Gharama ya Kuweka Solar VS Umeme wa Tanesco, wataalam mtuchanganulie...

Tatizo ni kwamba watanzania wengi walifeli hisabati na inawezekana hata wewe ni mmojawao.

Hiyo milioni tatu ni kwamba hutaendelea kulipia bill za umeme. Hapo unakuwa umejikomboa kwa miaka 25 ijayo.
Hio sio shidaa... Masharti ya matumizi na Pia umeme wake hauna nguvu ya uhakikaa kiasi hicho.. Kingine sio kila siku kuna Juaa..! Kuna msimu wa mvuaa na mawingu siku nzimaa.. Unapiga hesabu ya Miaka 25 ya kuishi kwa matumaini


Nitatumia solar kama Umeme wa tanesco haupoo na si vinginevyooo... Hayo ndo yale mahesabu yenu ya faida za Kulima matikitiii...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hio sio shidaa... Masharti ya matumizi na Pia umeme wake hauna nguvu ya uhakikaa kiasi hicho.. Kingine sio kila siku kuna Juaa..! Kuna msimu wa mvuaa na mawingu siku nzimaa.. Unapiga hesabu ya Miaka 25 ya kuishi kwa matumaini


Nitatumia solar kama Umeme wa tanesco haupoo na si vinginevyooo... Hayo ndo yale mahesabu yenu ya faida za Kulima matikitiii...

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa tunaelimishana ...
Kuna siku betri inaonekana imejaa by saa nne asubuhi; ukiona hivyo toa betri weka nyingine ... siku kuna wingu tumia betri ya ziada.
 
Haya mkuu.. !! Mambo ya kubadilisha mabetri tenaa...

Sent using Jamii Forums mobile app
Tafuta fundi akuungie betri zote ulizo nazo ili ikijaa moja iendelee kuchajiwa nyingine.

Hata Tanesco huwa wanatoa sababu za umeme wao kukatika kwamba ni upungufu wa maji kwenye vyanzo vyao. Hapa kinachoonekana ni kwamba watanzania wengi hawana ile kasumba ya kujitegemea. Utakuwa tegemezi hadi lini?
 
Ghalama ya kuweka sola yenye uwezo sawa na umeme wa tanesco ambao haujakatika zina uuwiano gani?

Faida na hasara ni zipi ktika option zote mbili?

wadau karibuni kwa ufafanuzi...
Sio solar tu, hata kama kuna option nyingize ambazo hazina uhusiano na GRID yetu (non-grid electricity)
Weka orodha ya vifaa vyako.
 
Nimenunua panel ya wat 40 (oceanic); betri ya volti 12 yenye 18AH, kwa laki na nusu.

Nimefunga taa NNE: mbili za nje ambazo ni wat 1 kila moja na huwaka kuanzia usiku had asubuhi; moja chumbani yenye wat 2, na moja chooni yenye wat 1.


Ninachaji simu zangu, na za wengine kwa malipo ya mia mbili.

Pia nimefunga charger controller kwa usalama wa betri.

Betri hujaa had volti 13.2. hata kama kuna mawingu.

Na kwa matumizi ya usiku, chaji hushuka hadi volti 12.7-12.5.


Na huanza kuchaji ifikapo SAA 12 asubuhi, so hadi SAA mbili asubuhi, betri inakuwa imejaa kufikia volti 13.3-13.5


Nimenunua mwez wa nane mwaka huu
Mkuu Aikambee naomba ingia PM kwako tafadhali,nahitaji msaada wako kidogo

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Nitafuteni niwaunhanishe na kampuni inayotoa huduma ya Sola na vifaa vyake toka ujerumani. Mwenyewe kuhitaji KARIBU PM. TUNAKOPESHA NA PIA TUNAUZA KWA CASH. Gharama za kufungiwa ni huu yetu.
 
Back
Top Bottom