Gharama ya Kuweka Solar VS Umeme wa Tanesco, wataalam mtuchanganulie...

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
45,532
2,000
Kama mfuko uko njema tafuta aina ya Generator Zinazoweza kujiwasha zenyewe Electric start, Hizi Unaweza fungiwa na automatic transfer switch na hauta notice power outage kabisa
Stand by generator.
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
45,532
2,000
Standby ni General name ila Technical zinaitwa Electric start tofauti na zile recoil start za ku pull up na kamba.
Ok, sema hizi si zinakuwa zile kubwa. Au kuna ndogo zina hio option?
 

Yales

JF-Expert Member
Oct 3, 2015
517
500
Ok, sema hizi si zinakuwa zile kubwa. Au kuna ndogo zina hio option?
Mara nyingi ni Zile kubwa ila ndogo pia zinaweza Fanyiwa modifications zikawa na hio function, Nunua tu kubwa kwanza iko na kelele kidogo mno
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
45,532
2,000
Mara nyingi ni Zile kubwa ila ndogo pia zinaweza Fanyiwa modifications zikawa na hio function, Nunua tu kubwa kwanza iko na kelele kidogo mno
Kubwa sina kazi nayo vile vile gharama zake siziwezi.
 

ellyrehema

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
1,199
2,000
mkuu solar wanatumia bettry ambazo kama unaataka N100 ni sh 200,000 mpaka 250,000 na ina llifetime 3-4 yers na inaanza kuchoka so infabidi ununue nyingine..kipindi chaa mvua ni majanga hata mawingu tuu shida
Boss nimekulia kwenye sola. Iliwekwa nikiwa nanmiaka 5 na sasa na 40 kasoro mwaka mmoja tu. Na bado inafanya bila shida, Pia nimesoma kidogo mambo ya solar. Service huwa nikubadili mabetri tu kila baada ya miaka 3-3.5 kama mawingu yanasababisha kukosa umeme ujue system designer wako mburura. Kuna kitu kinaitwa hours of autonomy usipo kizingatia lazima hayo unayoyasema yajitokeze. Unatakiwa uweke kama masaa 72 for the best result ila kawaida masaa 48 yaanikiwa usiku kwa siku mbili bado wewe utaendelea kupata umeme.
 

ellyrehema

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
1,199
2,000
Ila pia na watumiaji. Unapotumia sola lazima uwe very trick. Mf. Ukiona jua hakuna siku ya kwanza na siku ya pili basi kwenye siku ya pili unaanza kupunguza vifaa ambavyo havina ulazima sana kutumika ili kutunza umeme usiishe mapema.
 

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
17,351
2,000
Mkuu kuna Project zinaendelea ,Solar panel yako inafungwa Na Case ambayo ita rotate na kufata upande wenye Jua zaidi
Hii niliiona youtube... Wanatumia arduino kama sijakosea... Yani inafwata jua lilipo


....
 

Yales

JF-Expert Member
Oct 3, 2015
517
500
Hii niliiona youtube... Wanatumia arduino kama sijakosea... Yani inafwata jua lilipo


....
Mimi nilifanya kwa Kutumia Sensor za LDR niliziaset nyingi ktk angle tofauti itakayokuwa illuminated zaidi inapeleka signal kwenye relay na Kuwasha Motor inayo rotate kidogo na kuturn off, Ukitumia Arduino inakuwa advanced zaidi na Ufanisi utapanda mkuu
 

ellyrehema

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
1,199
2,000
Hii niliiona youtube... Wanatumia arduino kama sijakosea... Yani inafwata jua lilipo


....
Yess hii kitu ipo ila kwa tanzania sijazion. Maanangharama zake kubwa. Ina search kitu inaitwa MPTS MAXMUM POWER TRACKING SYSTEMyenyewe inazunguka kufuata uelekeo wa jua
 

ellyrehema

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
1,199
2,000
Ila huwa kuna mahesabu tunafanya kuitafuta hiyo MPT angalau uwe na masaa5-8 ya kupata jua katika siku nzima. Ila kwa ukanda waikweta sio kazi sana. Maana mda mwingi jua huwa lipo katikati
 

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,383
2,000
Kwa upande wangu, solar ni nzuri kama Back up tu. Unapokuwa kwenye Grid, unaweza kuwa na matumizi ya namna zote(domestically) bila kujali uwezo wa supply yako.

Solar ikiwa ndio primary source, utajikuta mwisho wa siku unaanza kuongea lugha za kiumeme hata kama huna taaluma hiyo.

Ndalilo, jibu lako ni sahihi kabisa (maandishi mekundu).

Nishati mbadala ya umeme, kwa matumizi ya nyumbani haiwezi kuwa nguvu ya jua (solar), ila ya nguvu ya maji (hydro) au upepo (wind). Sababu ni kwamba mbali na sahani (panel) za kukusanya nguvu ya jua kuhitajika kuwa kubwa, kumudu kutoa nishati inayohitajika, utahitaji vifaa vingi kubadilisha mfumo wa umeme kutoka DC kwenda AC, ili uweze kutumika nyumbani, kwa kuwa vifaa vingi vimetengenezwa kutumia AC.

Pamoja na mahitaji hayo, utahitaji betri za kuhifadhi umeme wakati hakuna jua. Na hili ni kikwazo kikubwa sana kwa kuwa haiwezekani kuwa na jua wakati wote na uwezekano wa kuwa na betri kwa ajili ya kutunza umeme, siyo tu ni gharama, utahitaji nyingi sana. Kumbuka, betri nazo zina maisha yake.
 

Arien

JF-Expert Member
Aug 29, 2017
11,095
2,000
Mimi ni mpenzi sana wa umeme mbadala kwa Tanesco...


Ila haya mambo ya kutaka ukifunga solar basi utafute pasi,tv,taa nk za solar pia zinazeleta ukakasi. Na ishu ya kuwa unabadilisha kila baada ya muda fulani ni wangapi tunaliweza hilo? Hizi ndo baadhi ya sababu za mimi kuendelea kubaki na hawa hawa wahuni waliobomolewa jengo lao!
 

Aikambee

JF-Expert Member
Sep 27, 2017
4,039
2,000
Hizo basic info plus wauzaji wengi nawajua, nilitegemea nipate more info kwa huyu mtaalam hapa kwenye thread.[/QUOTE


huyu 'mtaalamu' anajibu kisiasa yaani anakwepa maswali. mfano, ulimuuliza kuwa kwa matumizi yako ya kawaida ya taa, TV, radio, ni solar ya ukubwa gani? ila majibu kwa kuzunguuuka.

kwanza lugha yenyewe anaboronga.


ghalama badala ya gharama.


kwa uzoefu wangu, wew anza na sola za kuwashia taa, TV, na redio, kama alivyokudhaur jamaa mmoja hapo.

then uanze kupanda taratibu.

usisahau kufunga solar charge controller
 

Aikambee

JF-Expert Member
Sep 27, 2017
4,039
2,000
Yangu nlinunua 530,000
Panel watts 150
Battery N120
Charger control
Inverter
Pamoja na waya wa kutoka juu kwenye panel had ndani;
Vyote hivyo ndio 530,000

Kwenye mchakato wa kununua waya za wayaring, switch pamoja na gharama za fund ikafika 900

Kwa mchana jua likiwepo unaweza kuangalia tv sanne asubuh had 12 jion, pamoja na feni na kama unachaj simu

Kwa usku kwakua jua hamna unaangalia tv masaa ma3 had matatu nanusu inatgemea na ukubwa wa tv.

Ila kuchaji simu nimda wote
(Pia subwoofer naskilza had nachoka usku na mchana, na vyote hivyo ni vifaa vya umeme wa kawaida sio kwamba ni tv ya sola au redio ya sola)inverter ina ukubwa gani.


pia charge controller ni ya volt ngapi
 

Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
10,579
2,000
Na mimi nichangie walau kwa uchache kwa uzoefu mkubwa wa kazi hii.

Umeme wa solar ni wa uhakika hasa unapokuwa na genuine parts. Pia umeme huu ni wa uhakika ukizingatia Ratings za vifaa unavyo tumia kuanzia Current (A) na power KWH. Pia umeme huu ni wa uhakika kwa nchi kama yetu maana tupo ukanda wa ikweta ambao kwa kawaida haukosi jua kabisa.

Umeme huu ni ghali sana (Initial cost) itakughalimu Fedha nyingi kununua vifaa genuine na ku install. Bei za Solar panels na bei za Battery ni Pasua kichwa. Jinsi matumizi ya umeme yanapo kadiriwa kuwa makubwa basi na gharama za kuandaa mfumo huongezeka

Kwa mtazamo wangu, Umeme huu unafaa eneo ambalo halina umeme wa grid ya Taifa. Lakini kama upo eneo lenye gridi ni nafuu utumie tu umeme wa Tanesco. Na kama utaweza weka na solar system ambayo itakusaidia kuchaji simu na kutazama/ sikiliza taarifa ya habari ikiwa ni pamoja na Lighting na shughuli ndogo. Sahau kuhusu kupiga pasi, Fridge, Water pump na vifaa vinavyo consume more than 1000 Watts au 1kW au 1 horse power (HP)

Umeme wa solar ukitumika kama umeme mbadala/ Buckup ni mzuri sanaaa ila sio ukitumika kama Chanzo kikuu cha nishati.

Kwa maswali zaidi
Occybeats@live.com
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom