Gharama za kuwapeleka watoto JKT ni mzigo mkubwa kwa wazazi

Nimetafakari gharama wanazoziingia wazazi kuwapeleka watoto ex form six JKT. Ni kubwa na mzigo usio na sababu ya msingi kwa wazazi masikini. Si chini ya laki mbili (200,000 Ths) kwa uchache. Hizi ni hela nyingi kwa mzazi wa vipato vya chini huko vijijini anaye-strugle kupata ada ya shule za Kata.

Najiuliza taabu yote hii ya nini kwa wazazi? Kwani JKT ina umuhimu gani WA LAZIMA kwa maisha binafsi ya mtoto na mzazi?

Kama serikali haina hela ya kuwagharamia watoto, mzazi anazipata wapi?

Kama serikali haina hela za kuwaweka watoto makambini waache mpango huo wa kuwapeleka JKT. Wasiumize watoto na wazazi kwa mambo ambayo si lazima sana katika maisha yao.

Bado kuna watoto wanahitaji hiyo JKT, wawaache hao waende maana wana uhitaji na hiyo JKT
Kipindi cha kikwete tulobahatika kwenda kipind kile ,,nauli na kila gharama ulotumia kumpeleka kijana wako inarudishwa plus maposho na nauli za kurudia tulipewa..
Burudani kbsa..
 
Nilikuwa JKT kwa mujibu wa sheria June 1985 hadi June 1986 wakati tunaenda kuripoti hakukuwa na gharama yeyote kila kitu ni serikali. Alafu ktk mwaka mmoja ukitoka kule umeiva kisawasawa ndio maana wakati wa vita na Idd Amin kuna vijana waliokuwa JKT kwa wakati ule waliungana moja kwa moja na wanajeshi ktk mstari wa mbele. Sasa hii ya sasa hivi ya miezi mitatu siielewi kabisa kama inakidhi dhumuni la kijana kupitia JKT. maana sisi miezi mitatu ilikuwa ni kipindi cha ukuruta tu. Sasa wenzetu miezi 3 ndio wanaita wamepita JKT. Labda mniambiye malengo ya JKT kwa sasa yamebadilishwa sio kama yale ya awali. Niko tayari kukosolewa.
 
Pole sana. Mimi niko kwenye mtanziko huo. Nimetumia jana laki 2 kununua vifaa, tena kwa kubana kweli kweli. Bado nauli. Naumia kweli maana hela haipo.

Jiwe ni laana, wacha aende zake, laaniwe Jiwe na wapambe wake.
Form six mwaka huu wanaenda JKT?
 
Jiwe aliendeleza. Program hii ilirejeshwa enzi za JK ikiitwa oparesheni Kikwete.

Akina Z.Kabwe, H.Mdee na wengine walihudhuria mafunzo hayo pia.

Kwenye lawama hii usimwondoe JK tafadhali.
Jk aliimudu vizuri ikiwemo bajeti ya chakula >sh 8000 compare to JPM 4500 na nguo za mazoezi na nauli
 
Hata Mimi nilitaka kumuuliza.
Nakumbuka MWAKA 2014 Kuna mzazi Kijiji Fulani aliuza shamba ili kijana wake aende jkt.
Sasa sijui MWAKA huu jiwe alikuwa madarakani!!!
come on, tunasema kujigharamia mahitaji ya kwenda JKT, take cre
 
Jiwe aliendeleza. Program hii ilirejeshwa enzi za JK ikiitwa oparesheni Kikwete.

Akina Z.Kabwe, H.Mdee na wengine walihudhuria mafunzo hayo pia.

Kwenye lawama hii usimwondoe JK tafadhali.
Enzo za JK serikali iligharamia kila kitu, hadi nauli ya kwenda hit ilirudishwa. Kwa sasa gharana zote ni jukumu la mzazi
 
Jiwe aliendeleza. Program hii ilirejeshwa enzi za JK ikiitwa oparesheni Kikwete.

Akina Z.Kabwe, H.Mdee na wengine walihudhuria mafunzo hayo pia.

Kwenye lawama hii usimwondoe JK tafadhali.
Wakati wa kikwetr gharama zilikuwa chini ya serikali na vijana wengi waliosoma sayansi walipata ajira jwtz now ni maafisa jeshini.
 
Nimetafakari gharama wanazoziingia wazazi kuwapeleka watoto ex form six JKT. Ni kubwa na mzigo usio na sababu ya msingi kwa wazazi masikini. Si chini ya laki mbili (200,000 Ths) kwa uchache. Hizi ni hela nyingi kwa mzazi wa vipato vya chini huko vijijini anaye-strugle kupata ada ya shule za Kata.

Najiuliza taabu yote hii ya nini kwa wazazi? Kwani JKT ina umuhimu gani WA LAZIMA kwa maisha binafsi ya mtoto na mzazi?

Kama serikali haina hela ya kuwagharamia watoto, mzazi anazipata wapi?

Kama serikali haina hela za kuwaweka watoto makambini waache mpango huo wa kuwapeleka JKT. Wasiumize watoto na wazazi kwa mambo ambayo si lazima sana katika maisha yao.

Bado kuna watoto wanahitaji hiyo JKT, wawaache hao waende maana wana uhitaji na hiyo JKT
Kwani mnalazimishwa? Na asipoenda inakuaje?
 
Back
Top Bottom