Gharama za kuwapeleka watoto JKT ni mzigo mkubwa kwa wazazi

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,179
73,616
Nimetafakari gharama wanazoziingia wazazi kuwapeleka watoto ex form six JKT. Ni kubwa na mzigo usio na sababu ya msingi kwa wazazi masikini. Si chini ya laki mbili (200,000 Ths) kwa uchache. Hizi ni hela nyingi kwa mzazi wa vipato vya chini huko vijijini anaye-strugle kupata ada ya shule za Kata.

Najiuliza taabu yote hii ya nini kwa wazazi? Kwani JKT ina umuhimu gani WA LAZIMA kwa maisha binafsi ya mtoto na mzazi?

Kama serikali haina hela ya kuwagharamia watoto, mzazi anazipata wapi?

Kama serikali haina hela za kuwaweka watoto makambini waache mpango huo wa kuwapeleka JKT. Wasiumize watoto na wazazi kwa mambo ambayo si lazima sana katika maisha yao.

Bado kuna watoto wanahitaji hiyo JKT, wawaache hao waende maana wana uhitaji na hiyo JKT
 
Mkuu, upo sahihi! Mwaka juzi, mtoto wangu alichaguliwa kwenda Mafinga JKT, nami nipo Mwanza. Kwa upande wangu, ilikuwa nafuu, kwani kuna wengine walichaguliwa kwenda Songea.

Nikatumia nauli, pamoja na baadhi ya vifaa. Kufika huko, ikabidi arudi ili aje achague vyuo, hivyo ikanibifi nimtumie nauli. Baada ya hapo, nikamrudisha huko Mafinga. Baada ya kumaliza, ikabidi nigharamie nauli.

Ile kufika tu Mwanza, akaugua na kupelekea kulazwa hospitali wiki nzima!

Kwa kweli, binafsi sioni faida yoyote ya kupeleka watoto wetu huko. Mwenda zake, alikuwa anataka kuonyesha kuwa kila kilichowashinda/kuacha wenzie, yeye alikiweza!
 
Pole sana. Mimi niko kwenye mtanziko huo. Nimetumia jana laki 2 kununua vifaa, tena kwa kubana kweli kweli. Bado nauli. Naumia kweli maana hela haipo.

Jiwe ni laana, wacha aende zake, laaniwe Jiwe na wapambe wake.
 
Kama mzazi ni masikini kwa nini alizaa watoto. Ukijiona masikini usiache kiumbe duniani ishi mwenyewe ujitafutie mwenyewe chakula basi.
Mkuu nisamehe sana kukuita wewe ni "faller"

Sio kusudio langu lakini umesababisha mwenyewe.

1. Je maskini hastahili kuzaa?
2. Hujui mwenye nacho hufikisika?
3. Ukose pesa na watoto?
Tafakari
Mshana Jr
 
Pole sana. Mimi niko kwenye mtanziko huo. Nimetumia jana laki 2 kununua vifaa, tena kwa kubana kweli kweli. Bado nauli. Naumia kweli maana hela haipo.
Jiwe ni laana, wacha aende zake . laaniwe Jiwe na wapambe wake

JKT ipo kabla ya hilo unaloliita Jiwe, itoshe tu kusema umenajisi hoja yako.

Faida za JKT kwa ex-form SIX, ni pamoja na kukoma kwa migomo ya Vyuo Vikuu nchini TZ.
 
Pole sana. Mimi niko kwenye mtanziko huo. Nimetumia jana laki 2 kununua vifaa, tena kwa kubana kweli kweli. Bado nauli. Naumia kweli maana hela haipo.

Jiwe ni laana, wacha aende zake, laaniwe Jiwe na wapambe wake.
Haya Mambo ya JKT mbona yameanza tokea kipindi cha kikwete? Mwacheni JPM apumzike kwa amani.
 
Nimetafakari gharama wanazoziingia wazazi kuwapeleka watoto ex form six JKT. Ni kubwa na mzigo usio na sababu ya msingi kwa wazazi masikini. Si chini ya laki mbili (200,000 Ths) kwa uchache. Hizi ni hela nyingi kwa mzazi wa vipato vya chini huko vijijini anaye-strugle kupata ada ya shule za Kata.

Najiuliza taabu yote hii ya nini kwa wazazi? Kwani JKT ina umuhimu gani WA LAZIMA kwa maisha binafsi ya mtoto na mzazi?

Kama serikali haina hela ya kuwagharamia watoto, mzazi anazipata wapi?

Kama serikali haina hela za kuwaweka watoto makambini waache mpango huo wa kuwapeleka JKT. Wasiumize watoto na wazazi kwa mambo ambayo si lazima sana katika maisha yao.

Bado kuna watoto wanahitaji hiyo JKT, wawaache hao waende maana wana uhitaji na hiyo JKT
Mkuu mbona uchangizi kwenye ujenzi wa ofisi za kanda za CHADEMA hujalalamikia?
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom