SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,805
- 1,874
Kumezuka mazoea kwa miaka mingi kwamba ndugu na jamaa wanataka kupata control yako kwa kusubiri ukifukwa na janga wakukomoeshe ili ujiunge nao kwenye vikundu wanavyounda hata kama havina tija.
Juzijuzi kaka yangu walitaka kumuangusha kwa kutaka kumwamisha maiti ya mama yake isisafiri kwa hoja kwamba huwa yeye hahudhurii misiba lakini alikuwa amejiandaa na akajigharimikia nauli yeye na mke wake kwa ndege hadi kanda ya ziwa.
Ninafanya research sasa hivi ili kujua msiba unahitaji mambo gani kuufanikisha. Si kwamba sijui, ninajua bali nataka list ya kila kitu ili niwe nimejipanga.
Kwa mfano nataka kujua gharama ya kununua sanduku, sanda, kuosha na kutunza maiti, gharama ya kusafirisha hadi Mwanza, kampuni inayosafirisha maiti hadi Mwanza.
Nikiyajua yote na gharama zote msiba ukitokea leo basi nalia kwa uchungu kwa masaa mawili na baada ya kumaliza kulia naanza mikakati mimi binafsi na kila anayekuja naishia kumwambia ratiba ya msiba kwamba kuaga mwili ni siku fulani na saa ngapi, misa ni saa ngapi, kusafirisha airport ni saa ngapi ndege ianondoka, na kule mkoani misa na mazishi ni saa ngapi na baada ya mazishi kuna vinywaji baridi na moto na baada ya hapo kila mtu kutawanyika.
Ninataka kujua mahitaji na kama jumla ni milioni kama sita basi hizo niwe nimeziweka pembeni ili ukitokea msiba nawakomesha hawa ndugu na jamaa kwa kumaliza kila kitu mwenyewe bila kuhitaji senti tano ya mchango wa ndugu au hata sentensi moja ya ushauri wa hawa ndugu na jamaa.
Na hata kile ki-daftari cha michangi sitaki kabisa kiwepo.
Hayo ndiyo nataka. Mimi nina tabia kama za yule kaka yangu tena zaidi. Mimi naona msiba nauona ni hiari kwenda na si lazima kupata umaarufu kuhudhuria, tena nakwenda kwa yule ninayepatana naye tu.
Na mtu anayekuja kwangu msiba au harusi ni hiari na si lazima.
Hivyo, nataka kuwakomoesha wale waliopania kunikomesha ili wakija kama nilivyosema wakute tayari nilishamaliza kila kitu mwenyewe.
Kama tutashirikikiana ku-list mahitaji ya msiba nitashukuru naamini itawasaidia na wengine.
Mwisho, kama kuna kampuni imejikita na ku-manage mambo yote ya msiba, iitwe vyovyote kama "funeral management, mourning management, kwamba ninawakodi wanakuja kufanya vyote, na kama kulia wanalia mimi niko tayari kuwakodi ikitokea msiba kwangu, mradi tu niwakomoeshe wale walionipania.
Shukrani natanguliza