Gharama za mtoko (Date): Kati ya mwanamke na mwanaume, nani huwa anaumia…?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
black-couple-on-a-date-pf-378x334.jpg



Maisha ya vijana wa siku hizi yamebadilika sana linapokuja swala la kutafuta mwenza, tofauti na miaka ya zamani. Siku hizi vijana wengi hutumia mitoko kama njia ya kutafuta mwenza kwani kwa kuwa na mtoko na mwanamke aliyevutiwa naye humpa fursa ya kujuana na mwanamke huyo ili kupata fursa ya ya kufanya maamuzi sahihi.

Mtoko *(date) ni ghali sana, na kwa bahati mbaya gharama za mitoko mara nyingi zinakuwa hazipangwi bali hutokea tu, kulingana na makubaliano wa wawili wapendanao, na gharama hizi huwaweka wahusika katika wakati mgumu na pengine kuwaingiza katika madeni.
stare.jpg

Ipo dhana imejengeka kwamba wanaume ndio huumia zaidi kwa gharama za mitoko kutokana na kwamba imezoeleka kuwa wao ndio wanaopanga mitoko hiyo, hivyo wao ndio hubeba gharama hizo za mitoko. Tumeshuhudia hata hapa JF katika jukwaa hili la MMU, kuwaona wadada wakishupalia kwamba hawapaswi kulipa chochote wakati wa mtoko kwa sababu wao ndio wamealikwa.
braids.jpg

Lakini jambo ambalo wengi hawalijui hususan wanaume ni kwamba, wanawake hubeba gharama kubwa kwa ajili ya mitoko. Unaweza kujiuliza kwamba gharama hizo ni zipi?

Ni swali zuri, lakini kabla sijajibu swali labda nikuulize swali moja. Hivi unajua ni kiasi gani wanawake hujiuliza kwamba ni kivazi gani watupie wakati wa mtoko?

Kwa taarifa yenu, wanawake huwa wanafanya maandalizi makubwa sana kabla ya mtoko na maandalizi hayo yanaanzia kwa kununua kivazi kipya (hii hutokeas sana), kutengezeza nywele , kutengezeza kucha na mambo ya vipodozi na vikorokoro vingine kabla ya kwenda kwenye mtoko. Mwanamke huweza kubeba gharama hizi kwa mtoko wa kwanza, wa pili na watatu… na hiyo itategemea viwanja anavyokutania na mwenzi wake.

Swali ambalo ninataka tulijadili hapa ni Je, ni nani huwa anaumia kwa gharama za mitoko kati ya mwanamke na mwanaume?


Naomba mtiririke hapa maana kesho na mie nina Ki-Date……….LOL
 
Kwa mtazamo wa haraka haraka mwanaume anaumia zaidi katika gharama za mtoko wenyewe, kama hana gari, pesa ya tax kwenda na kurudi, gharama ya kila kitu watachokitumia siku hiyo.

Kwa upande wa pili mwanamke umgharimu zaidi kwa uchukua muda mwingi kujiandaa na mtoko kuliko mwanamme, mathalani kununua viwalo vipya na kujiweka kisoap soap, huwa inamgharimu sana mwanamke.
 
Mwanaume huingia gharama sana kwani huwa na hofu saa zingine kwani hajui kwanza watatumia shilingi ngapi jambo linalomfanya atembee na Master Card, lakini pia wanawake husema kabisa kwamba nataka niende saloon nikaoshe nywele niwezeshe, mara baby kuna gauni zuri nataka nitoke nalo, kiatu kipo kwa fundi(umununulie kipya),

MWANAUME ANAINGIA KTK GHARAMA KUBWA SANA HASA YA HOFU SHILINGI NGAPI? UNAWEZA BEBA 500,000..UKAJIKUTA BADO UNAHISI HAITOSHI, ME NAONA SEHEMU ZA STAREHE WAWEKE HUDUMA ZA CARD ILI TUSIWE NA HOFU.....
 
We nawe, kila siku kazi yako kuguna tu........
Haya sema una guna kitu gani sasa, sema kama unatunia kiasi gani kwa kujipodoa kabla ya mtoko.........................LOL

nikisema utaweza kuyabeba............?!?!!?:eek:hwell::shut-mouth:
 
its still the man who pays more. think about it this way
  1. 1st date, mimi ndio ntalipa for the whole thing. food/transport/entertainment etc. gharama zako za nguo/vipodozi sio point for 1st date after all hautanunua vipodozi/nguo mpya every time unaenda date (lol) and I'm sure una nguo 'za kanisani' unazoweza kuvaa kwenye mtoko.
  2. kama ni wapenzi/wanandoa recent, usually the asker ndio analipa but mwanaume hatupendi kulipiwa coz inaleta noma kidogo. hasa kwa hawa wadada wa dot.com, wataanza kujigamba na kuleta vidharau
 
Ni yule jirani yako ameanza kutafuta wa mtoko eti eeh,
mwambie akiona vinaelea vimeundwa; inabidi ajitahidi kubeba tu gharama zote.
 
Mtambuzi,
formula ni kuwa mwanaume atalipa, unless mie ndo niwe nimemwalika huyo mwanaume.....

akithubutu kunialika halafu nikashare cost in any way asahau kidate kingine....
 
Last edited by a moderator:
wanawake ni wa wabinafsi sana, kama gharama ataingia ni gharama binafsi za kujipendezesha yeye,

wanaume sisi sio wabinafsi gharama tunaingia zaidi kuliko mwanamke tena ni gharama za pamoja!
 
si huwa mnataka haki sawa?

nikienda na demu mahali nikanunua chakula yeye akanunua vinywaji au vice versa, tha gal will not get out of my mind, nitamrespect mpaka basi!

Mtambuzi,
formula ni kuwa mwanaume atalipa, unless mie ndo niwe nimemwalika huyo mwanaume.....

akithubutu kunialika halafu nikashare cost in any way asahau kidate kingine....
 
Kwa maelezo yako Mtambuzi, gharama kubwa anakuwa nayo Mdada kuliko Mkaka. Mkaka anatoa gharama za mtoko tu ilhali mwanamke anajiandaa sana katika kuhakikisha anamshika kihalisi mwanamme kwa wasifu wake wa nje.


Bazazi!
 
Last edited by a moderator:
Juzi juzi hapa Lara1 alikuja anajuta kushobekea vi offer mbuzi.
Ambapo kuna jamaa alimuinvite lara1 somewhere bada ya kuspend, bill ilipoletwa mshkaji akashindwa kulipa bill, ikabidi manzi abebe mzigo wote kudadadeki.

All in all mara nyingi kama sio zote mwanaume ndie anaegharamika compared to women.
 
Back
Top Bottom