Gharama za Kuanzisha Website ya Biashara 2020 (Mwongozo Rahisi)

Mmh kaka mimi nisikudanganye, hicho kiasi kwa application hakitoshi hata kidogo, kwa sababu kima cha chini kabisa ili kutengeneza application nzuri kwa ufahamu wangu sio chini ya 1M, kama kweli unahitaji kitu cha kudumu na kuna wababaishaji wengi wataongea kuwa inawezekana kutengeneza app kwa 300k au hata 50k ... Lakini kwa experience yangu utakuwa unapoteza fedha na hutoweza kutatua tatizo unalohitaji hiyo application itatue.

Ushauri wangu hiyo fedha ni kheri, uiongeze kidogo tu. Utengeneze Website kwa kutumia template na hosting ya bei rahisi. Website itaweza kukusaidia kukusanya hizo oda pia kama unavyohitaji tena inaweza kuwa bora kuliko app. Kwa sababu hakuna habari ya kutumia data kudownload. Na tena ukitengeneza brand yako vizuri kupitia social media watu watakuwa wanaoda bila kuanza kwenda kudownload app ila wataingia kwenye website chap na kumaliza shughuli zao.

Mi nitakusaidia kukupa ushauri tu bure, ila kwenye suala la kuifanya hiyo kazi bajeti yako mkuu, sidhani kama itafaa muda wangu nisamehe kwa hilo. Nashkuru pia kwa kunitakia mema kuhusu scholarship, ila kwa upande wangu naamini katika kujiendeleza mwenyewe kupitia experience ya kufanya kazi halisi.
Poa poa kwa ushauri nitakutafuta mkuu.
 
Kuna mtu anaweza nifanyia training ya week mbili ya web development?
 
Mkuu hongera sana uko deep umetupa elimu ya bure.
Nilikuwa natafuta hii elimu siku nyingi sana ila sikupata mtu wa kunipa hizi lectures,ubarikiwe.
Swali:Je nikihitaji unifanyie website ya template utanilipisha kiasi gani cha pesa?

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom