Gharama za kuegesha magari uwanja wa ndege kilimanjaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama za kuegesha magari uwanja wa ndege kilimanjaro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ulimbo, Oct 31, 2009.

 1. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Nasikitishwa na gharama zinazotozwa kwenye uwanja wa kimataifa Kilimanjaro, kipind cha njuma kidogo wakati huo uwanja ulipokuwa umepewa mwekezaji, gharama za kuegesha magari zilikuwa Sh 200 -500 kwa magari yasiyo ya kibiashara, na sh 1000 kwa magari ya biashara. Gharama hizi zilitozwa unapoegesha gari kwa muda wote/kwa siku, kama unashusha mtu/mgeni na hauta egesha gari, ulikuwa ulipi chochote.
  Kwa sasa huu uwanjwa umerudishwa serikalini na unaendehwa na serikali. Cha kusikitisha ni gharama za kuegesha magari zinazotozwa kwa sasa bila kujali unaegesha gari au unashusha mgeni na kuondoka. Ukiingia tu kwenye eneo la kiwanja, unatakiwa kulipa sh.1000 uwe umeegesha au umeshusha mgeni, na kama utaegesha, basi kwa kila saa moja, utalipa sh.1000.
  Sijui gharama hizi zimepanda kwa sababu gani kwani hakuna la zaidi lililofanyika labda ukarabati n.k.

  Mwenye taarifa/sababu zaidi naomba anipe.
   
 2. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hii ndo Tanzania yetu tunayoipenda
   
 3. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Ili kukwepa kulipa ushuru kwa masaa mengi,madreva ambao wanakwenda kupokea wageni wana egesha magari yao nje ya kiwanja hadi ndege itue, na hapo ndipo wanaingiza magari ndani ya eneo la kuegesha.
  Kwa wale ambao hajui mabadiliko haya, wana kumbana na kizazaa kwenye geti la kutokea wanapodaiwa kulipia zaidi, jambo ambalo linawafanya wageni (Watalii) kubaki midomo wazi.
   
 4. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Ili kukwepa kulipa ushuru kwa masaa mengi,madreva ambao wanakwenda kupokea wageni wana egesha magari yao nje ya kiwanja hadi ndege itue, na hapo ndipo wanaingiza magari ndani ya eneo la kuegesha.
  Kwa wale ambao hajui mabadiliko haya, wana kumbana na kizazaa kwenye geti la kutokea wanapodaiwa kulipia zaidi, jambo ambalo linawafanya wageni (Watalii) kubaki midomo wazi.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hakuna kitu kama hicho, nani kasema uwanja huu umerudishwa serikalini...!

  Mimi ni mdau wa karibu kabisa wa uwanja huu, bado uko chini ya KADCO ambao ni PRIVATE kwa 100%, na hauendeshwi na TANZANIA AIRPORTS AUTHORITY (TAA).

  Ninachojua ni kwamba kama unaona gharama zimepanda ni kwasababu kuna mwekezaji aliyechukua tenda ya PARKING, yaani kama unavyoona hizi PARKING SYSTEMS ZA HUKO DAR, na ni lazima aende kibiashara, na apate hela ya ziada ya kuwahonga wanene ili aendelee kuimega keki yake taratiiibu!

  Habari ndo hiyo!

  Nawasilisha!
   
 6. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Nashukuru kwa kwa kunijulisha hilo.
   
Loading...