DA HUSTLA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2012
- 3,663
- 3,882
Ndio maana wanaamua kwenda uarabuni tu.Huduma za afya zina gharama na hii ndiyo sababu watu wengi wanaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu. Wengine wanakwenda kupiga ramli kwa kuanguka na kuzimia bila kujua kuwa hii ni dalili ya hatari na inahitaji uchunguzi wa kitaalamu. Wengi huponea hutoa sadaka kanisani ili waombewe. Kuna wanaokwenda kwa Mwamposa kisa wanaharisha. Hili si kusudio la mada.
Nia yangu ni kuongelea matibabu ya hawa wanaotusaidia kazi za ndani. Kuna wanao ambiwa wajinunulie Bima ya Afya kutoka kwenye mishahara wao. Wengine wanaunganishwa kwenye bima ya familia (Hawa ni wachache sana).
Kuna mama mmoja alimtoa binti wa kazi Dodoma, binti alikua mdogo kama miaka 16. Wazazi wake walimtoa kutokana na ugumu wa maisha wakitegema kurushiwa hata 20,000 kutoka katika mshahara wake kila mwezi.
Yule mtoto alikuwa mgonjwa, alianguka mara nyingi baada ya kuamka asubuhi. Yule mama alimpeleka hospitali. Vipimo vya siku ile vilimgharimu laki tatu na mtoto aligundulika na matatizo ya moyo.
Yule mama alilaani sana kutumia laki tatu hospitali. Alimsimanga binti kuwa kama ulijua ni mgonjwa kwanini ulikubali kuja kwangu. Baada ya pale alimrudisha kwao. Ukizingatia hali za maisha ya wazazi wa binti Yule ni wazi kuwa hawataweza kumtibu mtoto wao.
Tunapotoa ajira kwa hawa ndugu zetu wanaotusaidia majukumu ya kulea watoto na wazazi wetu, tukumbuke pia kuwa wao ni binadamu na kuwe na utaratibu wa kuwasaidia katika matibabu. Mnaweza kushauriana nae apate Bima yake ya Afya.