Gharama za uchaguzi Igunga ni aibu kwa nchi yetu

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,537
1,303
Ni haki ya msingi ya kikatiba kwa wananchi wa Igunga kupata.mwakilishi wao bungeni ila kwa mwenendo wa kampeni za.vyama vinavyoshiriki uchaguzi sio siri garama ni kubwa mno kuliko uwezo wa uchumi wa.nchi yetu.Ni muda muafaka sasa kuachana ni huu upuuzi wa utitiri wa vyama kwani si tu vinatafuna kodi za walalahoi lakini pia usanii wa kuwadanganya wapiga kura kwa ahadi hewa ni dhambi ambayo haiwezi kusamehewa hata kidogo
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
Kweli kabisa mkuu..

Kuna haja ya kuangalia sheria za uchaguzi kupunguza matumizi makubwa ya fedha za umma..

Pesa walizotumia CCM, CUF na CDM combined zingeondoa kero zote jimboni hapo maji, shule madaraja etc..

Sijaona ulazima wa gharama zote hizo kwa ajili ya kumpta mbunge moja wa miaka 3..

Hii inaonyesha tunatumikia siasa (call demokrasia) bila kuangalia mazingira, mapato yetu..yaani copy and past..of western policies..without any tailor made adjustment ..
 
kiche

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
456
155
Hali hii inanikera sana,pesa zinateketea bila sababu!Kulikuwa na maana gani kutunga sheria ya gharama za uchaguzi?
 
Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,221
368
Ni haki ya msingi ya kikatiba kwa wananchi wa Igunga kupata.mwakilishi wao bungeni ila kwa mwenendo wa kampeni za.vyama vinavyoshiriki uchaguzi sio siri garama ni kubwa mno kuliko uwezo wa uchumi wa.nchi yetu.Ni muda muafaka sasa kuachana ni huu upuuzi wa utitiri wa vyama kwani si tu vinatafuna kodi za walalahoi lakini pia usanii wa kuwadanganya wapiga kura kwa ahadi hewa ni dhambi ambayo haiwezi kusamehewa hata kidogo

Hii ni kutoka na mfumo mbaya wa NEC na serikali iliyopo madarakani wao wameona ni muda wa kumwaga pesa za umma kwa ajili ya uchaguzi wamesahau kuwa wakitoka hapo wataisahau igunga mpaka uchaguzi ujao inafika mahali wananchi twapaswa kujitambua nini maana ya uchaguzi ni viongozi kututumikia sio sisi twatumikie wao,

Hebu tizama hizo gharama za Igunga it doesnt make sense at all kwa nchi maskini kama TZ kukimbizana kwa gharama hizo kwa uchaguzi kwa jimbo dogo, eg CCM kama wao wanapendwa kwanini waingie gharama hizo zote hiyo ni dalili ya kuta kujidhihirisha ati wanapendwa kwa sasa watanzania hawana mvuto na CCM na hawaitaki CCM wanataka mabadiriko mampya ya kuwa kwamu hapo walipo kiuchumi na kimaisha yao
 
opwa

Member
Jun 10, 2010
66
5
hivi tutahesabia hata yale mahindi , sukari pia na risasi si ndio wanajamvi? mmh ni hatari
 
UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
6,306
4,688
Wakuu, nakubaliana na nyie kwamba yawezekana gharama ni kubwa sana. Sina ubishi na hilo.
Lakini, kwani serikali imetoa fedha kwa vyama kwa ajili ya uchaguzi wa Igunga pekee? Kama vyama vinatumia pesa wanayopata kama ruzuku basi ni haki yao, maana wamepewa pesa hiyo kwa mujibu wa sheria. Unless Kama kuna sheria inayowazuia wasizidishe kiwango fulani, au kama wanazuiwa kutumia pesa ya ruzuku kwa baadhi ya mambo km hayo ya uchaguzi. Kwa hiyo hapo tatizo siyo matumizi ya pesa Igunga, bali ni sheria yenyewe inayohalalisha utoaji wa pesa zetu za kodi kwa vyama vya siasa.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
13,096
13,977
Kweli kabisa mkuu..

Kuna haja ya kuangalia sheria za uchaguzi kupunguza matumizi makubwa ya fedha za umma..

Pesa walizotumia CCM, CUF na CDM combined zingeondoa kero zote jimboni hapo maji, shule madaraja etc..

Sijaona ulazima wa gharama zote hizo kwa ajili ya kumpta mbunge moja wa miaka 3..

Hii inaonyesha tunatumikia siasa (call demokrasia) bila kuangalia mazingira, mapato yetu..yaani copy and past..of western policies..without any tailor made adjustment ..

