Gharama ya wanafunzi kusimamishwa masomo analipa nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama ya wanafunzi kusimamishwa masomo analipa nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, May 11, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Leo ni takribani wiki mbili sasa tangu wanafunzi zaidi ya 1,000 wa kitivo cha taaluma ya habari na mawasiliano cha UDOM wafukuzwe chuoni kutokana na sababu za kitoto...

  Kitivo hiki ni miongoni mwa vitivo ambavyo wanafunzi wake wanasomeshwa bure (hawakopeshwi) na ni moja wapo ya matarajio tuliyonayo kama taifa kutuwezesha kushiriki kwenye kijiji cha ulimwengu katika kipindi hiki cha teknolojia ya mawasiliano na habari, ajabu ni kwamba kwa uzembe wa watu wachache ambao wanaamini kuwa maamuzi yao kamwe hayatakiwi kuhojiwa na kupingwa wamesababisha wataalamu wetu hawa watarajiwa wafukuzwe na serikali iendelee kuingia gharama kubwa ya kulipa watumishi ambao hawafanyi kazi. Taasisi kama UDOM naamini inaajiri watu wengi wanaolipwa pesa nyingi, achilia mbali gharama zingine za uendeshaji kama umeme, maji,muda unaopotea kwa wanafunzi hawa, n.k.

  Ifike wakati sasa tukatae kuingizwa kwenye gharama zisizostahili kama hizi na watu wachache wanaodhani ni miungu watu, ifike wakati wazazi tupinge kwa nguvu zetu zote watoto wetu kunyanyaswa na kunyimwa haki zao za msingi kama watanzania. Tusiwaruhusu watendaji wasiowajibika kutuingiza kwenye hasara kama ilivyotokea kwenye mikataba feki na ya kifisadi ambayo wametuingiza na bado wanakula kuku kwa mrija.... INATOSHA!
   
 2. T

  TAITUZA Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siasa zimeingia sana vyuo vikuu,nawashauri wanafunzi na malecturer wakae pembeni mwa siasa, wafanye kazi ushabiki wa uccm na uchadema hautawafikisha popote,daini ya msingi,na mnapotimiziwa someni huo ndo wajibu wenu, badala ya kila cku kuwa barabarani mnaandamana, hv mko hapo chuoni kuandamana kila sikuuuuu au kusoma? siasa zipo tuuu, malizeni mje mtaaani mfanye siasa. kozi ya miaka 3 unajikuta unasoma miaka 6 kisa kila mara unafukuzwa na wakati huo huo wewe ni mtoto wa mkulima, je hii ni kwa faida ya nani?wao wenye pesa zao watoto wao wako europe na america wanasoma tuliiiii, nyie kila cku migomo,ANGALIENI MUSTAKABALI WENU KWANZA NCHI BAADAE!
   
 3. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo sio migomo na maandamano bali ni chanzo chake! Watawala kwenye vyuo vikuu ndio wana matatizo kwasababu wanaendesha vyuo kwa ushabiki wa kisiasa (CCM). Wana chuo wana haki ya kushiriki siasa za nchi na kujiunga na chama chochote wanachotaka. Kwamba wana chuo wasishiriki siasa ni mawazo mgando, vijana wengi walioko kwenye siasa kwa sasa walishiriki kikamilifu kwenye siasa za chuo mfano Zitto Kabwe, John Mrema, Mtatiro etc
   
Loading...