Tigershark
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 7,051
- 12,560
Hili swali halikuwahi kunifika mpaka mgombea urais wa CCM kufika Kigoma. Mambo yalikuwa hivi:
*Magari kama Coaster na mabasi yalikodiwa kuchukua wananchi kutoka vijiji mbalimbali. Nina rafiki yangu ambaye gari zake zote zilikodiwa kwa kazi hiyo!
* Wananchi wote waliopakiwa kwenye magari hayo kwenda kwenye uwanja wa kampeni waligawiwa tshirt na vipepereshu vya CCM bure!
* Boda boda walipewa T-shirt na namba ambayo waliitumia kujazia mafuta kwenye sheli!
* Wasanii hulipwa kiasi gani kwa mkutano mmoja? Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, 2015 diamonda na alikiba walikuwa wanapata mil 15! Sijui na wasanii wengine mil 5 kwa mil 2 kulingana na ukubwa wao,sijui kwa sasa wanalipwaje.
* Nimeshuhudia msafara wa magari zaidi ya 60 katika msafara wa mgombea urais.
* Mengine unaweza ukaongeza wewe kama vifaa,chakula,posho za msululu wa watu nk.
Hivi kweli gharama za uchaguzi zinazingatiwa na kwa mujibu wa NEC. Gharama hizi zinapaswa zisizidi kiasi gani kwa mwaka huu wa uchaguzi?