Gharama za kwenda serengeti na ngorongoro kwamapumziko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama za kwenda serengeti na ngorongoro kwamapumziko

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by frozen, Jul 3, 2012.

 1. frozen

  frozen Senior Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Habari wanajamii,
  naitaji kufahamu gharama za mtu mmoja kwenda na kurudi serengeti na ngorongoro...kuanzia gharama za usafiri, malazi, chakula na gharama za matembezi ukiwa katika sehemu hizi za utalii
  mwenye taarifa ntashukuru akinijuza hapa.
  Asante sana
   
 2. t

  tabu kuishi JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kuna option mbili ya kwanza kama unakwenda ngorongoro crater panda basi hadi arusha ukifika arusha panda noha hadi karatu , ukifika karatu unatafuta guest house nzuri ya ukweli ni kama 10,000/= hadi 15,000/= (nauli ya noha ni 6000/= hadi 8000/= arusha karatu) halafu unakodi gari ya kukupeleka ngorongoro tdi au mkonga nje ni kati ya 80000/= hadi 150000/= unazungushawa siku nzima crater, ukiwa tayari nina watu nawafahamu wanaweza kukupokeya karatu na kukusadiya katika swala hilo
   
 3. m

  muhinda JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 336
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Hutapata majibu kwenye hii thread, inaelekea watu wengi hawana utamaduni wa kwenda vacation. Hata mimi nilijaribu kutafuta info za vacation humu sikupata wachangiaji
   
 4. t

  tabu kuishi JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  OPOTION YA PILI UNAKODI GARI LA TOURS TOKA ARUSHA WANAKUPA FULL PACKAGE YA AMBAYO INAJUMUISHA GHARAMA ZA USAFIRI MALAZI NA CHAKULA KWA SIKU UTAKAZO TAKA HOTEL UTAPELEKWA HOTEL ZA KIZUNGU NA ZA WAKUBWA aka wanene. NA UTALIPA DOLLARS
   
 5. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kutokea wapi?maana inategemea kama unaingilia mwz au arusha.
   
 6. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kama Una nia ya Kupumzika wewe piga simu tu Mkuu. Mboni makampuni mengi yanafanya hizi shughuli na gharama nafuu tu sio za kifisadi. Jaribu hawa mimi nilifanya hivyo nikiwa na mama na watoto and i am always a return customer to them.
  Welcome To Ebony Tours & Safaris
   
 7. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Huu ni ushauri mzuri na wa bei rahisi. Niliwahi kupita Ngorongoro nikiwa nasafiri kutoka DAR kwenda Mwanza na gari la binafsi na tulilala Karatu gesti nzuri bei ilikuwa 8000 mwaka 2006. Ila usiku ule majira ya saa 2 kulikuwa na milio ya bunduki, kumbe ni majambazi walivamia duka moja hapo mjini. Ni vizuri akalala Hotelini kwenye usalama zaidi. Na kisha akodi gari la tours kama ulivyomshauri kwa siku na bei ni hiyo around 150K.

  Hii option ni ghali sana ila inategemea na kamba yake. Kama ni ndefu basi afanye hivyo. It is more safe and comfortable
   
 8. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  mtu mmoja ni ghali zaidi hasa huduma ambazo ni sharable kama gari.
   
 9. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kama naenda na wife na mtoto kwa mfano halafu mimi najifikisha hapo Karatu nachukua Hoteli gharama za kunipeleka huko Mbugani na kurudi inakuwa how much?
   
 10. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa Mtanzania wa kawaida ambaye si Fisadi kwenda Polini kutalii kwa kutumia magari ya Watalii ni ghali sana na ndo maana TANAPA WANAJARIBU KUHAMASISHA KWA WATU KWENDA KWA KUTUMIA USAFIRI WA TANAPA ILA NI KWA BAADHI YA HIFADHI AMBAZO SI ZA KULALA HUKO MFANO
  1. ARUSHA NATIONAL PARK

  2. TARANGIRE

  3. LAKE MANYARA

  KWA UPANDE WA NGORONGORO WAO HAWANA HUO UTARATIBU NA UKIZINGATIA KWAMBA TANAPA NA NGORONGORO CONSERVATION AREA NI VITU VIWILI TOFAUTI,

  ILA KAMA JAMAA ALIVYO SEMA HAPO UNAWEZA TUMIA OPTIONAL HIZO, ILA KWA KUONGEZEA

  1. KWA HIFADHI ZA TARANGIRE, MANAYARA NA ARUSHA NATIONLA PARK HAKUNA SHIDA KABISA MAKE SEHEMU YA KULALA INAPATIKANA

  TARANGIRE- Hapa unaweza kwenda na gari lako au la kukodi na ukarudi kulala either Arusha town, Babati town, Mto wa mbu au Karatu

  2. MANYARA NATIONAL PARK- Hapa unaweza kwenda kwa usafiri wako au wa kukodi na ukarudi kulala Mto wa mbu, Karatu au Arusha Town

  3. ARUSHA NATIONAL PARK- Hii ndi hifadhi cheap kwan unaweza hata kwenda na mark II yako na ukarudi kulala A town

  4. NGORONGORO- Hii unaweza tumia usafiri wako au wa kukodi, ila kama ni usafiri wako hakikisha ni gari la 4WD vinginevyo hutaruhusiwa kushuka creter, na hata kama wewe ndo Dreva na gari ni la 4WD ni lazima uwe na mtu mzoefu akuendeshe zile barabara ni noma hukawii kupiga chini na gari lako, na MADREVA wageni wengi wanaopita hizo njia kwenda hata MUSOMA HUWA WENGI WANAPATA MISUKOSUKO SANA

