Gharama ya ujenzi wa vyumba vitatu, sebule, jiko na choo cha ndani

Brother achana nao bhana sisi tunajua na tumefanya kwa namna yetu sisi, acha waendelee kujifanya wajuaji ila ukweli utabaki kwamba ukiwa na 15M inafikisha nyumba ya vyumba vitatu na master mbali sana kiasi unaweza kuhamia kama itakua bado basi ni finishing ndogo ndogo sana.
Hapo jirani yangu kuna aliyejenga hakuweka mkanda wa nondo kwenye msing wala kati hakuweka seng'enge na nyumba imesimama imara tu maisha yanakaribia kuanza anafanya finishing ahamie.
Kwa hiyo 15m unamaliza nyumba?

Hatukatishani tamaa, hakuna mwenye hela hapa wote makapuku tu, ila tunaongea uhalisia.

Unasema 15m nyumba unahamia, je hiyo nyumba itakuwa imeisha au unahamia kwa vile uchumi hauruhusu kuendelea kupanga? Na je, ungekuwa na cash ya kutosha ungehamia nyumba ya three-four bedroom iliyongarimu 15m?

Tuwe wakweli jamani, tunahamia nyumba zetu sio kwa vile zimeisha, ni kwa sababu uchumi hauruhusu na ndipo uwezo wetu unapoishia.
 
Wakuu, Natumai mko vyema na mmejiandaa kikamilifu kuhesabiwa.

Unaambiwa upange maisha yako kwanza, uhakikishe unakuwa kwenye mstari wa mafanikio kisha uwaze kuhusu maisha ya ndoa. Uki-vise verse tambua kabisa utakuja kupigwa na kitu kizito kichwani mpaka ushangae. Nimeishuhudia mahali

Twende kwenye hoja:
Nahitaji kujenga nyumba ya vyumba vitatu (3 bedrooms), sebule ya ukubwa wa kawaida (yaani lisiwe casino), dining room iliyounganika na kitchen room kiaina, bila kusahau choo na bafu la ndani. Nahitaji kuweka vigae pamoja na singboard. Kupiga leap na kupakaa rangi nje na ndani. Madirisha ya aluminium yatakuwa sita nyumba nzima jumlisha na tu aluminium tudogo tuwili twa choo na bafu! Nahitaji kufanya wiring na kuweka umeme kabisa.

Niko mbele zenu ili kujua gharama zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha jukumu hili. Gharama za jumla kwa wenye uzoefu, ili kusudi nikienda kuchukua huu mkopo benki nimalize suala hili moja kwa moja, yasiwepo masuala ya aliishia kwenye renta! Hata kama una uzoefu may be na mchanganuo wa matofali, au sementi, au mabati (msaudhi) yatakayotosheleza pamoja na mbao zake naomba msaada wako kuhusu gharama. Nafahamu wengi wenu humu mmejenga!

Mawazo tafadhari!

Huwezi jenga ukihangaika na ushauri wa humu kuhusu gharama watakutisha sana.

We anza ujenzi na ulichonacho, endelea kadri unavyopata pesa.

Utaona njia tu ukishaanza
 
Inategemea na wapi unaishi,mimi nipo rukwa sumbawanga manispaa,nataka kujenga km wewe ila kwa tafiti zangu kujenga boma km lako si Zaidi ya 5M kuaniza msingi lenta mpk tungilizi ya juu, paa inategemea unataka lipande sana juu, kati au chini napo km ni chini nayo unaweza kuwa chini ya 5 M kwa sababu,bati,mbao na misumari havitatumika vingi, kwa sumbawanga madirisha na milango ni kati ya 200000-300000 ukiwa fully
Kwa haraka haraka 8-15m kwa sumbawanga unapata NYUMBA
 
Ujenzi wa nyumba ( gharama zako tofauti na za wengine) ni kama kuingia kwenye ndoa (changamoto zako tofauti na za wengine).

Kwann tofauti? Material tofauti, Umbali wa site tofauti, mafundi tofauti, ardhi (hivyo muundo wa msingi) tofauti, ukubwa tofauti, shimo la choo tofauti, n.k

Nyumba Anza tu kujenga mkuu. Hela yako itakapoishia ndiyo hapo hapo. Utakuja kumalizia utakapokopa tena baada ya kumaliza deni la mkopo wako wa Sasa.
Nimecheka hapo kwenye mkopo
We umejuaje kama kakopa?
Pengine ameozesha binti yake akapokea mahali milioni saba
 
