Hivi karibuni niliona sehemu ya barabara ya pugu ikiwa inafanyiwa marekebisho ambayo yanatokana na kutuama kwa maji maeneo ya karibu na Q/plaza.
Nasikia hata misafara ya wakubwa iliwahi kutaka kukwama pale.
Lakini maamuzi ya matumizi makubwa namna hii ya fedha za umma yanatakiwa yawe yanazingatia utaalamu zaidi.
Ile barabara haikuwa na hilo tatizo kwa miaka mingi tu baada ya kujengwa na ikitumika bila shida wakati ile mikondo ya maji ilipokuwa wazi. Nadhani kilichotokea ni kwamba wameuziwa watu viwanja kwenye ile mikondo wakaijaza na kujenga majumba ya biashara na kusababisha maji kukosa pa kutokea.
Lakini serikali badala ya kuliangalia kwa busara zaidi na kitaalam, haraka ikaanza kuwaza ni nani apewe hiyo tenda.
Maamuzi kama haya huchangia sana kudhoofisha uchumi wa nchi changa.
Naomba tutafakari.