  KULALA- Hapa kama umekodi gari ni lazima uwe na pesa ya kutosha na isiwe ya mawazo hapo unaweza lala hoteli kama SERENA, CRETER LODGE, NGORONGORO WILDLIFE LODGE, SOPA LODGE NA KAZALIKA HAPA UKITAKA BEI ZAO WEWE google tu zipo na huitaji kusimiliwa, ILA NI GHALI SANA TENA SANA WAPO HATA WAZUNGU WANAOSHINDWA HIZO BEI ZA KULALA
  KULALA- Au unaweza lala sehemu inaitwa KIMBA kwa wamasai ni gest house ila haiko freshi, au urudi kulala KARATU

  5, SERENGETI- Hii ndo hifadhi Ngumu kuriko zote na hapa ni lazima ujipange vya kutosha make kule hakuna UJANJA NI LAZIMA ULALE TU INGAWA KUNA OPTIONAL KIBAO
  - Hapa ni lazima ukodo gari za tours au utumie la kwako wewe na familia yako na ni lazima liwe 4WD kwa sabau barabara za kule zina vumbi na mchanga wa kufa mtu so hukawii kukwama na ni lazima uwe na Mzoefu wa kukuendasha kwani SERENGETI NDO HIFADHI YENYE AJARI NYINGI SANA, KAMA WEWE HUNA UELEWA WA ZILE BARABARA KUPIGA CHINI SI KITU CHA KUSHANGAZA KABISA

  KULALA- Hoteli za kitalii, SERENA, SERENA KILAWIRA. LOBO WILDLIFE LODGE, SERONERA WILDLIFE LODGE, SOPA LODGE, SERENGETI KEMPISK HOTEL- Hizi hoteli ni ghali sana kwa PESA ZA MAWAZO HUWEZI LALA HUMO

  KULALA- Camp KAMA MKO WENGI MNAWEZA NENDA NA MAHEMA YENU AU YA KUKODI NA MKAPIGA CAMP SEHEMU ZIPO ILA NI LAZIMA KULIUPIA MAKE MNAPEWA NA ASKARI WA KUWALINDA MWENYE BUNDUKI MSIJE KUVAMIWA NA TEMBO AU MAJANGIRI

  - HOSTEL YA TANAPA- Hii ndo sehemu ya kulala iliyo cheap kuliko zote ila booking inahitajika mapema sana make zinatumiwa sana na wanafunzi na hata wazungu wasio kuwa na uwezo wa kwenda kwenye hoteli kubwa, ILA NI SAFI NA ZINA VIWANGO

  - MUGUMU SERENGETI- Hapa manweza maliza kuzunguka makenda kulala KWENYE MJI WA MUGUMU ni kama kilomita 70 kutoka Seronera

  SO Mkuu ghalama kubwa ya kwenda kwenye hizo hifadhi mbili iko kwenye kulala na chakula na wala si usafiri magari ya kukodi ya bei che yako mengi sana, ishu ni kulala na chakula, na hata chakula mnaweza beba je kulala?

  HOTELI HIZI
  SERONERA, LOBO WILDLIFE LODGE, NGORONGORO WILDLIFE LODGE NA MANYARA wakati zikiwa za Serikali kabla ya kuuzwa walikuwa na bei nzuri kwa ajiri ya Watanzania, ila baada ya kuuzwa nazani wamiliki wake hawana huo utaratibu tena
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hakuna usafiri wa moja kwa moja kutoka Dar...kwa mfano ndege au helikopta?
   
 12. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni pesa yako tu,

  1. Magari- Unaweza book na wakakufuata Dar ila ni wewe na na hizo kampuni za tours tu

  2. Ndege- Unaweza Panda ndege Ndogo lakini zinazo fanya safari kati ya Seronera, Manyara, Arusha, Zanzibar, Dar na kwingineko,

  It means Ukipanda hizo ndege hadi seronera utapokelewa na Kampuni ambayo mtakuwa mmesia kubalina nayo na unaweza maliza kutalii ukapanda ndege huko huko Ukarudi Dar

  Ila ni lazima ujipange make hapo hakuna cha bei za watanzania wala wageni, waote ni sawa
   
 13. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Asante sana, umekuwa wa msaada mkubwa.

  Ningepata mtu wa kunipa makadirio ya hiyo safari kwa ndege ningeshukuru mno pia
   
 14. crunkstaa

  crunkstaa JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2017
  Joined: Aug 4, 2012
  Messages: 293
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  ASANTE SANA MKUU,JAPO ULITOA USHAURI SIKU NYINGI LAKINI BADO UNAISHI!!!!
   
 15. manizzle

  manizzle JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2017
  Joined: Apr 29, 2015
  Messages: 1,876
  Likes Received: 1,835
  Trophy Points: 280
  Nimewahi kwenda huko ila kwa usafiri binafsi hivyo sikuwahi kulala. Ila sopa lodge nimefika aisee

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 16. Ngozi Joram

  Ngozi Joram JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2017
  Joined: Sep 9, 2016
  Messages: 587
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 80
  Frozen asante kwa uzi huu walau na mm nimejifunza

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 17. a

  antimatter JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2017
  Joined: Feb 26, 2017
  Messages: 443
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Taarifa nzuri
   
Loading...