Kakope around 40 M
Si unataka kujenga nyumba nzuri mkeo umnyandue kwa kujiachia na mkweo akija alale na kujisaidia kwa raha zake?
Kama ndio andaa hiyo pesa hapo juu,achana na hao wanao kuambia 15 to 25M hiyo nyumba au double self?
15-25m ni pesa nyingi sana kujenga nyumba sema inategemea na eneo unaloishi.. pia gharama ya nyumba ni finishing tu ila boma+ paa ndi kawaida na finishing ina maana kubwa sana na wewe unataka iweje.! Watu kibao wanajenga boma wanaezeka nyumba mlango wa kutoka na kuingia choo+ floor na kusajafia ukuta ndani, frame za madirisha na pazia inatosha sana, vingine utamalizia ukiwa NDANI
 
Hivi mnaona 100m kuwa nyingi sana kwa ujenzi wa leo? Are you guys serious? Kuna nyumba na NYUMBA mkuu, zipo nyumba kwa sababu ya accessories zilizopo 100m ni kawaida tu.

Watu wanajenga nyumba nzuri mno, mno kiasi kwamba unajiuliza hizi pesa wao wanatoa wapi.

Kama nyumba yenye 150sqm mtu anatamia almost 15m-20m kupaua na kuezeka tu, unaonaje ajabu nyumba kugharimu 100m hadi finishing?mwingine hiyo 15m-20m amejenga msingi, boma na bati kashaweka.

Wewe useme kibongobongo na nyumba zetu kwa ujenzi wa kuungaunga ni kweli 100m ni nyingi, lakini kwa mtu mwenye resources zake anashusha mzigo wa 100m au zaidi kwa three-four bedroom house.
Fahamu kuwa wanaouliza kuhusu ujenzi humu ni watu wa kipato cha chini, yaani, watu wa kawaida. Hivyo ujenzi wa nyumba za watu wa hawa huwa haufuati taratibu zote za ujenzi kitaalamu kama unavyofikiria badala yake hutafuta njia au namna itakayofanya ujenzi huo kuwa wa gharama rahishi kulingana na kipato cha mtu huyo.

Kwa sababu nilizotaja hapo juu, nyumba nyingi zimejengwa chini ya viwango vinavyotakiwa hivyo kuathiri uimara wa nyumba kama vile kutokuweka msingi imara, uwiano wa saruji, mchanga n.k kutokuwa wa kiwango kinachopendekezwa. Madhara ya ujenzi wa namna hii huweza kuonekana papo hapo au hata baada ya miaka kadhaa. Na madhara hayo ni kuta kuwa na nyufa zilizo za kina, pande za nyumba kutitia na hata nyumba yote kuanguka.

Hivyo ni bora kujenga chumba na sebule kwa viwango stahiki kuliko kujenga nyumba ya vyumba vitatu katika viwango visivyopendekezwa.
 
Shida siyo kutumia 100m shida ni una ujanja gani kwenye building materials

Nadhan ndo sehemu watu wanapigwa zaidi

Product ya 90,000 ukishangaa unauziwa 150,000 utaachaje kufika 100M

Ukijenga nenda na fundi dukani upate details zote then ghairisha safari nenda duka jingine ukiwa mwenyewe bila fundi kujua
Unaweza kulia
 
Kwa hiyo 15m unamaliza nyumba?

Hatukatishani tamaa, hakuna mwenye hela hapa wote makapuku tu, ila tunaongea uhalisia.

Unasema 15m nyumba unahamia, je hiyo nyumba itakuwa imeisha au unahamia kwa vile uchumi hauruhusu kuendelea kupanga? Na je, ungekuwa na cash ya kutosha ungehamia nyumba ya three-four bedroom iliyongarimu 15m?

Tuwe wakweli jamani, tunahamia nyumba zetu sio kwa vile zimeisha, ni kwa sababu uchumi hauruhusu na ndipo uwezo wetu unapoishia.

Tatizo unataka kulinganisha ujenzi wa mkoani na Dar

Nikiwa singida 15M namaliza nyumba nahamia

Machimbo ya finishing ninayo kiganjani ni nini kitashindikana..

Nyie endeleen kupigwa mkisema nyumba za milion 100
 
Inategemea na wapi unaishi,mimi nipo rukwa sumbawanga manispaa,nataka kujenga km wewe ila kwa tafiti zangu kujenga boma km lako si Zaidi ya 5M kuaniza msingi lenta mpk tungilizi ya juu, paa inategemea unataka lipande sana juu, kati au chini napo km ni chini nayo unaweza kuwa chini ya 5 M kwa sababu,bati,mbao na misumari havitatumika vingi, kwa sumbawanga madirisha na milango ni kati ya 200000-300000 ukiwa fully
Kwa haraka haraka 8-15m kwa sumbawanga unapata NYUMBA

Watakukatalia mkuu
 
Fahamu kuwa wanaouliza kuhusu ujenzi humu ni watu wa kipato cha chini, yaani, watu wa kawaida. Hivyo ujenzi wa nyumba za watu wa hawa huwa haufuati taratibu zote za ujenzi kitaalamu kama unavyofikiria badala yake hutafuta njia au namna itakayofanya ujenzi huo kuwa wa gharama rahishi kulingana na kipato cha mtu huyo.

