Gharama za kuhifadhi makontena bandarini zapanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama za kuhifadhi makontena bandarini zapanda

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BAK, Jan 1, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,773
  Likes Received: 83,114
  Trophy Points: 280
  Gharama za kuhifadhi makontena bandarini zapanda
  Mwandishi Wetu
  Daily News; Thursday,January 01, 2009 @20:00

  MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeongeza gharama ya kuhifadhi makontena bandarini kwa asilimia 100 kuanzia jana. Vilevile TPA imetangaza kwamba itapiga mnada makontena yaliyokaa kwa muda mrefu bandarini bila ya kuchukuliwa na wahusika.

  Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa Bandari, Peter Milanzi alitoa taarifa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana. Milanzi alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya wateja kutochukua makontena kwa wakati na kusababisha msongamano wa meli nje ya mlango wa bandari.

  "Kuanzia leo Januari mosi (jana) gharama ya kuhifadhi makontena bandarini imeongezeka na kwamba kontena litakalokaa bandarini baada ya siku 21, gharama yake itakuwa dola za Marekani 40 (zaidi ya Sh 51,000) kwa kontena la futi 20 na dola 80 kwa kontena la futi 40,” alisema Milanzi.

  Aidha, alisema makontena yote yaliyokaa kwa muda mrefu bandarini zaidi ya siku 21 kama hayatachukuliwa ifikapo Januari 15 mwaka huu, yatakabidhiwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kupigwa mnada. Milanzi alisema upigaji mnada makontena hayo utafanyika kwa haraka na hatua hiyo itakuwa endelevu.

  Aliwataka wateja kwenda kuyaondoa makontena hayo haraka kabla ya kazi hiyo kuanza. Alisema TPA pamoja na wadau wake wataendelea kufanya kazi kwa saa 24 kila siku ili kuwezesha wateja wao kuchukua mizigo muda wote wanapotaka kufanya hivyo.

  Hata hivyo, aliwataka wateja kutambua kuwa bandari ni mlango wa biashara na siyo sehemu ya kuhifadhia mizigo. Alisisitiza kwamba wateja wanatakiwa kuheshimu taratibu kwa kufuata muda unaofaa kuchukua mizigo yao.

  Kwa mujibu wa ofisa huyo, awali makontena ya wateja wa ndani ya nchi kuanzia siku moja hadi siku saba, yalikuwa yakihifadhiwa bure, na kuanzia siku ya nane hadi 30, kontena la futi 20 lilikuwa likitozwa dola za Marekani 20 kwa siku na la futi 40 lilikuwa likitozwa dola 40 kwa siku.

  Hata hivyo, alisema kuanzia siku ya 30 hadi kontena linapotolewa na mhusika, kontena la futi 20 lilikuwa likitozwa dola za Marekani 27 kila siku na la futi 40 lilikuwa likitozwa dola za Marekani 54 kwa siku.

  Kwa makontena ya nje ya nchi yanayotumia bandari ya Dar es Salaam, awali yalikuwa yanahifadhiwa bure kwa siku 15 tangu siku ya kwanza. Kuanzia siku ya 16, kwa siku 30 baada ya hapo, kontena la futi 20 lilikuwa likitozwa dola za Marekani 20 kwa siku na la futi 40 lilikuwa likitozwa dola 40 kwa siku.

  Hata hivyo, alisema kuanzia hapo baada ya kipindi cha siku 30 kwa makontena ya nje ya futi 20, yalikuwa yakitozwa dola za Marekani 27 kila siku na dola 54 kwa kontena la futi 40 kila siku
   
 2. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2009
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi ndio vitu ambavyo tunaona wazi kabisa kwamba Serikali inasimamia upumbavu, ni wazi kwamba kuna tatizo la ziku nyingi na ushahidi wa tatizo hilo la bandari si wa kutafuta. Mizigo huchelewa kutolewa bandarini kwa sababu ya utaratibu mbovu unaoelemewa na urasimu ulioko kwenye kila kitengo cha bandari yetu. Tunakosa hela kwa sababu hii, ina maana hakuna namna nyingine ya kumrudishia huyo mpumbavu Karamagi hela zake alizotoa wakati wa kampeni au lazima alipwe fadhila kwa kuharibu maslahi ya taifa nzima? Serikali imekosa kabisa jinsi ya kufanya kumweka sawa huyo mjinga hadi ionekane kwamba sisi wote ni wapumbavu? Mbona imewezekana kuwakamata akina Yona na Mramba hata kama ni Politics? Basi politics hiyo hiyo itumike kutudanganya kwa kumpa Karamagi kitengo kingine atakachokula bila kuathiri uchumi wa nchi nzima. Karamagi ni mpumbavu sana kwasababu kwa muda wote TICTS wamepigiwa kelele kuhusu huduma zake angesharekebisha na isingekuwa shida kupandisha bei kama mizigo inatolewa haraka tukaacha kuichukua. Serikali imezidiwa hapa? Kama JK na Pinda wameshtuka tunataka kuona kazi zinafanyika, hotuba zao hazitutii moyo tena hata kama wakiongea na sisi kila wiki, KAZI MBELE, HOTUBA BAADAYE..!
   
 3. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Je mamlaka husika kama TRA nao watafanya kazi 24hr?? Benki nazo wanaopokea malipo nao watafanya kazi 24hrs?? Tatizo sio kuongeza ada ndio kutaondoa msongamano, ni kwa mamlaka husika kuacha kuritimba katika kutoa huduma za utoaji wa makontena. Vile vile vifanye kazi kwa muda mrefu zaidi pasipo na visingizio vya hapa na pale
   
 4. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2009
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu hapa sio kweli kwamba watafanya lolote la tofauti, kimsingi hizi zile politics zao za kipumbavu kutuona sisi ni wajinga wa wakati ule wa zama za mawe. Akili zao zinawaonyesha kwamba kwa kufanya hivyo watu watauana kuhakikisha mizigo inatolewa haraka na hao wafanyabishara wenye mizigo, athari zake hakuna anayeangalia ikiwemo serikali yenyewe. Mambo kama bei za mafuta kushushwa kimsingi nayo naona ni politics, ama basi kama ni kweli nasi kuna ujinga mwingi ambao unafanya bei za mafuta zibaki juu kama haya mauvundo ya ucheleweshaji usio wa sababu hapo bandarini. Inakera sana tunapodanganywa tukiona kwa macho yetu, ni mbaya sana. Hasira zetu hazijapungua kwa kuwakamata akina Yona na Mramba. Kuna mambo mengi bado ya kurekebisha, mojawapo ni hili, WIZI MTUPU..!
   
Loading...