Gharama za serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama za serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamende, Nov 7, 2008.

 1. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2008
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wakuu
  Heshima mbele!!!!
  Ninawataka radhi kwamba nilikuwa mbali kidogo ya mtandao na hivyo sikuwa katika mijadala kwa takribani wiki 5. hata nilipopata kanafasi kidogo kuingia hapa jukwaani haikuwa rahisi hata kidogo kushiriki kikamilifu mjadala kwa undani.

  Waheshimiwa sana, wazalendo, wapenda nchi ya Tanzania.
  Leo ninakuja na ombi la kujua gharama halisi za uendeshaji wa serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Ninatamani kujua kwamba serikali inatumia kiasi gani kwa:

  1. Uendesheja wa Ikulu na wizara zilizoko pale
   Ofisi ya waziri Mkuu na wizara zake.
   Ofisi ya Makamu wa Rais na Wizara zilizoko chini yake.
   Wizara zote moja moja
   Uendeshaji wa Ofisi za Mikoa na Wilaya
   Uendeshaji wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya
   Uendeshaji wa Mhakama
   Gharama za Bunge
   Gharama za Majeshi ya ulinzi
   Gharama za Majeshi ya Usalama wa Raia
   Gharama za Uendeshaji wa Vyuo.
   Gharama za Utafiti
   nk.

  Baada ya hapo tujue kila Mtanzania anatakiwa kuchangia kiasi gani kwenye kuwezesha huo uendeshaji baada ya kutoa mchango wa wahisani.
   
 2. I

  Iga Senior Member

  #2
  Nov 7, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  GHARAMA ZA SERIKALI ZINAWEZA KUPUNGUZWA, JE, SERIKALI IKO TAYARI KUFANYA HAYA?  Kuna njia mbalimbali za kupunguza gharama za serikali:

  1. Kuacha kununua magari ya bei mbaya toka nje na kukopi gari moja (Ardhi-rover) na jeshi kupewa changamoto ya kuzalisha gari hilo kwa ajili ya matumizi ya wakubwa wote wa serikali kama India ilivyofanya na gari lake la viongozi.
  2. Kujenga ghorofa moja yenye pande tatu pale Dodoma ili serikali nzima ikae pamoja. Bado mawaziri watakuwa na ofisi ndogo Dar na mikoani panapostahili.
  3. Bunge kuainisha masuala ya kimkoa na kitaifa na kuachia mabaraza ya wawakilishi mkoani kuzungumzia yale ya mkoa na Bunge la taifa kuzungumzia yale ya kitaifa.
  4. Kupunguza ukubwa wa serikali kwa kuwa na wizara kati ya 14-18 tu.
  5. Kuzigeuza Wizara nyingine wakala au taasisi za kutoa huduma husika.
  6. Kupunguza safari za nje na ukubwa wa misafara safari hizo zinapokuwa za lazima.
  7. Kuhakikisha masuala ya matatizo ya Afrika yanalipiwa ama na AU au UN.
  8. Kudhibiti ununuzi wa mashine, zana na vifaa toka nje. Ili kupunguza gharama zinazoongezwa na tenipasenti.
  9. Kuhakikisha kuwa mkuu wa mkoa au gavana wa mkoa analipwa kulingana na mapato ya mkoa wake na jinsi walivyofanikiwa kupunguza gharama.
  10. Kuwa na ndege ya mizigo ya serikali inayosambaza mizigo ya kila mkoa hadi mkoa husika au mkoa wa karibu.
  11. Kuwa na ndege, mabasi, boti na malori ya serikali kusafirisha watumishi wa umma kwa gharama nafuu.
  12. Kupunguza maofisa balozi katika nchi ambazo hatuna masoko makubwa wala faida nyingine za maana.
  13. Kupunguza matumizi ya karatasi, bahasha na makalabrasha kwa kutumia zaidi wavuti na tovuti.
  14. Kupunguza au kukata fedha zinazolipwa magazeti ya serikali na TBC ili vyombo hivyo vijiendeshe vyenyewe kama redio za watu binafsi.
  15. Serikali kukarabati majengo mazuri kati ya jiji na kuyakodisha kwa watu binafsi nayo itafute majengo madogo lakini yanayofaa nje ya mji. Fedha inayopatikana katika kukodisha majengo ya zamani itoshe kuendesha majengo mapya madogo.
  16. Wizara na idara zote za serikali zitumie LUKU.
  17. Utaratibu wa kulipa kampuni za simu mabilioni ya fedha katika kile kinachoitwa 'pay after use' ukome na badala yake kila ofisa agawiwe fungu lake na anun ue kadi za prepaid.
  18. Simu zote za TTCL katika wizara na idara za serikali ziwe za prepaid.
  19. Pawe na resheni ya peteroli na dizeli kwa kila ofisa wa serikali nayo isizidi lita50-70 kwa wiki.
  20. Serikali idhibiti utoaji matangazo katika televisheni na kulazimisha gharama hizo kuwa chini kwa serikali kuondoa kodi zote za kijinga zinazoongeza gharama za matangazo kwenye redio, televisheni na magazeti na kufanya gharama hizo kuwa kubwa kuliko kipato cha serikali.
  21. Kuzuia mizigo inayoondolewa bandarini na airport bila kulipiwa.
  22. Kuangalia upya mishahara ya wateuliwa wachache kwenye sehemu kama Wizara ya Fedha, TRA na taasisi nyingine tukizingatia kwamba 'credit crunch' Marekani na Ulaya imesababishwa kwa kiasi fulani na mishahara mikubwa ya viongozi wa serikali, watumishi wa umma na mameneja wa makampuni.

  Je, mpaka hapa tumewasaidia kwa kiasi gani wachovu wetu?
   
 3. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Hapo naunga mkono. Serikali ianaweza kuanzia hapo. nina hakika tutaokoa hela nyingi sana na kuzipeleka kwenye mambo muhimu kama afya. elimu na miundo mbinu.
   
Loading...