Chendembe
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 416
- 462
Wadau, nimekuwa mhanga wa gharama za matibabu hali iliyonisukuma kuandika mada hii.
Aidha, nimeguswa kwa masikitiko kauli mbalimbali za viongozi wetu katika suhala la afya nchini.
Nategemea na ukoo wangu, ivyo, sinashaka mnafahamu ninavyosumbuka. Hali hii inanifanya kuwaza kipi bora kufanywa na Serikali kwa Sasa; Kuendelea kujenga majengo au kuongeza upatikanaji wa dawa au kutoa ruzuku kwa sekta ya afya ili gharama zishuke?
Jamani, hali ni mbaya, watu wanashindwa kumudu gharama za afya na kupelekea watu kununuwa vijidawa bila vipimo au kutibiwa kienyeji na wengine kufia majumbani.
Tumezika Jana dada yetu ambaye alilazwa hospitali Fulani na baada ya kuzidiwa, akapewa rufaaa kwenda Mhimbili, kilichotokea ni uzuni, mume alilia Kama amechomwa moto na kulazimisha mgonjwa apewe ruhusa arudishwe nyumbani. Dokta alimruhusu na kafa nyumbani. Tulipomuuliza shemu, alijibu heri nimzike mwenyewe kuliko Jiji.
Nashauri tozo zielekezwe katika ruzuku ya matibabu na ziada tu ndo iangalie ujenzi mpyaa.
Pia, ruzuku isaidie kushusha gharama za kukata bima ya afya kwa wananchi.
Zaidi, nashauri kuundwa kwa mamlaka ya kudhibiti gharama za matibabu nchini.
Nawasilisha