Gharama za kuwaondoa machinga zibebwe na viongozi wa mitaa

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,233
12,508
Kasi ya kuwahudumia wananchi kutatua kero zao inapungua kutokana na rasilimali watu, fedha, vifaa na muda kuelekezwa kwenye kitatua shida ambazo zimezalishwa na viongozi tuliowapa madaraka na kuwalipa kwa Kodi zetu.

Wakati mmachinga wa kwanza anaanza kuweka biashara sehemu isiyo sahihi viongozi wetu hawa wa mitaa, kata, tarafa na wilaya wapo na wanaona, Leo hii tunatumia rasilimali ambazo zingetumika kusambasa maji, umeme, afya, usafi na visima kwa wananchi katika kuondoa machinga mitaani. Huu ni uhujumu uchumi sawa na uhujumu uchumi mwingine TU.

Kwanini viongozi hawa wasichukuliwe hatua kwa uzembe huu unaotuingizia hasara kila mwaka?
 
Kirusi hiki kililelewa na ccm,kwa neno wapiga kura wangu

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
Tukishawapeleka mahakamani wakajibu kwanini wanatuingiza kwenye gharama hizi za kijinga kabisa ndio tutafahamu kwanini hawakuchukuwa hatua mapema kuzuia watu kufanya biashara hata sehemu zisizostahili. Tutajua kama
1. Walikura rushwa kutoka kwa machinga.
2. Wenyewe walikuwa pia na biashara hizo huko.
3. CCM ndio iliyowakataza kuwaondoa
4. Serikali ndio iliyowazuia wasiwachukulie hatua
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom