Gharama za uchukuzi katika botii za dar/zanzibar

Mgombezi

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
610
178
Wana JF

Nimekuwa nikisafiri na boat za Abiria Dar/ZNZ, utaratibu unaotumika katika kupakia na kushusha mizigo ya abiria si SHWARI.

Katika bandari zote mbili (DAR na ZNZ) kuna wachukuzi ambao wanaweza huchukua mizigo ya abiria mpaka ndani ya boat, hivyo inamlazimu kila abiria kutafuta mchukuzi wake. Wachukuzi hawa wameajiriwa na mtu asiyejulikana; kwani gharama zao huwa ni za juu sana na wanadai kila kifurushi watakachobeba wanatakiwa kumpa BOSS wao Sh. 500. Ninaamini hiki kikundi kinawatumikisha watu kwa maslahi yao binafsi.

Kwa kweli hali inasikitisha sana kwani kila kona ni VURUGU, kila mmoja anatafuta kula yake. Nimeshangaa kuona AZAM MARINE wanaboresha ofisi zao na sehemu ya kupumzika wageni lakini suala la mizigo ya abiria haijaangaliwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom