Gharama za kuwekewa umeme Tsh. 27,000 Tanzania nzima. Je, hii siyo credit kwa Rais Samia suluhu?

Hilo ni tamkwa kwa Mhemko.Shirika halitaweza kujiendesha hili.Tutashuhudia ucheleweshaji mkubwa wa kuunganishiwa umeme au kutengeneza mazingira ya Rushwa.
Labda kama unajaribu ku-justify irresponsibility ya TANESCO!! Hata wakati walipokuwa wanalipisha wananchi malaki ya pesa kwa ajili ya nguzo na kuunganishiwa umeme bado walikuwa wanategemea ruzuku ya serikali; kwahiyo hakuna jipya hapo! TANESCO wape kila kitu bado watadai rushwa! Waambie watoze nguzo moja kwa 5M bado watadai tu rushwa kwa sababu hizo 5M haziigii mifukoni mwao wakati rushwa inaingia mifukoni mwao!
 
Kamwe usimwamini mwanasiasa.

Kalemani aliwahi kusema nguzo ni bure, sasa Nenda tanesco uone kama watakuletea nguzo bure.
Maisha,na hata ukinunua nguzo bado inakuwa nyara ya serikali sio yako tena😆
 
Ni makosa makubwa kupima utendaji wa Rais kwa siku miamoja.
Toka 321,000 mpaka 27000.
Rais ameanza kuwaonesha wapi anaipeleka nchi na huu ndiyo utetezi kwa wanyonge.

Je, hili halimpi credit mama yetu Samia?
Hizo pesa ni hisani ya serikali ya Sweden kupitia SIDA. Kazi hii ilianza enzi za JK, Mama Samia na Magufuli wameendeleza tu kilichokuwa tayari kinaendelea. Pesa za kwanza kabisa za miradi hii ya umeme vijijini (rural electrification) zilitolewa na Benki ya Dunia kuanzia mwaka 2010 kupitia mradi wake wa TEDAP, ulipoisha ndipo Waseden wakaendelea na juhudi hizo, ambapo pia serikali ya Norway ilichangia kutengeneza rural electrification master plan pamoja na prospectus ya miradi ya umeme.
Nilitaka kuweka rekodi sawa.
 
changamoto ipo katika kukuunganishia huo umeme wenyew, kama ule wa 300,000+ tu ulikua unazungushwa wee!, huu wa 27K sijui itakuaje
 
Hizi ni kiki tu za kisiasa. Kuna siku mtakuja kuelewa tu.

Hivi jiulize kipindi cha nyuma wakati watu walikuwa wakilipia gharama kuunganishiwa umeme bado shirika lilikuwa linayumba (nguzo hamna) je itakuwaje kipindi hiki watu walipe tu 27,000?

Halafu kumbuka hapo hiyo 27,000/ ni VAT na inaenda TRA sio Tanesco.

Hapo hujajiuliza je mtu anaehitaji extension ya line nguzo labda 10 mfano nae atalipa hiyo hiyo gharama?

Hili suala tusikurupuke kushangilia mwishowe itakuja kuwa ni kiki tu ilitafutwa.

Waziri Kalemani na Tanesco wana wajibu wa kufafanua hili jambo watu wajue vigezo na masharti yake. Ila kusema kila anaetaka kuunganishwa alipe 27,000 hata kama anahitaji nguzo hiyo ni uongo wakuu. Haitawezekana.
 
changamoto ipo katika kukuunganishia huo umeme wenyew, kama ule wa 300,000+ tu ulikua unazungushwa wee!, huu wa 27K sijui itakuaje
ya 321k Chanika kuungiwa ni miezi minne, wale wa 27k kuungiwa si chini ya Mwaka au huungiwi kabisa
 
Ni makosa makubwa kupima utendaji wa Rais kwa siku miamoja.
Toka 321,000 mpaka 27000.
Rais ameanza kuwaonesha wapi anaipeleka nchi na huu ndiyo utetezi kwa wanyonge.

Je, hili halimpi credit mama yetu Samia?
Kuna ka ujanja ujanja kapo. Sasa hivi kwa wanaotaka kuingiza umeme hali umekuwa ngumu kuliko mnavyofikiria.
Tanesco ukiwaendea watakuambia unahitaji nguzo? Kama ndiyo utajaza fomu ila hawatakuja kamwe kufanya survey, au wakija hautakaa upate control namba. Kuna ka mgomo ka chini chini. Ukiongea nao binafsi wanakuambia hili limejaa siasa ndani yake, hakuna budget hiyo ndiyo maana hawatekelezi.
Kama hilo lingekuwa linatekelezeka leo tisingekuwa na mtu ambaye hana umeme kwake, maana ukilipa 27,000 unaletewa hata kama ni nguzo 4. Je, kiuhalisia iko hivyo?
Hapa wanaohusika ni wale walioko kwenye mradi wa REA tu, wengine wote wembe ni ule ule
 
Mjifunze na kuandika kwa usahihi, siyo kujifunza kisukuma pekee,
Dada nitake radhi,Mimi Wala sio wa kabila ilo la washamba,,
Sometimes mtu unaweza ukawa unachangia mada humu ukiwa una drive, au unabeba boksi sehemu, etc, kwaiyo usitegemee mtu ataandika kwa ufasaha kila muda dada angu
 
mbona tunaenda tanesco wao wanasema hawana mwongozo huo?acheni uwongo tunapotosha watu.ukienda tanesco wao wanasema hawapewa mwongozo huo na wao hawawezi kufanya kazi kwa matamko sasa tupieni humu ndani huo mwongo kama si siasa na propoganda tu?
 

Attachments

  • HOTUBA WAZIRI WA NISHATI MWAKA 2021_22 - Final Draft2 31.05.2021.pdf
    4 MB · Views: 6
Ni kweli, ni mpango wa siku nyingi, tangu enzi za JK lakini kwa mujibu wa mtoa mada, hivi sasa hiyo 27K ni kwa nchi nzima wakati mpango unaosema wewe, hiyo 27K ilikuwa ni kwa vijijini peke yake!! Kwahiyo kama habari hizi ni za kweli basi Mama Samia anatakiwa kupongezwa kutokana na ukweli kwamba atakuwa amesaidia maskini wengi wa mijini ambao hapo kabla walikuwa wanashindwa gharama za kuunganishiwa umeme.
clip hii hapa, lakini hili laweza kuwa tamko tu la kisiasa maana kwenye hotuba yake iliyoandikwa, (kama ilivyo kwenye bandiko namba 66 hapo juu) haijaeleza hayo
 
Dada nitake radhi,Mimi Wala sio wa kabila ilo la washamba,,
Sometimes mtu unaweza ukawa unachangia mada humu ukiwa una drive, au unabeba boksi sehemu, etc, kwaiyo usitegemee mtu ataandika kwa ufasaha kila muda dada angu
Nani kakwambia kuwa mimi ni dada? Mimi ni beberu ndugu
 
Ni makosa makubwa kupima utendaji wa Rais kwa siku miamoja.
Toka 321,000 mpaka 27000.
Rais ameanza kuwaonesha wapi anaipeleka nchi na huu ndiyo utetezi kwa wanyonge.

Je, hili halimpi credit mama yetu?
Mama mwenyewe hajasema kuwa anataka credit, acha shobo we nguruka!
 
Ni makosa makubwa kupima utendaji wa Rais kwa siku miamoja.
Toka 321,000 mpaka 27000.
Rais ameanza kuwaonesha wapi anaipeleka nchi na huu ndiyo utetezi kwa wanyonge.

Je, hili halimpi credit mama yetu Samia?
mwenye wazo lake na aliyeanzisha utekelezaji kwa vitendo Mh. Jakaya bado yu hai, Mungu aendelee kumpa umri mrefu.
wengine wanaendeleza tu.
 
Nikikumbuka 800,000+ niliyotoa kwa ajili ya nguzo 2 natamani siku zingekuwa zinarudi nyuma.
Maanina Hawa watu
 
Back
Top Bottom