Gharama za bando kubaki vilele wakati vifurushi vinapunguzwa kila kukicha tunaoumia sisi

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Hivi karibuni tumeona bei za bando zikiwa zimebaki vile vile lakini vifurushi vinanywewa na kubaki na kiasi cha data ambacho kiuhalisia hakiendani kabisa na gharama tunayolipia.

Mfano kwa watumiaji wa mtandao wa Halotel, ulikuwa unanunua kifurushi cha intaneti cha mwezi mmoja kwa kiasi shilingi elfu 10,000/= za kitanzania na kupata GB 10. Taratibu wakaanza kunywa data zetu na mpaka sasa hivi nashusha uzi huu kwa gharama hii hii ya shilling elfu 10,000/= unapata GB 5.7, yaani wamekunywa karibia nusu nzima ya bando tulilokuwa tunapata awali.

Tunaelewa kuna vita na gharama za maisha zimepanda lakini hamuoni kwa kasi hii tunakaribia kuacha kutumia smartphones turudi kwenye enzi za kutumiana barua?! Mbaya zaidi sio kwamba hatupazi sauti au tunayosema hayasikiki, vinafika lakini tunapuuzwa.

Wameshazoea tunalalamika tu, hakuna anaeingilia kati na wao wanaendelea na mambo yao utafikiri hakuna wa kishughulikia kero hii ambayo wengi inatugharimu.

Hata kama ni kupandisha bei basi ziendane na uhalisia sio kujifanyia mambo tu bila utaratibu wowote na kuweka mzigo mkubwa kwa watumiaji wa huduma hizi ambao kiukweli wameelewa na vitu vingi.
 
Kila sehemu ni wizi tu
Na mie nikiupatia napiga,
Na wewe ukipata piga tu
Hapo ndio tutaelewana na hii mijizi ya mitandao
 
Kilio chako kimetufikia. Sisi wanaccm kwa buku tunapata 3GB. Nyie wapiga zumari endeleeni kumkwamisha mama nyuki
IMG-20220803-WA0034.jpg
 
Ukiwa manager halafu bahati mbaya wakakusimamisha halafu bahati nzuri wakakurudisha, kudadeki hapo lazima uzipige Kweli kweli, ukizubaa ujinga wako
So tegemeeni maumivu zaidi
 
Back
Top Bottom