Gharama ya Maendeleo - Kupanga ni kuchagua!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Tangu jana reality imeanza kuniingia taratibu na imeanza kuniangazia kama vile jua lichomozavyo alfajiri! Na kama vile Zuhura mwanga wake umeendelea kubakia katika akili zangu kwa muda sasa. Nimejikuta nikifia hitimisho ambalo upande mmoja linakatisha tamaa lakini upande wa pili linatia moyo.

Kwamba, ukosoaji wetu mwingi wa serikali, uongozi, na taasisi mbalimbali yawezekana umeshindwa kuzingatia kitu kimoja kikubwa, kitu ambacho hatujakishughulikia bado. Siyo sisi tu lakini pia kama viongozi tumeshindwa kuamua ni nini tufanye kwanza na matokeo yake tumejilundikia mambo mengi kiasi kwamba tunajikuta nguvu zetu zimetawanyika na hivyo kufanya mambo mengi kidogo, kuliko kufanya mambo machache kwa uzuri zaidi.

Kitu ambacho ninakiona na nimekiona huko nyuma ni kuwa kwa wale ambao tumekaa nje muda mrefu au hata miezi michache tunaporudi nyumbani kutembea tunajikuta wakati mwingine na hisia "siwezi kuishi hapa" na hivyo kusubiri kwa hamu muda wa kurudi tena majuu. Hisia hizi wakati mwingine zinachangiwa na sababu moja kubwa ambayo wale wanaoishi nje hasa nchi za magharibi wanaichukulia "for granted". Kitu hicho ni "convenience" ya maisha.

Sijui neno zuri la "convenience" kwa kiswahili ni lipi lakini nitumie "Urahisi" wa maisha. Hapa ni tofauti na "unafuu" wa maisha. Urahisi wa maisha upo pale ambapo mtu anaweza kupata kitu anachokitaka wakati wowote, kwenda anakotaka wakati wowote, na kufurahia kitu anachotaka wakati wowote. Ukitaka maziwa, hauhitaji kumsubiri mtu afungue duka, au mtoto toka kwa kina "John" alete maziwa asubuhi kabla hamjaanza kupika chai.

Katika maisha yenye "urahisi" mahitaji muhimu ya kila siku siyo ya kutabirika au kupiga mahesabu utaenda kuyapata vipi. Kama unataka kutafuta kitoweo si lazima uende ferry, mwaloni, tandika, "soko mjinga", soko matola, n.k lakini kule kule unakoishi unaweza kupata karibu mahitaji yote na zaidi ya yote, siyo katika muda fulani lakini muda wote wa siku.

Ni kweli kuwa hata ughaibuni maduka mengi hufungwa jioni na si yote yanayofanya kazi masaa ishirini na nne au kufanya kazi hadi jumapili lakini kwenye maeneo mengi kuna vile vinavyoitwa "convenient" stores maduka kama "Seven 11" n.k ambapo mtu waweza kwenda saa ya yoyote na kupata unachohitaji. Hili ni gumu kwenye nchi kama ya kwetu hasa kwa watu wetu wengi ukiondoa wale wa mjini ambao kidogo maisha ni rahisi zaidi.

Tatizo la maji kwa mfano, kwa watu wengi bado linabakia kuwa ni ndoto kwani japo kuwa maji yapo lakini upatikanaji wake ni hadi uende mtaa wa pili, kwenye bomba la kijiji, au wakati fulani hadi "wauza maji" wapite. Nakumbuka mwaka 2005 nilipokuwa nyumbani wakati fulani gari la "Fire" lilitumika kutuletea maji mtaani kwetu.

Angalia kwa mfano tatizo la kutumia muda. Watanzania na bila ya shaka wananchi wengine wa nchi za zinazotaka kuendelea wanapoteza muda mrefu sana njiani. Mahali ambapo pangetumia saa moja panatumia masaa matatu na wakati mwingine mahali pa masaa manne panachukua masaa 12. Kutoka Dar hadi Kigoma ni umbali wa masaa ishirini na nne tu kwa gari lenye mwendo wa kawaida na kwenye barabara nzuri. Lakini inachukua karibu siku nne na wakati mwingine wiki kwa mtu kutoka Dar hadi Kigoma kwa kutumia usafiri wa barabara. Lakini anayetoka Arusha kwenda Mbeya, anatumia ndani ya masaa ishirini na nne, kiasi kwamba mtu anaweza kufikiri Arusha na Mbeya ni karibu kuliko Kigoma na Dar!

Siyo tu kwenye usafiri mrefu kama huo, hata usafiri ndani ya mji wenyewe bado tunapoteza muda mrefu sana kutoka pointi A kwenda Point B, na wakati mwingine inamlazimu mtu kupitia point X na Z kabla hafika kwenye point B!

Lakini haya yote yanathibitisha nini? Binafsi naamini kuna mambo kadhaa ya kuangalia.

a. Watanzania tunatamani tusivyostahili. Sisi bado ni taifa changa sana na ambalo bado linasafari ndefu kuelekea mafanikio. Hivyo mara nyingi tunapolinganisha maisha ya wananchi wetu na kutaka yawe au "yangeshakuwa" kama ya nchi za magharibi tunashindwa kuona ukweli. Wenzetu wamelipia gharama ya mafanikio na maendeleo miongo kadhaa iliyopita. Bila gharama hiyo tutastahili vipi mafanikio?

b. Watanzania tunatamani tusivyotolea jasho. Tumezoea kuishi kiujanja ujanja sana kiasi kwamba wanaotoa jasho la kweli kwa kazi zao hasa ni wale wanaotumia misuli yao kujipatia kipato. Mafundi ujenzi, wakulima, maseremala, n.k ndio ambao wanahenyeka kila siku kutumia jasho lao kula. Sisi wengine ambao kwa namna fulani tumepata nafasi ya kufanyua kazi za maofisini, hatutoi jasho hasa inapotokea kwamba tunajua "hela zilipo" na tunajua jinsi ya "kuzipata" bila kuhangaika sana.

Kashfa zinazoliandama taifa letu leo hii ni ushahidi wazi wa jambo hilo. Mkapa hakutaka kufanya kazi ya kupata Kiwira kwa haki akatumia "inside information" na Waziri wake wakajigawia mradi huo, na sasa wanatanua! Kina Kagoda na wenzake vivyo hivyo, wasingeweza kupata fedha za EPA kihalali (wangeweza kama wangetaka kutoka jasho) lakini wakaamua kutumia njia ya mkato; Wafanyakazi kwenye maofisi vivyo hivyo wengine wanapofanya kazi wanaangalia ni kwa jinsi gani watajiongezea kipato kwa kuuza mali za serikali au kujikopesha kinyemela alimradi wasitoke jasho!

Kati ya vitu ambavyo nilijifunza tangu mdogo ni kuwa hakuna mafanikio yasiyo tokana na jasho. Wazazi wangu walinifundisha mapema kutafuta fedha kwa njia halali. Nakumbuka jinsi ambavyo tulijifunza kuuza "mchicha" tuliopanda katika bustani za nyumbani na fedha tulizozipata kuzitia mfukoni na kuzitumia tupendavyo kwani ni za "kwetu". Watu walikuwa wanashangaa kwanini "watoto wa mkubwa" wauze mchicha na nakumbuka hisia ya aibu na kukereka "kudhalilishwa" hivyo. Ni baadaya ya kuona njuluku zinavyoingia ndivyo fedhea na aibu ilipotoka na kujifunza somo moja kubwa, kazi halali ya mtu haina aibu wala fedheha! Leo hii, ni wachache wetu kweli ambao wanaweza kubadili kibarua chao na kuweza kuishi kwa jasho lao.

c. Watanzania tumezoea vya kunyonga. Hakuna kitu kibaya kama kuzoea mambo rahisi rahisi na njia za mkato. Mojawapo ya masomo ya kipindi cha 'Azimio la Arusha' na somo la kipindi cha "Ulanguzi" ni kuwa aliyezoea njia ya mkato ni vigumu kufuata njia sahihi.

Nakumbuka miaka ile tulipoimba kwa fahari "mabepari yalia, kukatiwa mirija" sikujua ni jinsi gani kuna baadhi ya watu kiliwauma sana hadi leo hii. Siwezi kushangaa leo hii tukianza kuimba tena "Mafisadi walia" kuna watu ambao watachukia kabisa kwa sababu tunajaribu kuwakatia mirija yao mirefu inayotumika kila kukicha kunyonya raslimali zetuu kama vile mbu anyonyavyo damu utadhani kama kwa mashine ya pump!

Kama mtu anaweza kuingia mkataba wa majenereta bila kufuata sheria alimradi kaleta jenereta kuna ubaya gani? Kama mtu anaweza kutumia fedha za umma kununua gari la umma bila kufuata taratibu za matumizi ya fedha za serikali kuna ubaya gani si gari limepatikana?

Ni mawazo haya ambayo kwa namna fulani yamechangia sana kutuchelewesha kuelekea maendeleo kwani kufuata taratibu na sheria ni kazi! Kufuata taratibu na sheria kuna maana ya kuwajibika, na kuwajibika kuna maana kuwa mwadilifu, na hili la kuwa mwadilifu ni gumu! tumezoea kuishi kijanja janja!

Naweza kusema mengi sana, lakini kimsingi ni kuwa kama kweli tunataka tuendelee na kuwa kama nchi zili tuzitamanio na kuwa na maisha yale tuyatakayo ni lazima tulipe gharama ya maendeleo! Gharama hiyo inalipwa kwanza na mtu mmoja mmoja na hatimaye na kama jumuiya na Taifa. Kama wizara moja ikianza kufuata taratibu, kama idara moja ikianza kuonesha njia, kama mfanyakazi mmoja ataanza kuwa mwadilifu na kuusimamia uadilifu wake basi cheche za maendeleo zitaanza kusababisha moto mkubwa wa mafanikio!

Lakini kwa kadiri ya kwamba tumekubali hali ilivyo na kuishi kwa tamaa ya "samaki wa picha" ndivyo hivyo hivyo tutajikuta tunakasirika na kukerwa kwani mambo hayawi jinsi yanavyopaswa kuwa.

Je, ni mambo gani ambayo yataonesha kuwa tumeanza kulipigia gharama ya maendeleo? Je nchi zilizoendelea zilifanya nini hasa kuhakikisha kuwa vikwazo nilivyovitaja hapo juu siyo tu vimeondolewa kabisa lakini vimepunguzwa kwa kiasi kikubwa na kusababisha maisha ya "urahisi"? Je tunaweza kweli kujenga taifa la kisasa, la kitanzania, bila ya kulipa gharama ya maendeleo?

Kwa sasa hayo yamebakia kwangu ni maswali!

M. M.
 
Heshima mbele mwanakijiji!!!!!!!!!

Tatizo kubwa naloliona kwa nchi yetu ni usanii, tumeubeba usanii, tumeutukuza, tuimeukumbatia tunatembea nao. Hata Mwalimu JKN amewahi kun'gaka wkt flani kwamba hii tabia mfano ya uvivu tumeitoa wapi maana wakoloni hawakuwa wavivu......... cha jabu ofisi zilezile ambazo watanganyika walikuwa wakipiga kazi kwa bidii chini ya mkoloni kukaanza usanii na uvivu.

Nchi yetu kwa sasa imekosa viongozi wa kuinspire watu, viongozi wenye visheni na viongozi wakweli. Inashangaza kumsikia hata raisi wa nchi akizungumzia tatizo la madawati, hv kweli hilo tatizo liko level hiyo??????????? Watanzania walio wengi leo ukiwaambia shule picha wanayokuwa nayo ni mjengo wa elo au yu, no ceilings, vyoo vya shimo, na madirisha ya mbao zilizopigiliwa permanently.

Viongozi kama wabunge ambao kazi yao kubwa inatakiwa kuwa ni kuoganaizi watu kupanga maendeleo yao leo wananchi wanawategemea wawe ni donors......Na sisi wananchi hasa wa mijini ndio kabisa hatuwezi hata kukaa pamoja kuakomplishi kaishu ka mtaro mtaani ambao gharama yake inaweza isiszidi laki.

Suala la kazi ni kipimo cha utu halipo tena bali waleti yako ndio haswaaa kipimo. Sijui tunaenda wapi?

Hivi kweli tukiamua kufunga mikanda tukasambaza natural gas nchi nzima haiwezekani????? Maana gesi ipo na gharama yake ni asilimia kama 28 tu ya petroli na hapo ndipo tutakuwa tumeanza kutengeneza misingi ya kweli ya kutoka. Magari, mashine za kusaga, kupasua mbao, kusindika maziwa nk yote itawezekana kwa gharama nafuu kabisa. Wale marafiki zetu wa zamani urusi hawawezi kutusaidia kweli kwa hili hata kwa mkopo maana hao ni wataalamu sana wa hii kitu!!!!

Miundo mbinu, hivi China ilivyo na njaa ya metals kwa sasa hatuwezi kuwakodishia mchuchuma kwa say miaka 30 wakajenga barabara zote lami kwa standard ya hali ya juu? Nisijeonekana kwamba nafikiri nchi itaendelea kwa misaada bali hii ni mifano halisi ambayo inawezekana na hata makampuni ya kibeppari huwa yanafanya.

Hivi hatuwezi kuwa hata na miji say mitatu nchini ya mfano ambayo huko systems zikawa ziko in place, mipango miji ya hali ya juu, miti, maji na umeme wa uhakika, shule nk? Na mengine mengi mengi tu.

Nna uhakika tunaweza sasa nini kinatuzuia?????

1. Kuweka siasa mbele na kwenye kila ishu.

2. Usanii kwa wananchi na serikali pia.

3. Uvivu hasa kwa watu wa mijini na kutokuwa na national focus, at least on one item.

4. CCM

5. Kutokuprayoritaizi na kuwa na malengo yenye clear action plans.
 
Juzi darasani kuna mtu aliniuliza kuwa kwa nini nchi yetu ni masikini wakati bei ya dhahabu inapanda siku hadi siku. Ilikuwa ni kind of attack na sikuwa nimejiandaa kujibu hili swali kwa dk mbili ambazo nilitegemewa kumweleza aelewe kuwa viongozi wangu wa serikali wanachangia kwa kiwango kikubwa kufanya nchi iwe masikini kwa wizi wao na ukosefu wao wa utu na utaifa.

Kwa kufanya story iwe fupi, nikamjibu kuwa ninasoma sasa hivi ili kujua jibu sahihi la hili swali. Kitu kikubwa nimeona hapa ni kuwa inafikia nafasi watu kuanzia somewhere. Juzi nilifurahi kusoma kuwa Mtanzania (memba wa JF) anakubali kupokea uteuzi wa ukatibu kata ili afanye the right thing kwenye level ya kata na kuendelea juu.

Mwanakijiji, najaribu kubadili hii thread yako kwenda kwenye umombo ili nimtumie rafiki yangu aliyeniuliza swali lile na kuweka hii debate kwenye another perspective.

Asante sana!
 
Tunaweza kuzunguka sana kuhusu chanzo cha umasikini wetu. lakini ukweli unabaki pale pale. Uongozi ndio umetu-let down! Kwa kweli kwa miaka arobaini ya uhuru tulipaswa kuwa mbali zaidi ya hapa tulipo leo. Ajabu ni kwamba viongozi wale wale waliotufikisha hapa tulipo ndio wanatuongoza leo na kutuambia wao ndio wametuletea maendeleo, amani na utulivu tulio nao sasa.

Hivi kwa nini usifanyike madahalo mkubwa wa kitaifa wa kuwaumbua hawa watu waliotufikisha hapa? Wanaweza kujitetea kwa jinsi yoyote ile? Dhamira zao haziwaumi kwamba wanaelekea sasa kaburini huku wakiiacha nchi kwenye umasikini wa kutupa lakini yenye utajiri wa rasilimali?

Aibu, aibu, aibu...... shame on you ...
 
Tabaka la uongozi uliopo hauna nia dhabiti ya kutaka kuwatumikia na kuleta maendeleo kwa wananchi. Kinachoangaliwa kwa sasa ni maendeleo na maslahi binafsi.

Hizi skendo tunazozisikia si kwamba watu wana uchungu na nchi, bali ni kulipizana visasi, kujaribu kukomoana au kuchafuana wao kwa wao.

Kwa kufua nguo zao za ndani hadharani, na sisi wananchi tumeweza kujua uozo uliopo katika uongozi wetu.

Aluta continua
 
Heshima mbele mwanakijiji!!!!!!!!!

Tatizo kubwa naloliona kwa nchi yetu ni usanii, tumeubeba usanii, tumeutukuza, tuimeukumbatia tunatembea nao. Hata Mwalimu JKN amewahi kun'gaka wkt flani kwamba hii tabia mfano ya uvivu tumeitoa wapi maana wakoloni hawakuwa wavivu......... cha jabu ofisi zilezile ambazo watanganyika walikuwa wakipiga kazi kwa bidii chini ya mkoloni kukaanza usanii na uvivu.

Nchi yetu kwa sasa imekosa viongozi wa kuinspire watu, viongozi wenye visheni na viongozi wakweli. Inashangaza kumsikia hata raisi wa nchi akizungumzia tatizo la madawati, hv kweli hilo tatizo liko level hiyo??????????? Watanzania walio wengi leo ukiwaambia shule picha wanayokuwa nayo ni mjengo wa elo au yu, no ceilings, vyoo vya shimo, na madirisha ya mbao zilizopigiliwa permanently.

Viongozi kama wabunge ambao kazi yao kubwa inatakiwa kuwa ni kuoganaizi watu kupanga maendeleo yao leo wananchi wanawategemea wawe ni donors......Na sisi wananchi hasa wa mijini ndio kabisa hatuwezi hata kukaa pamoja kuakomplishi kaishu ka mtaro mtaani ambao gharama yake inaweza isiszidi laki.

Suala la kazi ni kipimo cha utu halipo tena bali waleti yako ndio haswaaa kipimo. Sijui tunaenda wapi?

Hivi kweli tukiamua kufunga mikanda tukasambaza natural gas nchi nzima haiwezekani????? Maana gesi ipo na gharama yake ni asilimia kama 28 tu ya petroli na hapo ndipo tutakuwa tumeanza kutengeneza misingi ya kweli ya kutoka. Magari, mashine za kusaga, kupasua mbao, kusindika maziwa nk yote itawezekana kwa gharama nafuu kabisa. Wale marafiki zetu wa zamani urusi hawawezi kutusaidia kweli kwa hili hata kwa mkopo maana hao ni wataalamu sana wa hii kitu!!!!

Miundo mbinu, hivi China ilivyo na njaa ya metals kwa sasa hatuwezi kuwakodishia mchuchuma kwa say miaka 30 wakajenga barabara zote lami kwa standard ya hali ya juu? Nisijeonekana kwamba nafikiri nchi itaendelea kwa misaada bali hii ni mifano halisi ambayo inawezekana na hata makampuni ya kibeppari huwa yanafanya.

Hivi hatuwezi kuwa hata na miji say mitatu nchini ya mfano ambayo huko systems zikawa ziko in place, mipango miji ya hali ya juu, miti, maji na umeme wa uhakika, shule nk? Na mengine mengi mengi tu.

Nna uhakika tunaweza sasa nini kinatuzuia?????

1. Kuweka siasa mbele na kwenye kila ishu.

2. Usanii kwa wananchi na serikali pia.

3. Uvivu hasa kwa watu wa mijini na kutokuwa na national focus, at least on one item.

4. CCM

5. Kutokuprayoritaizi na kuwa na malengo yenye clear action plans.

sawa kabisa nyambala,hatuwezi kuendelea kama CCM itaendelea kuwepo madarakani,vipi tunaweza kuing'oa?hapo ndio kwenye kazi kubwa kwani hawa jamaa mtandao wao umeshakuwa mkubwa sana kiasi kwamba tunaweza tukajikuta tunaendelea kuongozwa na wasio na uchungu na nchi(CCM)kwa miaka mingi mbeleni kwani Kila kitu chenye maslahi na nchi yetu basi lazima siasa za CCM(ufisadi)zitaingia.
Tutake tusitake,tukitaka mabadiliko ya kweli na maisha bora kwa watanzania inabidi watanzania wakiue chama cha mafisadi(CCM)ili wanachama wao watawanyike katika vyama vingine na huko wasipewe hata ujumbe wa wa serikali ya mtaa na hapo tunaweza kupata viongozi wapya kabisa na damu changa yenye uchungu na nchi yao.
Mapinduzi ya kweli yanaweza kuchukua hata miaka100 lakini kama nia ya kweli itakuwepo basi siku moja itakuja kuwa history.
kwani leo tunasikia kuwa UVCCM wanatarajia kufanya uchaguzi,na ukiangalia majina ya wanaotaka kugombea utaona ni WATOTO wa MAFISADI au wana maslahi na MAFISADI,kwa maana hiyo hawa watoto waliokulia kwenye UFISADI ndio watakaokuja kuwa viongozi wetu ktk serikali miaka ijayo
TUFANYEJE?ni wakati wa watanzania na vijana wenye moyo na ujasiri kwenda kuchukua fomu na kugombea kupitia CCM kwa nguvu zote ili waweze kuingia kwenye chama cha mafisadi na kisha wakiingia wajijengee ngome kisha wakisambaratishe,najua kwa njia hii inawezekana ingawa linahitaji subira na uvumilivu wa muda mrefu lakini bila kukisambaratisha CCM na kikifuta kabisa kwa msajili tusitegemee LOLOTE JIPYA!
 
