Gharama ya Kuweka Solar VS Umeme wa Tanesco, wataalam mtuchanganulie...

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
Ghalama ya kuweka sola yenye uwezo sawa na umeme wa tanesco ambao haujakatika zina uuwiano gani?

Faida na hasara ni zipi ktika option zote mbili?

wadau karibuni kwa ufafanuzi...
Sio solar tu, hata kama kuna option nyingize ambazo hazina uhusiano na GRID yetu (non-grid electricity)
 
Kwa mfumo wa Solar zinazokuja nchini kwetu kwa sasa ni bora kutumia solar tu kuliko Umeme wa Tanesco
Japo solar kwa mara ya kwanza utaingia gharama za ununuaji na Instalation lkn baada ya hapo unasahau kabxaa hii dhiki ya umeme wa Tanesco usioisha kukatika katika
mkuu hakuna muwekezaji, aliyeiona hiyo fursa na kutuletea solar zenye viwango kwa bei rafiki hasa kwenye installation.
 
Kwa upande wangu, solar ni nzuri kama Back up tu. Unapokuwa kwenye Grid, unaweza kuwa na matumizi ya namna zote(domestically) bila kujali uwezo wa supply yako.

Solar ikiwa ndio primary source, utajikuta mwisho wa siku unaanza kuongea lugha za kiumeme hata kama huna taaluma hiyo.
 
Ghalama ya kuweka sola yenye uwezo sawa na umeme wa tanesco ambao haujakatika zina uuwiano gani?

Faida na hasara ni zipi ktika option zote mbili?

wadau karibuni kwa ufafanuzi...
Sio solar tu, hata kama kuna option nyingize ambazo hazina uhusiano na GRID yetu (non-grid electricity)

kama sehemu unayotaka kuweka tayari kuna umeme ume pita yani una hitaji nguzo moja au mbili hata tatu, hapa tanesco itakua nafuu

nitakupa gharama za kuweka solar na tanesco. so far hakuna umeme na kila kitu kipo kwa laptop nayo imesha isha battery
 
Kwa upande wangu, solar ni nzuri kama Back up tu. Unapokuwa kwenye Grid, unaweza kuwa na matumizi ya namna zote(domestically) bila kujali uwezo wa supply yako.

Solar ikiwa ndio primary source, utajikuta mwisho wa siku unaanza kuongea lugha za kiumeme hata kama huna taaluma hiyo.
nakupata vizuri, na mahala pote ninapoziona huwa zinakuwa kama backup.
vipi kwa hiyo mkuu TANESCO ni kama maji, usipoyanywa lazima uyaoge haikwepeki.
Huko duniani tafiti zinasemaje kuhusu non-grid electricity kwa matumizi 24hrs.
 
kama sehemu unayotaka kuweka tayari kuna umeme ume pita yani una hitaji nguzo moja au mbili hata tatu, hapa tanesco itakua nafuu

nitakupa gharama za kuweka solar na tanesco. so far hakuna umeme na kila kitu kipo kwa laptop nayo imesha isha battery
natanguliza shukrani, naamini taarifa zako sio kwa ajili yangu tu bali na wadau humu.
vipi kwa mahala ambapo Tanesco wapo, solar tu bila tanesco sio uamuzi rafiki?
unaweza kutoa na sababu za kitaalam ili kutanua uelewa ktk hilo... hasa sisi vilaza wa mambo ya umeme.
 
Zipo mkuu
Na kuna Makampuni binafsi hapa hapa nchini wanauza na wanakufungia wao pia wanakupa na warranty
Isipokua zinatofautiana Voltage kutokana na bei zao
matumizi na uhakika ndio pa muhimu.
je unaweza kuwa na solar na jirani Tanesco na gharama zako zikawa chini?
lkn wote mkaenjoy 24hrs, 7 weeks, 366days bila shida huku wewe ukiwa na guarantee ya availability.
hiyo case huwa ipo, au solar itabidi uwe unaviziavizia jioni, mara sijui hutumii friji, mara betri zimekufa, mara hazijajaa.
nasema hivyo kwa sababu sijawahi kuona hii case mkuu.
 
Nenda jukwaa la technology palikua na uzi unao ongelea hii solar kwa undan sana...
 
Kwa upande wangu, solar ni nzuri kama Back up tu. Unapokuwa kwenye Grid, unaweza kuwa na matumizi ya namna zote(domestically) bila kujali uwezo wa supply yako.

Solar ikiwa ndio primary source, utajikuta mwisho wa siku unaanza kuongea lugha za kiumeme hata kama huna taaluma hiyo.
Kweli kabisa solar back up ni nzuri na kama unataka kutumia solar kama umeme mbadala ya TANESCO ni gharama kubwa sana na baada ya.miwili ama mitatu lazima uingiee gharama kubwa kwenye betri tena
 
Kweli kabisa solar back up ni nzuri na kama unataka kutumia solar kama umeme mbadala ya TANESCO ni gharama kubwa sana na baada ya.miwili ama mitatu lazima uingiee gharama kubwa kwenye betri tena
nimekupata mkuu...
TANESCO hawana mbadala, wanatakiwa kujua hilo kwa manufaa ya jamii.
badala ya sisi kutafuta backups wao watafute backup incase kuna technical faults.
nimeuliza kwa sababu kuna site moja nimewahi kuitembelea solar panels na battery za kutosha lkn umeme ukikatika zikijitahidi saana ni masaa tu. ndio maana nimeuliza maana wakubwa huko duniani huwa hawashindwi kitu, ukute zipo sinazopiga kazi mwaka mzima bila kuchoka kwa gharama ndogo au kuna option zaidi wadau wakatufumbua macho.
 
Ukubwa wa ghalama za umeme jua( solar power) hutegemeana na ukubwa wa vifaa vinavyotumia umeme huo.
Kitu muhimu tunachopaswa kukitizama katika suala la usimikaji wa nishati fulan iwe ni umeme jua, umeme wa tanesco au chanzo chochote cha nishati kwaajili ya matumizi ya majumbani ni ghalama halisi za usimikajii wa hiyo nishati husika(installation cost) na ghalama za uendeshaji wa chanzo hicho cha nishati(running cost).
Kwa kawaida ghalama ya usimikajia wa umeme wanishati jua huweza kuonekana ni wa ghali kidogo kwa hapo awali lakini baada ya hapo ghalama za uendeshaji ni ndogo sana na wakati mwingine ni kama hakuna,Pia wewe ndio unakuwa mmiliki wa huo mfumo wa umeme jua utakao ufunga, utakachotakiwa wewe kama mtumiaji ni kuzingatia kila baada ya mda flan unafanya checkup mfano kutizama wire connections, kutizama battery connections nk.
Kitu kikubwa katika umeme jua ni kwamba mfumo ukifungwa kwa kutumia vifaa halisi na wataalam wa umeme jua huwa ni wa uhakika sababu jua lipo kila siku na nika bure.

Kwa suala la umeme wa tanesco sina taarifa halisi za usimikaji(installation cost) ila ghalama za uendeshaji( running cost) hizo huwezi kuzikwepa ambapo mojawapo ni malipo ya LUKU kila muda kulingana na ukubwa wa matumiz yako.
Kumbuka ili tuweze kujua kwamba chanzo fulani cha nishati ni fanisi kulingana na matumizi ya kila siku tuliyonayo kinachoangaliwa sana huwa ni ghalama za uendeshaji wa chanzo cha umeme chaguliwa baada ya kusimikwa.(running cost after installation)
 
Utaanza kuambiwa nunua friji yya solar,tv ya solar mara nini sijui cha solar....solar sio umeme tuliouzoea
Hakuna ulazima wa kununua upya kila kitu kitumiacho solar mkuu labda ukiitaji iwe hivo.
Kwa mtu ambaye tayari yupo katika mfumo wa umeme wa tanesco na tayari anavifaa vitumiavo AC current kunakifaa hufungwa wakati wa installation kina itwa inverter hichi ndio hufanya kazi ya kubadili DC current kwenda AC current kwaajili ya matumizi ya vifaa vilivyokuwa na vinavyotumia umeme unaotolewa na tanesco
 
Ila ninavyojua Mimi umeme wa Solar una limit yake ya muda kwa maana kwamba muda flani ukifika hutaweza kutumia tena hyo solar mfano Solar zingine zinachukua miaka 25 solar zingine Miaka 10 lakini umeme wa Tanesco hauna Limit yake utatumia mpaka utauacha
 
Hakuna ulazima wa kununua upya kila kitu kitumiacho solar mkuu labda ukiitaji iwe hivo.
Kwa mtu ambaye tayari yupo katika mfumo wa umeme wa tanesco na tayari anavifaa vitumiavo AC current kunakifaa hufungwa wakati wa installation kina itwa inverter hichi ndio hufanya kazi ya kubadili DC current kwenda AC current kwaajili ya matumizi ya vifaa vilivyokuwa na vinavyotumia umeme unaotolewa na tanesco
Unaweza kunipa gharama ya kufunga solar itakayoniwezesha kutumia vitu vyote vya umeme kama nitumiavyo umeme wa tanesco
Tv,friji,taa,ac unlimited
 
Back
Top Bottom