yako... hii ni fursa pia, ila najua tcra watazingua lakini haina namna ni kuwa mbishi tu...
 
t_20210825-161245-1.jpg
 
Mnataka hela ya kampeni tutoe wapi ilihali mnaona upinzani wa ndani ushaanza kuwa mkubwa...ngoja tukusanye pesa kwanza bei zitashuka hali ikitulia...
 
Kwa sababu tunatumia bidhaa walizotengeneza wao kwa wingi zaidi...
miundo mbinu kwenye uchukuzi na mawasiliano ndio usiseme, hapo kariakoo tafuta duka halina bidhaa za China nakupa 10000...
Mchina hakwepeki sasa, tuanzeni kujifunza ki China ..., boda boda hizi ndio usiongee kabisa... tv sasa ndio utakimbia kabisa...
pasipo yeye wa Tanzania wangapi mlikuwa na pesa ya ku affor iphone 13 ambayo na yenyewe pia imepita mikononi mwao, vianda 98% vya electronics USA uzalishaji ni China... naweza ongea hapa mpaka kesho...

China ni mkombozi hilo tusibishe...
La boda umelisema bila kuliwekea wino mweusi.

Bila ya Mchina hizi fujo za boda boda kujimwambafy barabarani zingelikuwa ni ndoto isiyooteka.

Bei ya piki piki ya mjapani ni bei ya IST.

Na bei ya pikipiki BMW ni bei ya Land cruiser nani angelithubutu!

Labda Taxfy na Uber ndo wangelitamba kitaa.
 
Mkuu usiwe na shaka, hizi kampuni zitapigwa doro mpaka watakua wanapita barabarani na kutangaza gb 100 kwa elfu 2 mwezi mzima, starlink ya Elon Musk tayari imefika Nigeria sisi huku ni next year hapo mambo yanajipa speed wanasema ni 150Mbps ikishuka ni 50Mbps.

Ushenzi wanaoufanya wanafikiri dunia inawasubiri, watu wanakwenda mwezini sisi bado tunapambania bundle.

$99 mwezi mzima unlimited ni very cheap tusisahau pia mchina mkombozi wetu atakuwa hayupo nyuma kuja na suluhisho la upatikanaji rahisi na nafuu wa mtandao.
Utashangaa wakazuia starlink isioperate Tanzania. Mana wao kazi yao n kuhakikisha wanaweka kikwazo kila penye uwezekano.
 
na mie nina wasi wasi huo lakini, mitandao yetu ni kama demand ya mtandao imekuwa kubwa mnooo, yaani huduma za unlimited sasa hakuna kabisa, hata wale wazee wa usiku unlimited wamepotea.

Lakini kama satellite zingine zinafanya kazi Africa wakizuia itakuwa sio fair, mpaka sasa kuna kampuni za satellite internet zinaoperate kama kawaida, hii ikija mimi nitanunua , uzuri mnaweza share na watu wakakusaidia kulipia fee/month...
Watafanya kama walivoifanyia PayPal
 
mkuu tena hili dili mie naliwahi mapema, ujue router zao zina support hadi devices 128 full speed...
sasa kwa mtaani hapo, we weka star link 1 tu, unaweza hudumia takribani watu 100...wachangishe 5000 unlimited week au 1000 kwa siku, unlimited, kwa mwezi una almost 3 million..
unalipia kifurushi na bado unafaidika na unlimited yako... hii ni fursa pia, ila najua trca watazingua lakini haina namna ni kuwa mbishi tu...
Walivo wapuuz watakwambia mpaka uwe na lesen
 
Utashangaa wakazuia starlink isioperate Tanzania. Mana wao kazi yao n kuhakikisha wanaweka kikwazo kila penye uwezekano.
inauma sana asee, ni kweli mkuu, Musk atakuja kuharibu business za watu, ikiwa hivyo ni bora wazime tu internet ijulikane tunaishi kama north korea...
 
Hili suala kwakweli limekuwa baya sana. Kadri siku zinavyosonga, maisha ya watu yanazidi kutegemea mtandao. Na kwa kawaida teknolojia inavyozidi kukua ndivyo bei inapozidi kushuka. Sasa inakuwaje hawa jamaa wanaongeza bei kwa asilimia 100.

Kwa Tsh 1000 nilikuwa napata GB 1 ya tigo. Sasa napata MB 500. Wanaongeza gharama mara mbili? Hili suala ni counterproductive kwa uchumi. Serikali imefika mwisho wa kufikiri na imeona njia pekee ya kupata pesa ni kodi! Haya, hizi zikifika sehemu hazitoshi mtaongeza kwenye nini tena? Maana haichukui muda hizi tozo zinakuwa hazitoshi. Mtapata wapi zingine na mmekwamisha watu biashara, mnajua ukubwa wa biashara zinazofanyika mitandaoni?

Hata wakoloni hawakuwa kama nyinyi, mnakamua bila kulisha.
Karibu ttcl kwa 1000 unapata GB 1.2 mkuu.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom