Gharama ya "Processing fee" inayotozwa na ma-bank hapa nchini kwa waomba mikopo ni Wizi uliohalalishwa kisheria

Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,720
3,237
Huu ni wizi, hakuna jina zuri la kuita hii tozo

Hebu fikiria unaenda kuomba mkopo ambao utaulipa na riba juu tena kubwa tu, pale bank wameajiri ma-afisa mikopo ambao kazi yao ni kutoa elimu na mikopo kwa wahitaji.

Ukifika, Unapewa maelezo na form then unaambiwa ufatilie mwenyewe kila document wanayotaka, kama ni muajiriwa utafitilia document zote za kiofisi mwenyewe ikiwemo saini za waajiri wako na stationaries kama zitakuwepo kwenye uhitaji, unamaliza unawarudishia form yao ikiwa imekamilika wanakuambia subiri siku kadhaa tutakujibu.

Then unaambiwa kuna gharama za "Processing fee" kwa bank kama NMB zinaenda mpaka 900k (Laki 9), kwa kazi gani waliyofanya hapo kama sio wizi?

Bank mnatoa mikopo kama biashara then kutupa hiyo mikopo mnataka tuilipie kutupa kama hisani, wakati tunairudisha kwa riba na mnatengeneza faida?

Ni bora hata mngekuwa mnazunguka wenyewe na hiyo miform maofisini, yaani mfatilie wenyewe kila kitu ingekuwa na tija, mnakata pesa ambayo hata jasho hamuitolei?

Nimeamua kubaki na form yangu ya mkopo katika hatua ya mwisho...

Nyie CRDB hii form yenu siirudishi, nimeshaghairi kuchukua huo mkopo, inabidi itumike kuwashia moto nyumbani, haiwezekani mnile pesa kizembe hivi tena kwa zama hizi za jiwe.


Acheni wizi..!!

NMB Tanzania
 
ITAKUWA UMEKOSA DHAMANA au mdhamini kagoma kukudhamini;
Mwenye shida na mkopo haogopi utitiri wa copy!
Hata umwambie atoe photocopy ya kwapa lake atatoa!
SHIDA ISIKIE TU KWA MWENZAKO
By the way una hoja ya msingi lakini haizuii kuchukua mkopo!
 
matter of business,, but ni kilio kikubwa sana....sasa si bora nyie wenye waajiri..... sie wajasiriamtaji....ni shida na rushwa wanataka.......yaani mkopo unachukua kama CHENJI!!!!!!...tutafika tu...japo kwa damu ya jasho....
Yan washenzi sana tena wanadai rushwa kama haki yao vile..
 
ITAKUWA UMEKOSA DHAMANA au mdhamini kagoma kukudhamini;
Mwenye shida na mkopo haogopi utitiri wa copy!
Hata umwambie atoe photocopy ya kwapa lake atatoa!
SHIDA ISIKIE TU KWA MWENZAKO
By the way una hoja ya msingi lakini haizuii kuchukua mkopo!
dhamana ya mtumishi wa umma ni nini mkuu?

Mimi nimeamua kuachana nao nimeona kuna plan B ambayo itaniwezesha kufanya jambo langu
 
ITAKUWA UMEKOSA DHAMANA au mdhamini kagoma kukudhamini;
Mwenye shida na mkopo haogopi utitiri wa copy!
Hata umwambie atoe photocopy ya kwapa lake atatoa!
SHIDA ISIKIE TU KWA MWENZAKO
By the way una hoja ya msingi lakini haizuii kuchukua mkopo!
Akili mshindo
 
Hata sielewi majibu yake hata sikurudisha form mpaka leo ipo tu ndani toka mwaka jana

Sent using Jamii Forums mobile app
Boss, hata mimi siwarudishii nimepiga mahesabu naona zaidi ya 1.3m kama nikichukua mkopo wanazikata kwenye huo mkopo juu kwa juu kama procesing fee na bima ya mkopo.

Halafu bado waanze kunikata kwenye mshahara na riba juu...upuuzi acha niwashie moto
 
Hua nasema hapa nchini hakuna watetezi ,so wanasheria,wabunge,wanasiasa na wasomi wote ovyo tu.hili ni tatizo sijui kwa Nini hawalioni?
Mabenki yananyonya Sana wakopaji,kuandaa mkopo ni kazi yao.kwa Nini watoze hela? Processing fee,sasa wao kazi yao Nini?
Sijui wizi huu utaisha lini aisee
 
Back
Top Bottom