Elections 2010 GHARAMA YA KURA.... Khanga + T-shirt + kofia + pilau = ???? Mtihani huo!

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Hivi mwananchi anapopokea tshirt na khanga anatarajia kiongozi aje amfanyie lipi zaidi atakapochaguliwa?
Ni nini kitambana kutumikia wananchi ilhali alichaguliwa kwa bei?
Hivi mwananchi unanunuliwa kwa kipande cha kitambaa?
Maendeleo yatapatikana vipi kama wananchi wanakula kabla ya kutoa Kura?

TAKUKURU wana kazi ya ziada... rushwa ziko za aina nyingi sana siyo lazima pesa, siyo lazima mtu agawe tshirt na khanga au baiskeli hadharani. Wanaokamatwa ni wale wenye bahati mbaya tu..wako wengi wanafanya vitu vyao kama kawaida bila hofu kabisa....

Wapo wanaotumiwa kwenye account za bank, wako wanaotumiwa kwa M-Pesa... hawa watakamatwa vipi?
 
Kwanini wailipie?
wanailipia kwa faida ya nani?


Wanalipia kwa mengi:
1. Wananchi wana matatizo kuanzia ya basic needs ( chakula, mavazi etc) hadi mengine....na hii inatuambia kuwa viongozi wana kazi kubwa kweli! Kama mwananchi anaweza kuridhika kwa mlo wa siku moja na kusubiri tena miaka mingine mitano hatuoni kuna tatizo kubwa zaidi ya tulionalo?

2. Kama uongozi haujaweza kuwafanya wananchi waweze kutatua abject poverty na sasa ni miaka karibu 50 tangu nchi ipate uhuru , itatuchukua miaka mingapi zaidi?

Ningetamani kujua wanaowania uongozi au hata walioko madarakani wanatafsiri vipi hali hii? Je isingewasaidia kuweka mikakati mizuri zaidi ya kuwasaidia wananchi? Nadhani au ingekuwa mimi ndio naingia madarakani, ningefanya utafiti mdogo kuona ni maeneo yepi wananchi wanazinguliwa na khanga na t-shirt na pilau na kuweka strategy ya kuwamalizia kiu hii kwanza ( sic!)... mipango ya maendeleo huenda ingechukua sura mpya. Badala ya kuwa na mipango yenye kuhitaji mabilioni huenda ingehitaji mamilioni machache tu...
 
well.. lakini kama kura zina gharama kwanini wananchi wasiilipie?

Kura zina gharama kubwa sana........... vinginevyo watu wasingehaha kuzunguka huku na huko kuhonga....

na Kura zinazopatikana kwa hongo, gharama yake ni kubwa zaidi kwa mwananchi anayetegemea maendeleo!
 
Hiyo formula ina-aply kwa siku moja tuu..miaka 5 yoote ni shida...
 
Hiyo formula ina-aply kwa siku moja tuu..miaka 5 yoote ni shida...

Usipokula pilau usipopokea kanga usipopokea kofia mgombea atapita na miaka mitano itapita hupati barabara maji ya kunywa hata lifti, so the least you can get ni kofia, kanga na pilau.
 
I gues wengi wetu humu ndani mmewahi kutembea vijijini.
Nasema vijijini nikimaanisha vijiji kweli!
Kule utakuta m2 anavaa fulani moja miaka na miaka,
Ukaenda sasa hivi ukampa fulana mpya atakuona wewe kama mkombozi.
Na kura utapewa bila kupingwa!!
Swali Langu ni kwamba. Mbona sijaona T-shirts za CHADEMA?
in maana
wao tu ndo wenye uwezo wa kugawa fulana na kofia?
 
I gues wengi wetu humu ndani mmewahi kutembea vijijini.
Nasema vijijini nikimaanisha vijiji kweli!
Kule utakuta m2 anavaa fulani moja miaka na miaka,
Ukaenda sasa hivi ukampa fulana mpya atakuona wewe kama mkombozi.
Na kura utapewa bila kupingwa!!
Swali Langu ni kwamba. Mbona sijaona T-shirts za CHADEMA?
in maana
wao tu ndo wenye uwezo wa kugawa fulana na kofia?

Chadema wanatakiwa kutoa Tshirts zikiwa kimkakati zaidi, hakuna haja ya kumpelekea poster ya shilling elfu tano au tatu mtu wa kijijini!, huyu mpatie tshirts yenye maneno mazito ya kumhamasisha apigie kura Dr Slaa na wabunge wake, hii itakuwa ni win-win stuation, umepata kura na yeye amepata t-shirt, kwa sisi tunaotembelea vijijini sana tunajua kwamba watanzania wanavaa tshirt za kijani kwa sababu hawana alternatives ya mavazi.
 
Kwa hiyo..ina maana T-shirt na khanga ( mavazi ) ndio kipaumbele cha kwanza katika matatizo ya watanzania walio wengi? Nimetoa hii changamoto nikitaka tujaribu kuangalia beyond the image ya khanga na pilau... nchi yetu basi haiweki vipaumbele sahihi katika kutatua matatizo ya wananchi?
 
Back
Top Bottom