Nadhani marekani hawana byelection. Mbunge au seneta akiachia ngazi basi gavana anateua mtu wa kuziba pengo hadi uchaguzi utakofuata. Chaguzi zao zimegawanyika katika makundi mbali mbali na hufanyika kila baada ya miaka miwili
 
The dirt paka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
371
65
Kwa nyakati kama hizi there are more to come nyie ndio mmeshituka leo kuwa vyama vinafuja pesa? Mwenzenu kitaaambo, cdm ilpointroduce kampen kwa helcopter watu hawakujua ni kwanini na hadi sasa hawaelewi, CCM NAO wamekopi wanadhani labda ni kastarehe kumbe....
 
Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Hizo ni gharama za demokrasia. Tuzipokee kwa mikono miwili.
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,395
Hizo ni gharama za demokrasia. Tuzipokee kwa mikono miwili.
Tunaigharamia sana SIASA kuliko kitu kingine kwa sasa labda inazidiwa tu na ufisadi. Madhara yake hayapimiki hasa ukiangalia huduma za jamii zinavyozidi kudorora kila uchao. Tujiulize tu kidogo. Kulikuwa na haja gani CCM kumpitisha Rostam, Chenge na Lowasa wagombee huku wakijua walivyo magamba kwa chama hicho? Huyu Dr Dalali Kafumu yeye sio Gamba kweli? Ile "palace" yake pale Pugu Kajiungeni kaijenga kwa mshahara upi wa serikali?
 
Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,735
1,195
Hili swali nimejiuliza na nimekosa jibu mujarabu kwakweli,,,ukipata nafas ya kusoma gazeti la mwananchi la LEO utaona tu kuwa hivi vyama vinashindana kwa kuonesha nguvu ya pesa
 
Iza

JF-Expert Member
Jan 8, 2009
2,001
588
Sio tu aibu bali ni matusi makubwa kwa wananchi ambao huduma za msingi kwao ni zimebaki paukwa pakawa,watu wanaotakiwa kuimplement sheria haswa juu ya matumizi wakati wa uchaguzi wanafanya kazi zao kwa woga-woga ndio maana mpaka leo hii sidhani kama kuna chama ambacho kimepeleka financial statement za uchaguzi mkuu uliopita na kama inavyotakiwa ziwe published publicly...Hizi chaguzi ndogo ni upotevu wa rasilimali muda na fedha bila sababu ya msingi utafutwe utaratibu wa kum-replace mtu usiohusisha matumizi yaliyopitiliza ya hizi rasilimali..
 
Sophist

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
4,481
3,363
Ndugu,
Taarifa nilizozipata kutoka Ofisi Ndogi ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba ni kuwa Chama Cha Mapinduzi kimetumi jumla ya shillingi billioni mbili katika Uchaguzi Mdogo wa Igunga.
Ni hayo tu>
 
gogozito

Member
Dec 21, 2010
46
15
Katika kuonesha kukua kimaadil na nidhamu ya matumizi ya pesa,i watanzania tungependa baada ya mwezi kila chama kitupe mchanganuao wa mapato na matumizi ya pesa ilichotumia katika uchaguzi mdogo Igunga.
 
HAKI bin AMANI

Senior Member
Sep 5, 2011
156
34
Pole sana ndugu yangu Mdanganyika. Je, umepata hiyo taarifa toka tume ya maadili ama wewe ni mgeni hapa bongo umekuja hivi karibuni toka ughaibuni.
 
gogozito

Member
Dec 21, 2010
46
15
watanzania tungependa kujua gharama halisi za matumizi na pesa zilizotumika katika kipindi hiki kwa kila chama kutueleza ni shilingi ngapi kimetumia,
 
regam

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
269
49
Nami alikuambia kuwa nchi hii ni maskini? La hasha, si maskini ila wananchi ndo maskini. Sababu ya umasikini ni kwa kukamuliwa kodi etc
Ni haki ya msingi ya kikatiba kwa wananchi wa Igunga kupata.mwakilishi wao bungeni ila kwa mwenendo wa kampeni za.vyama vinavyoshiriki uchaguzi sio siri garama ni kubwa mno kuliko uwezo wa uchumi wa.nchi yetu.Ni muda muafaka sasa kuachana ni huu upuuzi wa utitiri wa vyama kwani si tu vinatafuna kodi za walalahoi lakini pia usanii wa kuwadanganya wapiga kura kwa ahadi hewa ni dhambi ambayo haiwezi kusamehewa hata kidogo
 
mchemsho

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
3,212
852
Kwa mujimu wa gazeti la tanzania daima la jumatano (kama sijakosea), liliripoti kuwa CCM imetumia billioni tatu kwa ajili ya kampeni zake huko igunga ikimaanisha kuwa kwa kura 26,000 kilizopata kilitumia wastani wa zaidi ya laki moja na elfu kumi na tano kupata kura moja pekee.! Hii inatoa taswira gani kwa uchaguzi mkuu ujao juu ya matumizi ya pesa kupindukia katika chaguzi zetu??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom