Chifu Ihunyo
Member
- Jul 3, 2006
- 63
- 10
Jamani tutafika au wachambuzi mnasemaje ?
Gharama za Baraza la Kikwete
Fungu la mishahara yao lazidi la Mkapa
Magari ya mawaziri yagharimu bil. 6.4
Na Tamali Vullu, Dodoma
BARAZA la Mawaziri la sasa linalipwa mishahara ya sh 1,012,764,000 kwa mwaka ikilinganishwa na baraza lililopita ambalo lilikuwa likilipwa sh 777,492,000.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, aliliambia Bunge jana kuwa katika baraza la sasa lenye mawaziri 30 wanalipwa mishahara ya sh 533,628,000; na naibu mawaziri 31 wanalipwa sh 479,136,000.
Ghasia alisema katika baraza lililopita lilikuwa likilipwa mishahara ya sh 499,284,000 kwa mawaziri; na naibu mawaziri 18 walilipwa sh 278,208,000 kwa mwaka.
Alisema gharama za ununuzi wa magari ya mawaziri 30 wa awamu ya nne ni sh bilioni 3.15 na naibu mawaziri 31 ni sh bilioni 3.255.
Baraza lililopita lilikuwa na mawaziri 28, gharama ya magari yao ilikuwa sh bilioni 2.94 na kwa naibu mawaziri ununuzi wa magari yao uligharimu sh bilioni 1.89.
Gharama za mishahara katika Baraza la sasa ukilinganisha na Baraza lililopita zimepanda kwa asilimia 32.6, alisema.
Waziri huyo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Grace Kiwelu (CHADEMA), aliyetaka kujua kiasi cha fedha kinachotumika katika Baraza la Mawaziri kama mishahara; na gharama za ununuzi wa magari pamoja na kiasi kilichoongezeka kikilinganishwa na baraza lililopita.
Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alihoji kama Ofisi ya Waziri Mkuu inaweza kufuta kauli yake kuwa gharama ni ndogo na haina madhara yoyote.
Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Juma Akukweti, alisema bado anasimamia kauli yake na kwamba kwa mazingira ya kazi ya sasa, inastahili kuwa hivyo.