Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,484
Tangu jana reality imeanza kuniingia taratibu na imeanza kuniangazia kama vile jua lichomozavyo alfajiri! Na kama vile Zuhura mwanga wake umeendelea kubakia katika akili zangu kwa muda sasa. Nimejikuta nikifia hitimisho ambalo upande mmoja linakatisha tamaa lakini upande wa pili linatia moyo.
Kwamba, ukosoaji wetu mwingi wa serikali, uongozi, na taasisi mbalimbali yawezekana umeshindwa kuzingatia kitu kimoja kikubwa, kitu ambacho hatujakishughulikia bado. Siyo sisi tu lakini pia kama viongozi tumeshindwa kuamua ni nini tufanye kwanza na matokeo yake tumejilundikia mambo mengi kiasi kwamba tunajikuta nguvu zetu zimetawanyika na hivyo kufanya mambo mengi kidogo, kuliko kufanya mambo machache kwa uzuri zaidi.
Kitu ambacho ninakiona na nimekiona huko nyuma ni kuwa kwa wale ambao tumekaa nje muda mrefu au hata miezi michache tunaporudi nyumbani kutembea tunajikuta wakati mwingine na hisia "siwezi kuishi hapa" na hivyo kusubiri kwa hamu muda wa kurudi tena majuu. Hisia hizi wakati mwingine zinachangiwa na sababu moja kubwa ambayo wale wanaoishi nje hasa nchi za magharibi wanaichukulia "for granted". Kitu hicho ni "convenience" ya maisha.
Sijui neno zuri la "convenience" kwa kiswahili ni lipi lakini nitumie "Urahisi" wa maisha. Hapa ni tofauti na "unafuu" wa maisha. Urahisi wa maisha upo pale ambapo mtu anaweza kupata kitu anachokitaka wakati wowote, kwenda anakotaka wakati wowote, na kufurahia kitu anachotaka wakati wowote. Ukitaka maziwa, hauhitaji kumsubiri mtu afungue duka, au mtoto toka kwa kina "John" alete maziwa asubuhi kabla hamjaanza kupika chai.
Katika maisha yenye "urahisi" mahitaji muhimu ya kila siku siyo ya kutabirika au kupiga mahesabu utaenda kuyapata vipi. Kama unataka kutafuta kitoweo si lazima uende ferry, mwaloni, tandika, "soko mjinga", soko matola, n.k lakini kule kule unakoishi unaweza kupata karibu mahitaji yote na zaidi ya yote, siyo katika muda fulani lakini muda wote wa siku.
Ni kweli kuwa hata ughaibuni maduka mengi hufungwa jioni na si yote yanayofanya kazi masaa ishirini na nne au kufanya kazi hadi jumapili lakini kwenye maeneo mengi kuna vile vinavyoitwa "convenient" stores maduka kama "Seven 11" n.k ambapo mtu waweza kwenda saa ya yoyote na kupata unachohitaji. Hili ni gumu kwenye nchi kama ya kwetu hasa kwa watu wetu wengi ukiondoa wale wa mjini ambao kidogo maisha ni rahisi zaidi.
Tatizo la maji kwa mfano, kwa watu wengi bado linabakia kuwa ni ndoto kwani japo kuwa maji yapo lakini upatikanaji wake ni hadi uende mtaa wa pili, kwenye bomba la kijiji, au wakati fulani hadi "wauza maji" wapite. Nakumbuka mwaka 2005 nilipokuwa nyumbani wakati fulani gari la "Fire" lilitumika kutuletea maji mtaani kwetu.
Angalia kwa mfano tatizo la kutumia muda. Watanzania na bila ya shaka wananchi wengine wa nchi za zinazotaka kuendelea wanapoteza muda mrefu sana njiani. Mahali ambapo pangetumia saa moja panatumia masaa matatu na wakati mwingine mahali pa masaa manne panachukua masaa 12. Kutoka Dar hadi Kigoma ni umbali wa masaa ishirini na nne tu kwa gari lenye mwendo wa kawaida na kwenye barabara nzuri. Lakini inachukua karibu siku nne na wakati mwingine wiki kwa mtu kutoka Dar hadi Kigoma kwa kutumia usafiri wa barabara. Lakini anayetoka Arusha kwenda Mbeya, anatumia ndani ya masaa ishirini na nne, kiasi kwamba mtu anaweza kufikiri Arusha na Mbeya ni karibu kuliko Kigoma na Dar!
Siyo tu kwenye usafiri mrefu kama huo, hata usafiri ndani ya mji wenyewe bado tunapoteza muda mrefu sana kutoka pointi A kwenda Point B, na wakati mwingine inamlazimu mtu kupitia point X na Z kabla hafika kwenye point B!
Lakini haya yote yanathibitisha nini? Binafsi naamini kuna mambo kadhaa ya kuangalia.
a. Watanzania tunatamani tusivyostahili. Sisi bado ni taifa changa sana na ambalo bado linasafari ndefu kuelekea mafanikio. Hivyo mara nyingi tunapolinganisha maisha ya wananchi wetu na kutaka yawe au "yangeshakuwa" kama ya nchi za magharibi tunashindwa kuona ukweli. Wenzetu wamelipia gharama ya mafanikio na maendeleo miongo kadhaa iliyopita. Bila gharama hiyo tutastahili vipi mafanikio?
b. Watanzania tunatamani tusivyotolea jasho. Tumezoea kuishi kiujanja ujanja sana kiasi kwamba wanaotoa jasho la kweli kwa kazi zao hasa ni wale wanaotumia misuli yao kujipatia kipato. Mafundi ujenzi, wakulima, maseremala, n.k ndio ambao wanahenyeka kila siku kutumia jasho lao kula. Sisi wengine ambao kwa namna fulani tumepata nafasi ya kufanyua kazi za maofisini, hatutoi jasho hasa inapotokea kwamba tunajua "hela zilipo" na tunajua jinsi ya "kuzipata" bila kuhangaika sana.
Kashfa zinazoliandama taifa letu leo hii ni ushahidi wazi wa jambo hilo. Mkapa hakutaka kufanya kazi ya kupata Kiwira kwa haki akatumia "inside information" na Waziri wake wakajigawia mradi huo, na sasa wanatanua! Kina Kagoda na wenzake vivyo hivyo, wasingeweza kupata fedha za EPA kihalali (wangeweza kama wangetaka kutoka jasho) lakini wakaamua kutumia njia ya mkato; Wafanyakazi kwenye maofisi vivyo hivyo wengine wanapofanya kazi wanaangalia ni kwa jinsi gani watajiongezea kipato kwa kuuza mali za serikali au kujikopesha kinyemela alimradi wasitoke jasho!
Kati ya vitu ambavyo nilijifunza tangu mdogo ni kuwa hakuna mafanikio yasiyo tokana na jasho. Wazazi wangu walinifundisha mapema kutafuta fedha kwa njia halali. Nakumbuka jinsi ambavyo tulijifunza kuuza "mchicha" tuliopanda katika bustani za nyumbani na fedha tulizozipata kuzitia mfukoni na kuzitumia tupendavyo kwani ni za "kwetu". Watu walikuwa wanashangaa kwanini "watoto wa mkubwa" wauze mchicha na nakumbuka hisia ya aibu na kukereka "kudhalilishwa" hivyo. Ni baadaya ya kuona njuluku zinavyoingia ndivyo fedhea na aibu ilipotoka na kujifunza somo moja kubwa, kazi halali ya mtu haina aibu wala fedheha! Leo hii, ni wachache wetu kweli ambao wanaweza kubadili kibarua chao na kuweza kuishi kwa jasho lao.
c. Watanzania tumezoea vya kunyonga. Hakuna kitu kibaya kama kuzoea mambo rahisi rahisi na njia za mkato. Mojawapo ya masomo ya kipindi cha 'Azimio la Arusha' na somo la kipindi cha "Ulanguzi" ni kuwa aliyezoea njia ya mkato ni vigumu kufuata njia sahihi.
Nakumbuka miaka ile tulipoimba kwa fahari "mabepari yalia, kukatiwa mirija" sikujua ni jinsi gani kuna baadhi ya watu kiliwauma sana hadi leo hii. Siwezi kushangaa leo hii tukianza kuimba tena "Mafisadi walia" kuna watu ambao watachukia kabisa kwa sababu tunajaribu kuwakatia mirija yao mirefu inayotumika kila kukicha kunyonya raslimali zetuu kama vile mbu anyonyavyo damu utadhani kama kwa mashine ya pump!
Kama mtu anaweza kuingia mkataba wa majenereta bila kufuata sheria alimradi kaleta jenereta kuna ubaya gani? Kama mtu anaweza kutumia fedha za umma kununua gari la umma bila kufuata taratibu za matumizi ya fedha za serikali kuna ubaya gani si gari limepatikana?
Ni mawazo haya ambayo kwa namna fulani yamechangia sana kutuchelewesha kuelekea maendeleo kwani kufuata taratibu na sheria ni kazi! Kufuata taratibu na sheria kuna maana ya kuwajibika, na kuwajibika kuna maana kuwa mwadilifu, na hili la kuwa mwadilifu ni gumu! tumezoea kuishi kijanja janja!
Naweza kusema mengi sana, lakini kimsingi ni kuwa kama kweli tunataka tuendelee na kuwa kama nchi zili tuzitamanio na kuwa na maisha yale tuyatakayo ni lazima tulipe gharama ya maendeleo! Gharama hiyo inalipwa kwanza na mtu mmoja mmoja na hatimaye na kama jumuiya na Taifa. Kama wizara moja ikianza kufuata taratibu, kama idara moja ikianza kuonesha njia, kama mfanyakazi mmoja ataanza kuwa mwadilifu na kuusimamia uadilifu wake basi cheche za maendeleo zitaanza kusababisha moto mkubwa wa mafanikio!
Lakini kwa kadiri ya kwamba tumekubali hali ilivyo na kuishi kwa tamaa ya "samaki wa picha" ndivyo hivyo hivyo tutajikuta tunakasirika na kukerwa kwani mambo hayawi jinsi yanavyopaswa kuwa.
Je, ni mambo gani ambayo yataonesha kuwa tumeanza kulipigia gharama ya maendeleo? Je nchi zilizoendelea zilifanya nini hasa kuhakikisha kuwa vikwazo nilivyovitaja hapo juu siyo tu vimeondolewa kabisa lakini vimepunguzwa kwa kiasi kikubwa na kusababisha maisha ya "urahisi"? Je tunaweza kweli kujenga taifa la kisasa, la kitanzania, bila ya kulipa gharama ya maendeleo?
Kwa sasa hayo yamebakia kwangu ni maswali!
M. M.