Gharama za umeme: Rais Samia muwajibishe Waziri Kalemani na uongozi wote wa TANESCO

We jamaa hata hujui ulichoandika. Nakupa mifano 3.

Kutengeneza mnara mmoja wa Simu ni zaidi ya 300,000,000 na kila baada ya km 3-15 kulingana na wingi wa. Watu makampuni ya simu wameweka mnara. Na simu kadi zinauzwa kwa tajiri au masikini kwa 1000 tu, je uliwahi kuona gaharama za mnara?

Pili wazalishaji wa bia na soda hata ukienda hapo getin kwao Bei ya soda au bia ni sawa na kule misenyi, Namtumbo, vudee au Makete. Wao wamewezaje Tanesco washindwe?

Miundombinu yote ya umeme Hadi meter ni Mali ya Tanesco, miundombinu ya mteja ni kuanzia umeme unatoka kwenye meter kuingia ndani mwako.

Swali, mteja anunua meter, nguzo, waya Kisha vyote viendelee kuwa Mali ya Tanesco. Hii ni sahihi?

Ukinunia line ya simu ni yako, simu yenyewe ni yako unachopatiwa na kampuni ya simu ni huduma ya mawasliano na sio vifaa vyao.

Hivyo hivyo kwa mashirika ya kugawa maji wanakuuzia maji tu mtandao wote ni wa kwao.
 
Daaaa tuvuteni umeme vijijini kwetu na mashambani hamani daaa safi sana
 
Bilioni 30 kilikuwa kiwanda Cha kutengeneza nuklia? Hicho kiwanda ni very simple na gharama nafuu sana hata 1 bilioni hakifiki.
Mimi nilishangaa sana. Manguzo yale ya miti hata hawa wauza mbao waliojijenga na uzoefu wa muda mrefu si wanaweza. Hata wakijenga mitambo ya kuchemsha nguzo za miti na kutia dawa, kutengeneza za simenti na za vyuma sitarajii ivuke bilioni 10 na hapo wakizalisha nyingi.
 
Nipo kwenye rekodi hapa ya kumtetea waziri Kalemani huko nyuma lakini leo naomba Rais Samia amfukuze tena ikibidi haraka Sana huyu waziri.

Kwa mujibu wa maagizo aliyowapa Tanesco waziri Kalemani anataka sasa karibu watu wote Tanzania nzima wakitaka kuunganishiwa Umeme walipe Elfu 27 tu bila kujali gharama halisi za kuvuta umeme kwa mtu huyo anasema Serikali imepitisha hela ya ruzuku kwa Tanesco.

Sasa hebu twende taratibu huku tunatumia akili kidogo. Mtu anajenga ghorofa lenye apartments 20. Mfano Masaki huyu mtu sio masikini why asigharamie gharama halisi?

Why Tanesco ijinyime mapato Kwa kutoa ruzuku hadi Kwa matajiri wa Masaki Hadi Upanga?

Anaejenga Fremu 20 Mbeya mjini au Dodoma mjini? Why alipe elfu 27 wakati Tanesco wananunua hizo Mita moja laki moja 20?

Kwanza hii tafsiri yake ya Mjini kuwa ni Ilala City Center kaitoa wapi?

Anajua maana ya Urban and Rural? Anajua history ya kuanzisha REA?

Why anakuja kuleta siasa za kutafuta umaarufu Kwa nguvu Kwa gharama za kuiua Tanesco??..kama mpaka sasa Tanesco haipati Faida inaishi kwa ruzuku. Why anakuja na maamuzi ya kupunguza mapato kwa Tanesco?

Mapato ya service charge yamefutwa. Mapato ya kulipisha fomu yamefutwa. Sasa hata gharama za kuvuta Umeme iwe Upanga au Masaki ziwe za REA kweli?

Huyu waziri anafanya siasa za hatari za kujifanya 'mtetezi wa wanyonge aliebaki'. Itasababisha Tanesco huko mbeleni ishindwe kujiendesha wala kulipisha wateja wake gharama halisi za Umeme.

Anataka aonekane yeye alipokuwepo gharama zilishuka wakati si kweli.

Gharama zipo zile zile anachofanya ni kutumia ruzuku ya serikali ambayo sio ya uhakika na haina guarantee ya kuwepo kila mwaka.

Tayari foleni ya umeme unaohitaji nguzo Tanesco inafika miezi sita sasa na bado waziri anaongeza tatizo badala ya kupunguza.

Utaratibu wa REA ulikuwepo kabla ya hata Kalemani hajawa waziri. REA ibaki REA kwa wananchi wa vijijini na wenye vipaji vya chini.

Kulazimisha REA itumike nchi nzima ni siasa za kufeli na kuja kulaumiana huko mbele wakati huduma itakapokuwa ngumu kupatikana baada ya mapato kushuka REA hadi Masaki na Sinza?

Wenye Bar na mafremu 40?

Wenye ghorofa zenye apartment 40?

Hi ruzuku ni pesa ambayo wananchi hasa masikini wanachangia. Why itumike kufaidisha hadi matajiri kwa siasa tu?

Viongozi wa Tanesco kuanzia Bodi hadi CEO wake wote wapigwe chini kwa kukubali maagizo haya ya huyu waziri...

Watu wenye uwezo walipie gharama halisi za umeme.

REA ibaki vijijini na kwa watu masikini.
Politiki kitu Mbaya sana

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Mm naona yuko sawa kazi ya serikali nakugharamikia wananchi wake kwn hakuna nchi umeme unavutiwa Bure kabisa acheni propaganda. Tanesco itazidi kupata mapato kwa wingi kama watanzania wengi wakiwa na umeme. Na kuwa tajiri sio kigezo chakutoa pesa nyingi ndio upate umeme Kwan tajiri pia ni mwananchi na anahaki pia kama wengine.
 
27,000 Bado ni nyingi,ilitakiwa umeme ufungwe Bure kabisaaaa.

Wameanza vizuri laki 5 na 20 ilikuwa pasua kichwa ila 27,000/= sio mbaya!! wananchi wengi watafunga umeme ,wengi walikuwa wanashindwa kuunganisha umeme gharama zilikuwa kubwa sana,kwa hili TANESCO wataongeza mapato sana maana wataongeza watumiaji wa umeme.
 
Wameanza vizuri laki 5 na 20 ilikuwa pasua kichwa ila 27,000/= sio mbaya!! wananchi wengi watafunga umeme ,wengi walikuwa wanashindwa kuunganisha umeme gharama zilikuwa kubwa sana,kwa hili TANESCO wataongeza mapato sana maana wataongeza watumiaji wa umeme.
Tanesco makao makuu watabisha
 
Tanesco makao makuu watabisha

Hawawezi kubisha maana order imetoka juu na maazimio yalifanyika tangu may 5 na taarifa imetoka jana kichofuata ni utekelezaji tu na Tanesco wenyewe wanayo hiyo taarifa ni 27,000/= tu tanzania nzima mjini na vijini kasoro Dar City centre tu hiyo ni umeme wa single phase.
 
Na sasa anataka mtu hata aliejenga fremu 40 za biashara nae alipe elfu 27.
Au ghorofa Upanga la apartment 40 alipe elfu 27.. imagine that
1. Gharama za elfu 27 ni kwa wale wa single phase tu.

2. Gharama hizo haziwahusu watu wa Dar es salaam City centre, wao watalipa gharama za kawaida.

3. Nia ni kuhakikisha umeme unafika nchi nzima. Ili nia hiyo itimie ni vyema kupunguza gharama za kuunganisha umeme.

4. Umeme kwa sasa unazalishwa mwingi. Hakuna haja kuwa na umeme unaobaki bila matumizi wakati unaweza kuwaunganishia watu na wakalipa bill/luku shirika likapata mapato.

5. Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Kalemani bungeni ya bajeti ya wizara yake, alisema Tanescoa imeacha kutegemea ruzuku ya serikali kuu tangu mwaka huu wa fedha kuanza. Kwahiyo, Tanesco inajitegemea siku hizi.
 
Serikali ndio inatoa hela kuunganishia watu umeme, wewe kinachokuuma ni nini?

Kwani hapo kuna hela ya Tanesco? Si ya serikali, sasa kama serikali inataka watu wawekewe umeme hata bure as long as inaipatia tanesco gharama za kununua material wewe unaumia nini?

Tanesco haina investment cost yoyote kwani hela zinatolewa na serikali. Wewe unaumia watu kuunganishiwa kwa 27000? Ilitakiwa kua bure kabisa.
 
1. Gharama za elfu 27 ni kwa wale wa single phase tu.

2. Gharama hizo haziwahusu watu wa Dar es salaam, wao watalipa gharama za kawaida.

3. Nia ni kuhakikisha umeme unafika nchi nzima. Ili nia hiyo itimie ni vyema kupunguza gharama za kuunganisha umeme.

4. Umeme kwa sasa unazalishwa mwingi. Hakuna haja kuwa na umeme unaobaki bila matumizi wakati unaweza kuwaunganishia watu na wakalipa bill/luku shirika likapata mapato.

5. Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Kalemani bungeni ya bajeti ya wizara yake, alisema Tanescoa imeacha kutegemea ruzuku ya serikali kuu tangu mwaka huu wa fedha kuanza. Kwahiyo, Tanesco inajitegemea siku hizi.
Haya maelezo (namba 2) umeyatoa wap? Waziri kasema sehemu zote kasoro ilala ambako hata hawahitaji kwa sasa
 
2. Gharama hizo haziwahusu watu wa Dar es salaam, wao watalipa gharama za kawaida.

Karudie kusoma vizuri tangazo ,except Dar City Centre , Je Dar city centre ni wapi? Unajua maana ya centre? Nyie ndio mnapotosha watu wa tanesco na kuwasikiliza nyie.

Mjini na vijini gharama za single phase ni 27,000/= except Dar City Center , hawakusema except Dar-es-salaam!! Maana hata Gongo la mboto mwisho wa lami ni Dar,Kongowe ni Dar,yale yale puna ni dar ,Bunju ni dar na wote hao wapo nje ya mji.
 
Tushaanza kuona madhara ya siasa kwenye huu upuuzi. Dodoma umeme ulikua haukatiki ila siku hizi kila siku..kama sasa hivi maeneo ya nkuhungu huku umekatika
 
Back
Top Bottom