Kwa sababu nilizotaja hapo juu, nyumba nyingi zimejengwa chini ya viwango vinavyotakiwa hivyo kuathiri uimara wa nyumba kama vile kutokuweka msingi imara, uwiano wa saruji, mchanga n.k kutokuwa wa kiwango kinachopendekezwa. Madhara ya ujenzi wa namna hii huweza kuonekana papo hapo au hata baada ya miaka kadhaa. Na madhara hayo ni kuta kuwa na nyufa zilizo za kina, pande za nyumba kutitia na hata nyumba yote kuanguka.

Hivyo ni bora kujenga chumba na sebule kwa viwango stahiki kuliko kujenga nyumba ya vyumba vitatu katika viwango visivyopendekezwa.
Mkuu, hoja yangu imejikita hapa, umeandika kitu kizuri. Mimi najua mtu akisema "nimetumia 15m na nyumba imeisha" ni kuwa kaweka tofali, kaweka bati, kaweka grill na kuona kwa hali yangu ngoja tu niingie kupunguza mzigo wa kodi. Na hivyo vyote vinafanyika chini ya kiwango.

Lakini kusema 3-4 bedroom unamaliza kwa 15m sijui ni TZS au ni SA rand. Tuseme uchumi wetu hauruhusu kujenga nyumba imara zenye viwango.
 
Tatizo unataka kulinganisha ujenzi wa mkoani na Dar

Nikiwa singida 15M namaliza nyumba nahamia

Machimbo ya finishing ninayo kiganjani ni nini kitashindikana..

Nyie endeleen kupigwa mkisema nyumba za milion 100
Ukisema 15m unamaliza nyumba nipe mchanganuo, nyumba ina ukubwa gani kwanza.

Just imagine unajenga nyumba inaingia tofali 5,000 za block. Hizo tofali tu ni zaidi ya 5m, bado mchanga, kokoto, cement, nondo, mengineyo na ufundi.

Mkuu, hizi nyumba zetu tunajua wenyewe jinsi zilivyo. Banda langu siwezi kuliweka kwenye viwango vya nyumba bora coz halina viwango stahiki, sema nitabishana tu kuwa nyumba yangu nimejenga kwa 40m japo haina viwango.
 
Shida siyo kutumia 100m shida ni una ujanja gani kwenye building materials

Nadhan ndo sehemu watu wanapigwa zaidi

Product ya 90,000 ukishangaa unauziwa 150,000 utaachaje kufika 100M

Ukijenga nenda na fundi dukani upate details zote then ghairisha safari nenda duka jingine ukiwa mwenyewe bila fundi kujua
Unaweza kulia
Hornet nipe mchanganuo wa nyumba ya kawaida ya vyumba vitatu kuanzia msingi hadi bati.

Then, nipe mchanganuo wako(hapa unatoa mchanganuo wako coz finishing inategemea mtu anatakaje) wa finishing tuone nyumba yenye 160sq.m utaijenga kwa shilingi ngapi hadi finishing.

Hii kazi pia nampa mkuu wangu DeepPond. Nataka kuona tofauti zetu ziko wapi hadi mtu aseme 15m "nyumba inaisha na anahamia"! Baada ya hapo tunaweza kufanya argument nyingine.
 
Ukisema 15m unamaliza nyumba nipe mchanganuo, nyumba ina ukubwa gani kwanza.

Just imagine unajenga nyumba inaingia tofali 5,000 za block. Hizo tofali tu ni zaidi ya 5m, bado mchanga, kokoto, cement, nondo, mengineyo na ufundi.

Mkuu, hizi nyumba zetu tunajua wenyewe jinsi zilivyo. Banda langu siwezi kuliweka kwenye viwango vya nyumba bora coz halina viwango stahiki, sema nitabishana tu kuwa nyumba yangu nimejenga kwa 40m japo haina viwango.
Zipo Ramani nyumba zake hazina kona kabisa, corridor moja, master bedroom, single room 2, dinning room, kitchen room, sitting room na public toilet..!
 
mimi nimejenga sana.kinachopandisha garama za nyumba ni kushindwa kupatana vizuri bei na.mafundi pamoja na kuibiwa vifaa.mafundi wengi ni wezi wa vifaa na garama za ujenzi siyo halisi.ukilijua vizuri soko la vifaa na kupatana vizuri bei hushuka kwa 50%.tulio na uzoefu wa estate nyumba ya kawaida.masta
3 rooms.jiko .choo .bafu.toilets.fens.paving.bati la msauzi haizidi 50.ukinipa 100m najenga gorofa.sizungumzii theory nimepractice 10 times
 
Back
Top Bottom