Gharama ya kununua Radi huko Rukwa ni Tsh ngapi? Je, naweza fanyiwa Delivery?

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
Huyu jamaa amekuwa akinifuatilia muda mrefu sana. Jumamosi kidogo nimchane na risasi pajani.but tukayamaliza. Leo nmekuta anaendelea kunipikia majungu.

Ni muda mrefu nlimwambia majungu si mtaji.lakini naona kawekeza sana kwenye hayo. Jamaa ana roho ya kichawi kabisa.yaani hivi mnacheka naye lakini ukigeuka tu anakusema vibaya sana.baadaye atakupigia simu akikuita bro n.k

Nlishamwambia apite kushoto nipite kulia ila naona haelewi.nmeona tusigawane majengo ya serikali.nirudi kwenye asili yetu.

Rukwa aka Sumbawanga nasikia wanatengeneza RADI. Radi zao hazitegemei msimu wa mvua. Je kuna mtu anafahamu gharama zake? Mi staki ile radi grade 1 ya kuua kabisa.

Hapana. Nataka ya kumchania chania nguo zote mbele za watu na kumgaragaza chini kinyama...kumpa michubuko mwili mzima.je kwa radi hiyo itakuwa Tsh. ngapi?

Pia nataka nijue kama nikinunua ni lazima niifate kiwandani au wanaweza ituma kwenye magari ya mikoani au posta?

Ushauri wangu pia. Kama wanaweza wangefungua vituo huku kuwe na agents wao ili tuwe tunapata hizo radi kirahisi tu kuwatumia watesi wetu.hii itatuondolea hbr ya kufuatilia kesi na kuwekwa ndani.

WALIOKO SUMBAWANGA/RUKWA MKOA. PLEASE NAOMBA MSAADA WENU.MNIPE BEI NA PIA NAMNA YA KUPATA HIYO BIDHAA.ASANTENI.
 
Mimi nauza mamba, atamtokea kwenye beseni la maji akiwa bafuni anaoga, au atatoka ndani ya bilauri anayonywea maji..mamba atampa adhabu ndogo tu ataondoka na mkono wake mmoja. Kama uko tayari karibu hapa hapa kibarazani tuyajenge.
 
Mkuu natamani Radi... Hii impige mchana wa jua kali. Tena akiwa posta katikati ya watu mpige mpaka achakae.

Mimi nauza mamba, atamtokea kwenye beseni la maji akiwa bafuni anaoga, au atatoka ndani ya bilauri anayonywea maji..mamba atampa adhabu ndogo tu ataondoka na mkono wake mmoja. Kama uko tayari karibu hapa hapa kibarazani tuyajenge.
 
Daah inawezekana nmetaka mzigo kipindi bei ipo juu?sure nataka iwe customized. Sema 760,000 parefu sana ndugu yangu. Kama una jamaa unamfahamu ashushe bei na pia kama akifanya bei nzuri mi naweza nikawa hata wakala wake huki Dar.najua wengi wanahitaji.tena umesema vyema kipindi hiki cha uchaguzi watu wanaweza tumiana hata kwenye kampeni.

Mwaka huu wa uchaguzi bei inapanda sana, maana wanasiasa wanazitafuta sana kupambana na wapinzani wao.

Kama hiyo unayoitaka, tunaweza kukufanyia kwa 760,000. Maana inahitaji customization.
 
Back
Top Bottom