Rais wa Tanzania kufanya ziara ndani ya nchi ni ghali kuliko nje

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,542
2,171

Gharama ya Rais wa Tanzania na deligate yake kusafiri ndani ya nchi ni kubwa kuliko ile yakwenda nje japo Safari zote mbili zinaumuhimu mkubwa kwa Taifa letu,​


Kipindi flani niliwahi kuhesabu magari ya msafara wa Rais wa JMT sina kumbukumbu sahihi ila yalizidi magari 40 mengi yakiwa ni aina ya " Land cruisers "

Nimejaribu sio kwa usahihi sana kufanya hesabu ya gharama za mafuta kwenye ziara ya Rais ndani ya nchi bila kuhesabu malazi na Chakula kama Rais atatokea Dar es salaam kwenda Mwanza na kurudi Dar es salaam bila kukatisha popote kwa msafara mdogo wa magari 40 tu,

Iko hivi gari aina ya Land cruiser V8 lililotumika kama haya yetu linatumia Lita 45.5 kwa umbali wa km 100 (45.5L/100Km )

Umbali kutoka Dar es salaam mpaka Mwanza kwa gari ni Jumla ya kilometa 1,146 hii ni hadi Mwanza mjini,

Chukua hizi 1,146km zigawanye kwa 100 utapata mizunguko 11.46 ya kilometa mia moja kila mmoja kutoka Dar-Mwanza.


Zidisha 11.46 kwa lita 45.5 ili kupata Jumla ya mafuta ya gari aina ya Land cruiser V8 kutoka Dar es salaam hadi Mwanza mjini ambapo utapata Jumla ya lita 522 za mafuta hii ni kwasafari moja ya gari moja kwenda Mwanza tu.

Sasa zidisha lita 522 kwa magari 40 kama makadirio ya chini ya msafara wa Rais utapata jumla ya lita 20,880 kisha zidisha mara mbili ilikujua gharama ya mafuta ya kwenda na kurudi Dar es Salaam,

Utapata Jumla ya lita 41,760 ikiwa ndio idadi ya lita za mafuta kwa magari yote 40 aina ya Land cruiser V8 kwa Safari ya kutoka Dar es salaam mpaka Mwanza na kurudi Dar es salaam.

Zidisha lita 41,760 kwa bei ya mafuta ya wastani wa TZS 2,500 kwa lita utapata Jumla ya TZS 104,400,000(milioni mia moja na nne na laki nne) Hii ndio gharama ya mafuta tu kwa Rais kusafiri kwa msafara wa magari 40 ndani ya Tanzania.

|[CHUKUA MFANO WA SAFARI YA RAIS SAMIA YA KWENDA MISRI]|


Gharama ya ndege za abiria anazopanda Rais Samia kama Ethiopia Airlines kutoka Dar -Cairo Misri kwa economy class ni TZS 850,000 per head na hii ni kwenda na kurudi Tanzania, ( two ways )

Kwamfano,kama Rais Samia atakwenda na deligate|msafara wa watu 40 basi atalipa nauli kwa wote Jumla ya TZS 34,007,000 kwa kwenda Misri na kurudi Tanzania,

Sasa gharama ya mafuta tu ya msafara wa Rais kwenda na kurudiMwanza,Geita,Kigoma,Kagera,Mara,Simiyu na maeneo ya jirani inakadiriwa kufikia TZS 100m bila kuhesabu Chakula na Malazi kwa deligates,


Wakati huohuo gharama ya kwenda Misri na kurudi na deligates ya watu 40 ni TZS 30m tu bila kuhesabu chakula na malazi,

Sasa kwamsiofahamu gharama za Rais wa Tanzania kufanya ziara ndani ya nchi ni kubwa kuliko gharama za Rais huyohuyo kufanya ziara nje ya nchi hasa kama Rais huyo atatumia ndege ya abiri kama anavyofanya Rais Samia Suluhu.

Namba hazijawahi kunidanganya mwenye akili ataelewa kuwa kumbe Rais anaweza asisafiri nje still deni la nchi likachipua kama uyoga.




IMG-20220214-WA0051.jpg


IMG-20220214-WA0049.jpg


IMG-20220214-WA0048.jpg


IMG-20220214-WA0050.jpg
 
Safari za ndani hutumia AirTanzania, hizo v8 hutumika ndani ya mikoa husika, lakini sio kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine labda kama hiyo mikoa iwe karibu, mfano Dsm - Pwani au Kilimanjaro - Arusha, lakini sio Mwanza - Dar thats too far.
 
Duuh kuna watu mnafikiri hata raha,

Aise kumbe Safari za ndani ya nchi ni gharama hivi,

Hongera Sana Rais Samia kachape kazi
 
Safari za ndani hutumia AirTanzania, hizo v8 hutumika ndani ya mikoa husika, lakini sio kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine labda kama hiyo mikoa iwe karibu, mfano Dsm - Pwani au Kilimanjaro - Arusha, lakini sio Mwanza - Dar thats too far.
Wewe unaishi nchi gani?

Magari yanafika hadi 100
 
Kwa misafara ya ndani umesahau na hesabu za mafuta ya helicopter 2
 
RAIS azunguke kadri anavyoweza... Wananchi lazima wapate unafuu kutokana na uwepo wa binadamu wengine!!
Zunguka Mama!

NB: Lakini Cairo Misri kaenda na ATCL
Afadhali marubani wetu angalau wapate perdm
 
Back
Top Bottom