Mwanakijiji,

Nilikuwa nasubiri kuona kama utaandika hii makala kama ulivyoniambia au inabidi nianzishe mada kukukumbusha ahadi yako. Ndiyo maana taratibu nikachombeza na "Que Sera Sera", "Ndivyo Tulivyo" na "Kosa ni kurudia, kulinda na kuendeleza"!

Nafikiri sisi kama jamii na hasa hapa JF inabidi tuanze kwa kuwa mfano wa kuigwa katika kuleta matendo kwa kufanya kazi, tukiwa na tija na ufanisi na kupunguza kufadhaishwa kutokana na dosari na ukosefu wa uongozi bora.

TUmeshakuwa mabingwa wa kulaumu na kutoa boriti au kibanzi kwenye jicho Serikali, je ni lini tutaanza kutoa kwenye macho yetu na kuanza kutoa ushauri wa kujenga Taifa katika nyanja zote bila kuyumbishwa au kuendelea kutegemea Serikali iongoze.

Si kuna sekta binafsi? kwa nini tusiende kwenye sekta binafsi na kuleta mapinduzi na maendeleo?
 
hili la sekta binafsi limekaa kiajabu sana, sekta binafsi iko zaidi katika mambo makubwa mawili katika kubadilisha jamii:

a. Kusaidia michezo
b. Kutoa misaada ya kijamii.

Inasikitisha kuwa hawashiriki kwa kiwango kikubwa katika ujenzi wa sera za manufaa kwa nchi au kutengeneza ajenga za kijamii na kisiasa (by lobbying). Tatizo jingine ni kuwa sekta binafsi (au mashirika na makampuni binafsi)ikianza kusogea karibu na mambo ya siasa swali la loyalty na political alignment linajitokeza. Je mfanyabiashara binafsi anaweza kufanikiwa bila kujionesha kuwa ni mwanaCCM au hahusiki kabisa na mambo ya siasa?
 
Nzuri sana! You are a truly deep thinker!

  1. Utendaji wa kazi bado ni mdogo Tanzania, watu kupenda short cut, kulalamika nk
.

  1. Mentality za kitumwa na umwinyi bado tunazo
Matatizo si kwa watanzania wanaokaa nchini tu, bali wanaokaa nje pia, kimasomo au kutumikia nje. Urahisi wa maisha nchi za magharibi unakuja na gharama zake pia, wengi tunafahamu kina uncle Tom, ambao kila kitu ni kibaya Tanzania wanapokuja kutoka nje. Mimi nawauliza,ni kitu ngani wanaweza kufanya na sisi tuwe na maendeleo kama hizo nchi zingine? Ni jukumu la kila mtanzania kujiendeleza and to take responsibilities
 
Mwanakijiji,
.Lakini kwa kadiri ya kwamba tumekubali hali ilivyo na kuishi kwa tamaa ya "samaki wa picha" ndivyo hivyo hivyo tutajikuta tunakasirika na kukerwa kwani mambo hayawi jinsi yanavyopaswa kuwa.
...

1. Umeonyesha wazi kuwa sisi ni Wapuuzi na Wazembe, hivyo basi:-
2. Viongozi wetu ni reflection yetu - Mzee FMES (wapuuzi na wazembe)
3. Ndivyo tulivyo - Nyani Ngabu (Wapuuzi na Wazembe)
4. Ndivyo Tulivyo na "Kosa ni kurudia, kulinda na kuendeleza"! (upuuzi na Uzembe) - Rev Kishoka!

Lugha ni ile ile tu mkuu -Tukikubali maradhi tuliyokuwa nayo basi ni rahisi kutafuta dawa!..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom