Gharama za matibabu ya viongozi wastaafu ni kufuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama za matibabu ya viongozi wastaafu ni kufuru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jul 8, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,189
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Gharama za matibabu ya viongozi wastaafu ni kufuru [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 05 July 2012 20:39 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] Mwananchi

  Bunge linaloendelea na kikao chake mjini Dodoma, juzi liliambiwa kwamba Serikali imetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya kugharamia matibabu ya viongozi wakuu wastaafu. Akihitimisha mjadala wa hotuba yake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti na Utumishi wa Umma, Celina Kombani alisema fedha hizo ni kwa ajili ya wastaafu wanaopaswa kutunzwa na Serikali.

  Bila kuelezea suala hilo kwa undani, Waziri Kombani alisema tu kwamba kiwango hicho kimepungua mwaka huu kutoka Sh10 bilioni zilizotengwa mwaka jana hadi Sh9 bilioni mwaka huu kutokana na idadi ya viongozi wastaafu wanaopaswa kuhudumiwa na Serikali kupungua. Wastaafu wanaoangukia katika fungu hilo ni marais Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

  Mawaziri wakuu wastaafu ni Joseph Warioba, Samuel Malecela, Cleopa Msuya, Salim Ahmed Salim na Edward Lowasa. Waziri Kombani hakuwataja viongozi wastaafu waliopungua, lakini sote tunafahamu fika kwamba Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na Mzee Rashid Mfaume Kawawa tayari wametangulia mbele ya haki.

  Bila shaka takwimu hizo zitakuwa zimewashangaza wengi kutokana na wingi wa fedha zinazotengwa kila mwaka kugharamia tu matibabu ya viongozi, bila kutilia maanani fedha nyingine nyingi zinazotengwa kama mafao ya viongozi hao wastaafu. Kwa akili ya kawaida, fedha hizo ni nyingi mno kulinganisha na idadi ya viongozi waliokusudiwa na takwimu hizo zinaacha maswali mengi kuliko majibu.

  Tunasema hivyo kwa sababu hatuoni jinsi kiasi hicho kikubwa cha fedha kinaweza kugharamia matibabu ya idadi ndogo sana ya viongozi wetu wastaafu, kwani siyo siri pia kwamba wastaafu wetu wengi wamekuwa wakipatwa na maradhi ya kawaida ambayo siyo tu hayahitaji fedha nyingi kuyatibu, bali pia yangeweza kupata tiba hapa nchini. Ndiyo maana tunasema vifungu vikubwa vya fedha zinazotengwa kila mwaka kwa shughuli hiyo siyo tu vinatia shaka, bali pia vinaacha ukungu na kiza kinene vikiwa vimetanda.

  Sisi hatusemi kwamba viongozi wetu hao wastaafu hawastahili kupata matibabu kwa kodi zetu. Tunachosema hapa ni kwamba gharama za matibabu yao hazipaswi kuwa siri au kuacha shaka hata kama wastaafu hao walitutumikia vizuri wakati wa utawala wao. Ni sahihi kabisa kwamba walipakodi wangetaka kujua kodi zao zinavyotumika kuwagharimia viongozi wao.

  Bado tunasisitiza kwamba Sh9 bilioni kwa matibabu ya viongozi hao wastaafu siyo tu ni nyingi mno, bali pia ni kufuru na za kufikirika. Takwimu hizo hazijumliki hata kidogo. Ni matibabu yapi yenye gharama hata robo ya kiasi hicho kilichotengwa, hata ukiweka usafiri, malazi na gharama nyingine? Ni kichekesho kwamba fedha hizo zimepitishwa na Bunge.

  Kinachosikitisha ni Bunge kutohoji fedha zote hizo zinakwenda wapi. Bunge lisiloona umuhimu wa kuibana Serikali iboreshe mazingira na huduma katika hospitali zetu ili viongozi na wananchi watibiwe katika hospitali hizo badala ya kupeleka fedha zetu nje na kujenga uchumi wa nchi nyingine. Ebu fikiria hili: Mwaka uliopita, wagonjwa waliopelekwa India kutibiwa mwaka wa fedha uliopita walitumia Sh7 bilioni zikiwa kodi za wananchi.

  Kwa nini tusitumie fedha hizo kuleta vifaa na wataalamu kutoka nje kwa lengo la kuimarisha hospitali zetu na wataalamu hao kutusaidia kujenga uwezo wa wafanyakazi katika hospitali zetu na sekta ya afya kwa jumla? Lengo la kuweka sheria ya mafao ya viongozi ilikuwa njema ili viongozi wetu wasiishi maisha ya mashaka baada ya kustaafu.

  Bahati mbaya hakuna aliyejua kwamba baada ya kuzikwa kwa Azimio la Arusha viongozi wetu wangetupilia mbali maadili ya uongozi na kuwa matajiri wakubwa, wengine wakifanya biashara na kuanzisha makampuni hata wakiwa bado katika ofisi za umma. Ndiyo maana tunalazimika kusema kuwa, huko tuendako tutalazimika kuangalia upya mafao ya viongozi, hasa suala hili la kutumia mabilioni ya fedha kila mwaka kwa matibabu ya kufikirika ya viongozi wetu.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. kalou

  kalou JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2012
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 997
  Trophy Points: 280
  hivi kwa mfano kwenye hizo bil 9 walizotengewa waki2mia bil 5 ,hizo bil 4 zinarudishwa?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,189
  Trophy Points: 280
  Kwa ufisadi ulivyokithiri ndani ya Serikali sidhani kama zinarudishwa bali huwa zinaingia mifukoni mwa wajanja wachache. Wakiambiwa watoe details ni kiasi gani kilichotumika katika miaka mitano iliyopita na payment receipts husika za matibabu ya Mwinyi na Mkapa basi wataanza kung'aa macho.
   
 4. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Sumaye amesahaulika akawekwa Lowasa?Kumbe Lowasa ni Waziri Mkuu Mstaafu!!!
  Hizo hela zitakuwa za kuwatibu wao,wake zao,watoto wao,ndugu zao mpaka na mifugo yao!!
  Kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa!!!
   
 5. C

  Chibenambebe Senior Member

  #5
  Jul 8, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kiukweli Tanzania mambo ni magumu na yanatia hasira mpaka basi. Uvumilivu utaja fika mwisho tuu!!!
   
 6. O

  Original JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tanzania ina wenyewe, wengine wote ni wapangaji tu.
   
 7. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,377
  Likes Received: 8,532
  Trophy Points: 280
  Hii aibu halafu hakuna hata mmoja anayetibiwa ndani ya nchi
   
 8. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Watatibiwa tu. Liwalo na liwe!
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,189
  Trophy Points: 280
  Ndio maana hawaoni umuhimu wa kuboresha sekta ya afya nchini maana wanajua watapelekwa nje kwa gharama za pesa za walipa kodi. Pesa za kuwalipia wao kutibiwa nje siku zote hazikosekani ila wakiulizwa pesa za kuboresha sekta ya afya nchini hawakawii kung'aka, "Serikali haina uwezo."
   
 10. kalou

  kalou JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2012
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 997
  Trophy Points: 280
  Huku wakipitia wale wakaguzi wa matumizi ya serıkali si itakuwa aibu tupu.
   
 11. P

  Pulpitis Senior Member

  #11
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli tanzania italiwa na wenye meno, Drs wana watete wananchi sababu wanajua madudu haya, watu wanawaona wasaliti, haya siku moja mtawakmbuka.
   
 12. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Naona kama wizi au kulipana fadhili. Lowassa anaingiaje wakati hakustaafu? Walaji wastaafu au?
   
 13. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Pamoja na gharama hizi za matibabu hawa viongozi wastaafu huwa wanabadilishiwa gari kila mwaka. Pia wanalipiwa dreva, gardener, mpishi na walinzi na pesa za chakula. Kwa kifupi ni kwamba wanatunzwa na pesa za walipa kodi kwa asilimia 100 mpaka watakapoondoka hapa duniani. Cha kushangaza ni kuwa pamoja na hayo yote jamaa hawaridhiki na wanaiba na kuiuza nchi. Hii nafikiri ni laana isiyo na mfano.
   
 14. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,062
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Kujibu swali lako, hazibaki, na kila mwaka inabidi ziongezwe kwani hazitoshi, hasa ifikapo mwezi wa Ogasti.
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  OH Yeah Sikujua kuwa FREDRICK SUMAYE hakuwa Waziri Mkuu kwa Miaka 10 alikuwa nani then?

  Hizi Habari zetu zinaandikwa bila kufuatilia zinaondoa umaridadi wa kuzisoma kweli; too many

  mistakes
   
 16. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  ukute huwa wanapewa hizi hela!
   
 17. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Majenerali wa jeshi wastaafu wote wanatibiwa nje, ni marehemu kyaro alikataa akabaki bugando hadi kifo chake.
   
 18. a

  andrews JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [h=2]kikwete ni mnafiki no 1[/h]
  Tangu tupate maraisi hatujawahi kuwa na rais mnafiki, mzembe,dhaifu na ndumila kuwili kama kikwete uendeshaji serikali yake umejaa fitina dhihaka na upuuzi mwingi anyemshabikia huyu naomba aweke haya maelezo kwa kuprint au kucopy na baa ya 2015 mtaona kwa nini tz imefika hapa ilipo ni sababu ya huyu mr dhaifu hakuna alichowahi kuongoza kikafanikiwa zaidi ya kutengeneza makundi ndani ya chama na nchini ili awe madarakani kirahisi mungu ibariki tanzania kwa haraka sana tuondokane na huyu mnafiki
   
 19. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Yaani matibabu tu kila mtu ana wastani kama wa bilioni moja na usheeeee! Ndo maana kila mtu anataka awe rais ndani ya magamba wanajua utaishi kama malkia wa nyuki pindi madaraka yakiisha, hapo mbali na mali za kifisadi ambazo tayari wanazo, aiseeeee!
   
 20. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  ndio maana kuepusha haya matatizo ndio maana kwa wenzetu huko Marekani Rais analipwa mafao kwa miaka 10 baada ya kustaafu na baada ya hapo anaweza kuongezewa miaka 5 kwa executive order ya sitting president. Hii ni kuzuia mtu kutumikia urais kwa miaka 8 halafu alipwe mafao miaka 20! Hivyo ukiamua kugombea Urais ukiwa na umri mdogo ni juu yako. Mfano mwaka jana nakumbuka Rais Carter aliibiwa baiskeli yake alipoenda dukani kwa vile kwa sasa hana ulinzi wa aina yeyote ingawa FBi wanaendela kumfuatilia kwa extra security lakini sio kama huku kwetu.
   
Loading...