Gharama za mawakili kitanzi kwa wanyonge

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Gharama za kuweka mawakili kwenye kesi mbalimbali ni kubwa hivyo wananchi wa kawaida wamekuwa wakishindwa kuzimudu.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na mjumbe wa mpango wa kutathmini utawala bora nchini (APRM), Severinus Hyera, wakati akizungumza kwenye mkutano baina ya majaji na wajumbe wa mpango huo.
Alisema hata gharama za kufungua kesi nazo ni kubwa na zimekuwa kikwazo cha wananchi wa kawaida.
Hyera alisema kumekuwa na uhaba wa Majaji wa mahakama maalum ambazo ni muhimu kwa maisha ya watu hasa Mahakama Kuu vitengo vya Ardhi na Biashara na Mahakama za Kazi.
Alisema vitengo hivyo viko Dar es Salaam pekee hivyo wananchi wa mikoa na wilaya nyingine nchini wanakosa huduma hiyo.
Hyera pia alizungumzia umbali wa baadhi ya mahakama kuwa ni kikwazo cha upatikanaji wa haki za msingi za watu.
Alisema mahakama za mwanzo na zile za Hakimu Mkazi zimetawanyika kwa kiwango kizuri lakini Mahakama Kuu na ile ya Rufani ziko mbali na wananchi.
Alisema hali hiyo kwa kiwango kikubwa inatokana na ufinyu wa bajeti ambayo hutolewa na serikali na uhaba wa watendaji.
Kuhusu msaada wa kisheria, alisema kwa sasa unatolewa kwa wale wenye kesi za jinai pekee tena zile zenye masuala magumu kama vile mauaji au uhaini.
Alisema wananchi wenye kesi nje ya hizo hawana uwezo wa mawakili wanasema kuwa hicho ni kikwazo kwa kupata haki zao.
Alisema jitihada mbalimbali zimefanywa ikiwemo kuingiza mtaala wa Sheria za haki za binadamu katika elimu ya sekondari.
Alisema vyuo vikuu zaidi ya sita kwa sasa vinatoa elimu ya Sheria kwa kiwango cha Shahada ya kwanza.
 
Back
Top Bottom